Lissu: Magufuli ameahidi kuwa sheria za madini zitarekebishwa kufuatana na mapendekezo ya kamati

Tundu Lissu aache kupotosha.

Hiyo ilikuwa imeandikwa ndani ya hotuba ya budget kabla ya mapendekezo ya Kamati ya pili ya kuchunguza sheria na athari za kiuchumi kutokana na sekta ya madini haijatolewa kwa Rais.

Badget imesomwa kabla ya mapendekezo 21 ya kamati ya Prof. Nehemia Osoro hayajatolewa na kukubaliwa na Rais.

Waziri wa sheria na Katiba leo amesema taasisi/watu wajiandae kutoa mapendekezo kuhusu sheria za madini na gesi.
 
Nieleweshe mkuu
Sikitiko la Lissu hapo, nikiasi cha pesa kinacho ongeza
kwamba bado ni kidogoo, ukilinganisha na vile wengi tulivo dhani kitaongezeka,,
maana io asimia 1, nikwamba wao awa acacia wakipata laki moja, 100,000/= yetu sisi iliyo ongezeka (inspection fee) ni shilingi 1000/= tuu
 
Tulijua tangu mwanzo kuwa ni kick za kisiasa zaidi kuliko hiyo mikataba. Kama walioidhinisha mambo hayo hawatakiwi hata kutajwa majina. Kelele za nini sasa?!!

Tusubiri labda huruma ya barick
Ni mwendo wa Dili juu dili wenzake walikula kwa mbinu zao sasa kaamua kuwakingia kifua baada ya kumlalamikia na yeye kaamua kuwapiga mikwara wazungu waandae mikataba mipya apige chake na yy apate pesa za kujenga uwanja wa ndege chato kisha asingizie ni wafadhili wamejenga kwa pesa zao.
 
Hicho kifungu kinazungumzia uanzishwaji wa werehouses kwa ajili ya ukaguzi na usafirishaji wa dhahabu nje inchi na kupiga marufuku usafirishwaji wa dhahabu direct kutoka migodini...na kua ada ya ukaguzi huo ktk izo warehouse itakua ni 1% ya thamani yote ya dhahabu itakayosafirishwa...hii itaondoa utoroshwaji wa dhahabu unaofanyika kutokana na migodi kua na viwanja vya ndege vya kusafirishia dhahabu nje...haya mapendekezo ya bajeti yalitolewa b4 ht tume ya pili haijatoa mapendekezo yake ila naona Tundu Lissu ameamua kutoa maelezo finyu ili kuupotosha Uma...Uma usiotaka kuchimba zaidi kujua hicho kifungu kinasemaje kwa ujumla wake ila wakawa wepesi wa kuponda na kulalamika....Uma wa WADANGANYIKA
 
Kwaiyo tumpe nchi Lisu eti ee?
Subiria Msukuma ajenge kwao chato kwanza kwani huenda makao makuu ya kanda ya Ziwa yakawa chato watalii wengi watatua chato kabla ya kwenda Serengeti kupitia Simiyu ni mbinu ya kuukuza mji wa chato kwa kasi kubwa, kwa sasa ni Dili faster faster alianza na vibali vya sukari, mabenk kurejesha nguvu BOT, safari za nje kupunguzwa, kubana matumizi, ununuzi wa ndege, ujenzi wa reli na sasa ukarabati wa bandari na madini zote ni Dili kapiga pesa kwa mda mfupi mpaka ajui azifanyie nini.
 
Mweka hazina binafsi wa mkulu ni Daud Bashite kwa sasa anaenda kuwa tajiri mkubwa kwani na yy baadhi ya pesa anazizungusha zinazaa ni mwendo wa kufa kufaana wazungu wanachachawa lakini mkulu na wenzake wananufaika huku wananchi wakiambulia kidogo sana tena sana.
 
Ameandika tena Lissu

"....Wajameni habari za usiku.

Wakati Jemedari Magufuli ameahidi juzi kuwa sheria za madini zitarekebishwa kufuatana na mapendekezo ya Kamati ya Prof. Osoro, leo serikali imewasilisha bungeni Muswada wa Sheria ya Fedha, 2017.

Muswada huo unapendekeza marekebisho ya sheria mbali mbali za kodi pamoja na Sheria ya Madini, 2010.

Kuhusiana na Sheria ya Madini, serikali hii inayotaka kulinda rasilmali zetu zisiibiwe tena na wezi wa kimataifa, inapendekeza kuweka kodi mpya kwa makampuni ya madini.

Kodi hiyo inaitwa 'ada ya ukaguzi' (inspection fee) ambayo itakuwa sawa na 1% ya thamani mauzo (gross value) ya madini husika nje ya nchi.

Kwa hiyo, baada ya kelele zote za wazalendo mamboleo hawa, hayo ndiyo marekebisho pekee wanayopendekeza kwenye Sheria ya Madini ambayo imepigiwa kelele ya kufa mtu kwa kutusababishia hasara ya matrilioni ya faranga.

Need I say more???...."

Tundu Lissu


Nafikiri huyu jamaa anatatizo kichwani hayo mapendekezo ya asilimia moja yalipangwa kabla ya sakata hili la machanga, baada ya sakata hili camander Magu Alisema kila mwenye akili timamu alimsikia kuwa sasa itabidi ifumiliwe sheri yote ya madini pamoja na mikataba ipendekezwe sheria mpya ya madini sio marekebisho, kamati ikisha pendekeza ipelekwe bungeni ikibidi siku ziongezwa za bunge, sasa huyujamaa naona kama vile kachanganyikiwa, wala haelewi anachosema hiyo ni sheria ya kodi ya ukaguzi ilio letwa na wizara ya fedha wala sio sheria ya madini !!!! vp?
Pia naona huyu Tindulisu naye ni Bashite huyu
 
Upumbavu unaangamiza mataifa!.

Hivi kuna siri gani kaika hii mikataba hadi isije kujalidiliwa bungeni?

Kwa nini watu wachache ambao ndio wanaangamiza uahi wa nchi, wajifungie ndani na kufanya marekebisho ya 1%?

Taifa linaweza kuwa mali ya mtu mmoja, wengine ni wafugwaji wake? Ni wafugwaji wa mmtu mmoja au ni mbwa koko wanaoishi ili mradi wako wanapumua?

Tatizo la CCM na watu wake wote ni kubwa sana. Siku zote wamekuwa wakiteka agenda za UKaWA ili kutafuta umaarufu lakini uwezo wala upeo wa kuzitekelza hawana na wanaishia kuharibu. Wanasimama na kusema tumetekeleza hili huku wamevurunda tu kwa kuwa ni wap..u.mb.vau ambao hata kuuliza kwa wenye agenda namna gani wafanye hawajui.

Llichama hili ni la kulimaliza! Mungu wasikie watu wako wanaoombea taifa!


Ameandika tena Lissu

"....Wajameni habari za usiku.

Wakati Jemedari Magufuli ameahidi juzi kuwa sheria za madini zitarekebishwa kufuatana na mapendekezo ya Kamati ya Prof. Osoro, leo serikali imewasilisha bungeni Muswada wa Sheria ya Fedha, 2017.

Muswada huo unapendekeza marekebisho ya sheria mbali mbali za kodi pamoja na Sheria ya Madini, 2010.

Kuhusiana na Sheria ya Madini, serikali hii inayotaka kulinda rasilmali zetu zisiibiwe tena na wezi wa kimataifa, inapendekeza kuweka kodi mpya kwa makampuni ya madini.

Kodi hiyo inaitwa 'ada ya ukaguzi' (inspection fee) ambayo itakuwa sawa na 1% ya thamani mauzo (gross value) ya madini husika nje ya nchi.

Kwa hiyo, baada ya kelele zote za wazalendo mamboleo hawa, hayo ndiyo marekebisho pekee wanayopendekeza kwenye Sheria ya Madini ambayo imepigiwa kelele ya kufa mtu kwa kutusababishia hasara ya matrilioni ya faranga.

Need I say more???...."

Tundu Lissu
 
Back
Top Bottom