DOKEZO Lissu aondolewa Keko. Anapelekwa wapi?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Tundu Lissu has just been collected by official motorcade from the Keko prison.

Not so sure where exactly is he being taken

———
UPDATE:

My insider indicates that he has been moved to Ukonga

3386da84-07e9-4adf-b04d-288328fb52e8.jpeg


TUNATAKA KUJUA ALIPO MHE TUNDU LISSU
Leo Ijumaa, Aprili 18, 2025, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Wakili Ali Ibrahim Juma, Mawakili, Familia, na wanachama kwa nyakati tofauti, wamefika katika Gereza la Keko ambapo Mwenyekiti wa Chadema, Mheshimiwa Tundu Lissu anashikiliwa.

Hata hivyo, juhudi zao za kumuona Mhe. Lissu hazikufanikiwa baada ya kuelezwa kuwa hayupo katika gereza hilo, cha kusikitisha, hawakupewa maelezo yoyote rasmi juu ya alipopelekwa.

Chadema tunalitaka Jeshi la Magereza, mamlaka husika na vyombo vya dola kutoa taarifa wazi na za haraka kwa umma kuhusu mahali alipopelekwa Mhe. Tundu Lissu. Iwapo bado anashikiliwa katika Gereza la Keko, ni haki ya familia, viongozi na wanachama kumuona - ni haki ya msingi ya kibinadamu na kikatiba.

Imetolewa leo Aprili 18, 2025
Brenda Rupia
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi

===========================

KAULI YA MSEMAJI WA JESHI LA MAGEREZA

JamiiForums imewasiliana na Msemaji wa Jeshi la Magereza, Elizabeth Mbezi kuhusu taarifa hizo ikidaiwa Lissu amehamishwa gereza, amesema “Bado sijazipata hizo taarifa”.

Alipoulizwa kama kuhamisha Watuhumiwa na Wafungwa ni siri, amesema: "Inategemea na makosa, yapo makosa wanahamishwa kwa siri na yapo makosa hawahamishwi kwa siri."

Alipoulizwa kuwa kuhusu tuhuma za Lissu ni kati ya ambazo zimo kwenye lista ya kuhamishwa kwa siri amesema "Ngoja nifuatilie kwanza."

Pia soma Pre GE2025 - DSM - Rose Mayemba: Tumetoka Keko, Lissu hayupo na Magereza hawajui alipo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom