Lembeli amsifu Rais Magufuli kwa kazi nzuri, Rwakatare awapinga CHADEMA kuhusu kuibiwa wa kura

Hili limetokea siku mbili tu baada ya mbunge wa Moshi mjini kumuunga mkono Magufuli kwa hatua anazozichukua.
 
Kuna makamanda-Asili ( Hawa ni CDM damu, na kuna baadhi yao hadi ndugu zao wamepata misuko suko mikubwa katika kutetea haki) hawa wanamkubali Magu kimya kimya, na hawakupenda ujio wa Lowassa. Kuna Makamanda-Lowassa ( hawa hawaijui CDM vizuri, wao kwao ni maslahi mbele, hawajawahi kupata misukosuko yeyote kwa ajili ya chama) hawa ndio wanamtukana Dr Slaa kila siku, lakini ni wakali kweli kweli Lowasa akiguswa ( Hoja yao kuu apelekwe mahakamani, wakiulizwa mbona mnawaita baadhi ya watu mafisadi ilhali hawajapelekwa mahakamani? wanapiga kimya).

Hongera Rwakatare
Makamanda asili ndio mimi hapa.Nataka chama kirudi kwenye misingi ya awali ya kupinga ufisadi hadharani bila kubagua mafisadi kwa vyama.Sipendi kuwekwa kundi moja na hawa wahuni wa " ulipo tupo".
 
Back
Top Bottom