Benson Mramba
JF-Expert Member
- Oct 29, 2013
- 668
- 1,522
Kwenye siasa kuna kitu kinaitwa dhana, kura za makurdi, na mtazamo wa makurdi. Kwa kiongozi yoyote ni lazima uwe makini sana kwenye mambo haya.
Juzi Mzee Paul Kimiti akiwa kwenye Kongamano la Mwalimu Nyerere Dodoma alisema kuwa Mzee Mkapa alikuwa ameshamteua awe Waziri Mkuu lakini Mwl Nyerere alimkataza na kumwambia kama unampenda Kimiti mpe kazi nyingine hamuwezi kujazana Wakatoliki watupu.
Kwa sasa Tanzania tuna Rais Mzanzibar, bahati mbaya kwa mujibu wa katiba yetu ni kuwa Rais huyu ni kama vile ni Rais wa Tanganyika zaidi maana Zanzibar wana Rais wao tayari.
Hivyo basi dhana na mitizamo ya Watanganyika dhidi ya Rais huyu ni vya kujihami zaidi. Hivyo Rais anapaswa kuwa makini dhidi ya mambo na matukio yote yanayoweza kuibua mitizamo hasi dhidi ya pande zetu mbili za muungano.
Matukio kama ya kuuzwa kwa bandari zetu, kutekwa na kuuawa bila kauli za kulaani au kubariki toka kwa Rais, kubambikia kesi zisizo na dhamana viongozi wetu wapendwa wa kisiasa mfano ugaidi, uhaini n.k, kuzuia tume huru, kujipitisha kuwa mgombea pekee wa Urais wa Tanzania/Tanganyika kwenye vikao vya chama tawala, kufumbia mambo ripoti ya CAG n.k ni hatari kwa muungano wetu maana zinaweza kushamiri dhana za Mzanzibari dhidi ya Watanganyika.
Historia inaonyesha hata Mzee Mwinyi alipotoka Kisarawe kwenda kuongoza Zanzibar alipata tabu sana hata leo mwanawe na mtoto wa Mzee Karume bado wanachuana huko.
Tuzibe ufa kabla hatujatakiwa kujenga ukuta