M-sure....

Hivi M-sure maanake nini? Nauliza hivi kwasababu kuna vijana around my office wananiita m-sure hata around my neighbourhood vijana wengine wananiita m-sure. Ni vijana nimewazidi miaka 10 au 15 hivi.

Utawasikia m-sure mamabo vipi? Au m-sure heshima yako?

Enzi mimi nakua m-sure tulikuwa tunamuita baba. Sasa ina maana mimi nalingana na baba zao hawa vijana au m-sure ina maana gani? Im over 30!
mzee wa bishoo
 
Hamjanipa jibu m-sure ni mtu wa aina gani? Mzee? Au?
1. Mwanaume wa makamo
2. Mwanaume anayejiweza kimapato
3. Asiyejisikia na anayejichanganya na rika zote
4. Anayetoa vimsaada kwa wenye mahitaji
5. Asiye na kashfa kama ujambazi/umalaya nk
 
1. Mwanaume wa makamo
2. Mwanaume anayejiweza kimapato
3. Asiyejisikia na anayejichanganya na rika zote
4. Anayetoa vimsaada kwa wenye mahitaji
5. Asiye na kashfa kama ujambazi/umalaya nk
Hapo nawaelewa sasa.
 
Inahusu pia kama huna tatizo kwenye malipo na ishu za pesa
timu ya mtaani ikija na mchango wa jezi unatoa tu fasta

jirani kuna msiba...mchango uko fasta

fundi anafyatua matofali hubishani malipo sana
unalipa in time...


Sometimes utasikia 'jamaa mzungu sana'
yule m sure hana shida....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom