Lowassa acha kuhadaa Watanzania, sema ukweli wako juu ya kuchukia umasikini

Magamba mna shida ya kutofikiri. Kama Lowasa ni tajiri haina maana utajiri wake ni wa kufanya kazi za serikali. Nashanga sana wanavyotag nchi kwa mtu badala ya serikali. Serikali ya CDM na Ukawa ndio itaondoa umaskini. Lowasa atasimamia tuu. Kusema ataondoa umaskini sio kugawa hela kama Magufuli anavyodai atagawa m 50 kwa kila kijiji.
Mbona hata JK ni tajiri lakini waswahili wa Msoga ni maskini sana?
 
Maskinini hawezi kwenda ikulu!

Na tajiri hawezi kuuona ufalme wa Mungu (tunaambiwa Mgombea ni Chaguo la Mungu). Kama wewe ni muumini wa Kristu soma Luka 6:20-27, ila hapa nitanukuu MISTARI michache tu kama hivi:

24 Lakini, ole wenu ninyi mlio na mali, kwa kuwa faraja yenu mmekwisha kuipata.

25 Ole wenu ninyi ambao mmeshiba sasa, kwa kuwa mtaona njaa. Ole wenu ninyi mnaocheka sasa, kwa kuwa mtaomboleza na kulia.

26 Ole wenu ninyi watu wote watakapowasifu, kwa kuwa baba zao waliwatenda manabii wa uongo mambo kama hayo.

TAFAKARI, CHUKUA HATUA.
 
Ili kuendelea tunaitaji watu wenye kuweka mfumo endelevu wakufikiria zaidi kuhusu maisha yetu ya sasa na baadae.kuwepo mfumo mzur wenye dira yakukomboa Taifa kutoka katika umaskini.Mfumo huo uwe ni wakitaifa na sio wachama.

Imezikwa siasa ya ujamaa na kujitegemea na mafisadi. Hata miiko ya uongozi kwenye Katiba pendekezwa imeparaza tu.
 
Hahaha ,labda angeiga akina Mrema ,alipewa cheo cha unaibu waziri mkuu ,alijipendeleaje kwao,barabara hadi nyumbani kwake ,akina Daniel Yona na Basil Mramba walijaza WACHAGGA TRA,hadi wafagizi wachagga ,jenga sana kasakzini ,usimtaje Sumaye ,Mama Anna Mkapa kupitia mfuko wa fursa kwa wote WachaGGA walipiga sana hela ,ndo maana tunaogopa ukaskazini na ukawa ,na uchagga,na ulutheri.
 
Ebu tuma na attachment za picha za uko monduli ili tujionea atujawahi kufika wengine
 
Uko sawa sawa mkuu; kwa kweli nakereka na aina hii ya viongoz; Nakumbuka nikifanya shughuli fulan huko jimbon kwake ilikua inanipasa kusafir na maji toka arusha mpaka lt 500 kwenye gar kuwapatia wale tutakaowatembelea kwa kias kichozid lt 5 kwa kaya.
Cha ajabu wakina mama wakitoka na punda kufata maji alfajir sana wanarud sa tisa au zaid ya hapo.
Tena wanarud na maji yenye rangi ya udongo kwani ni mabwawa wanayokunywa ngombe ndiko nao wsnaponea.
Imagine na kweli huezi amin ukimnawisha mtoto wa kimasai mkono hapo kijijin utarud after 2 wks ndo atabahatika kunawa tena. Leo tunadanganyana eti umaskini hapend!!!!!!
wanasiasa ni watu wabaya sana lowasa anawatenda watu wake vibaya kuliko ngombe wake mwenyewe leo hii anagawa mamilion kila kona wakat angalau kila kijiji kingeeza kua na kisima kimoja cha kuchimba!!

Mkuu usemayo ni ukweli tena ukweli mtupu kama sio mkubwa, ILA najua wapo humu ndani mabingwa WA kutukana watakutukana na kukwambia umetumwa, ILA ukweli ndio huo monduli hakuna maji/hakuna mradi wowote WA maji wananchi wanategemea mabwawa tena yenyewe ya msimu wanaoenda kutafuta maji kwa punda ndoo moja ni tsh 500 mpaka 1000 na ukiona mtu anabisha ujue hapajui au hajawahi kufika wilaya au jimbo la monduli Kule ni shida shida shida tupu hakuna miondombinu yeyote huko sijui miaka yote 30 Huyu jamaa alikuwa anapeleka Wapi mgao WA jimbo lake duuu
 
Vipi utajiri wa nchi nzima na umasikini wa wananchi wake? Angeendeleza sana kwake mungesema anapendelea kwao. Tusilete tafiti zaki shabiki hapa. Wewe ukiwa na hela ndo unalisha majira wako wote? Mbona ww hata kutoa mia kwa ombaomba unashindwa. Tafakari kabla yakuleta uzi hapa. Ni jimbo gani nchi lipo juu ya majimbo yote? Shida ya maji, umeme ni nchi nzima. Ndo maana nijuku la REA ku hakikisha umeme una fika vijijini, ni jukumu la wizara ya maji kwamba maji yanapatikana nchi nzima.Mbona kwao kwa rais maji na umeme nitabu tuu. Sasa tumpe usukani awe namaamuzi ya nchi na mgawanyo mzuri wa resources za nchi, sasa hapo unaweza ku mpima kama anaweza au laa. Usishangae alikua ana omba mgao lakini alikua hape. Jiulize nchi ina deni trioni 31, maji, umeme, elimu, afya etc, ni hovyo hela zilienda wapi? Ccm hawana jipya lakutusanganya tena.


Mpendwa najua unampinga mleta maada ni kwakuwa sijui monduli hupajui Kule ni shida eti wee, kama ni hivyo mbona mh nassari amekaa bungeni miaka mitano tu jimboni kwake hakukuwa na maji saahivi yapo kwakweli kwa mtu anayeleta maendeleo siasa weka pembeni Lowassa ni mzingo utajiri wake hauna manufaa kwa wananchi wake hata akiwa Rais tarajia hayohayo yaliyopo jimboni kwake
 
Nimezunguka karibu jimbo zima la Monduli. HAKUNA MAJI, UMEME, VYOO,Kuna Umasikini wa kutosha! Nimepita Eslalei, Mswakini, Mbuyuni, Nanja, Mti mmoja, Losimingori hali ni mbaya.

Najiuliza huyu lowassa anayegawa mapesa nchi nzima anashindwaje kuendeleza jimbo lake?

Kipimo cha umaskini ni nini? Kikwete bagamoyo wamekuwa kama London , chato kwa magufuli ni kama Washington DC, Mtwara kwa Ben mkapa ni sawa na......malizia
 
Yeye kama kiongozi nilitarajia angejenga ata viwanda vya kusindika maziwa pia vya kutumika mazao ya mifugo ie kwato,ngozi,pembe etc

Anyway labda tumpe uraisi atakumbuka ilo
 
Nimezunguka karibu jimbo zima la Monduli. HAKUNA MAJI, UMEME, VYOO,Kuna Umasikini wa kutosha! Nimepita Eslalei, Mswakini, Mbuyuni, Nanja, Mti mmoja, Losimingori hali ni mbaya.

Najiuliza huyu lowassa anayegawa mapesa nchi nzima anashindwaje kuendeleza jimbo lake?
Umepasahau Mguu wa Zuberi!
 
Eti mtu huyo anataka aondoe nyumba za nyasi Tanzania, Jimbo lake kama mfano tuu hali taabani, huyu bwana asituadae na neno mabadiliko! kwanza mabadiliko gani anaongelea maana mabadiliko ni neno pana. EL hachukii umaskini anachukua maskini ndo maana jimbo lake lipo hivo na mradi wa maji pia alipiga pesa akaacha watu wake wakishirikiana maji na mifugo. Huyo Hapana kwa kweli.
 
Nimezunguka karibu jimbo zima la Monduli. HAKUNA MAJI, UMEME, VYOO,Kuna Umasikini wa kutosha! Nimepita Eslalei, Mswakini, Mbuyuni, Nanja, Mti mmoja, Losimingori hali ni mbaya.

Najiuliza huyu lowassa anayegawa mapesa nchi nzima anashindwaje kuendeleza jimbo lake?

Umeshindwa kujua Tanzania na utajiri wake lakini wananchi wake tunaishi katika dimbwi la umasikini na unashindwa kuiuliza ccm ni kwa nini? Bali unakaa kueneza unafiki wambie waliokutuma bado hatudanganyiki tena jipange upya.
Hapa ni Lowasa tu
 
Back
Top Bottom