Lembeli amsifu Rais Magufuli kwa kazi nzuri, Rwakatare awapinga CHADEMA kuhusu kuibiwa wa kura

Mkuu labda nikujuze kitu kimoja ambacho inawezekana hata wewe hukijui. Lakini kwa mimi ninaye ijua vizuri Ccm nitakuambia hivi; CCM HUWA HAWAIBI KURA, BALI WANAIBA MATOKEO. Mfano jimbo la Newala mkoani Mtwara, matokeo ya kura zote zilizohesabiwa zinaonyesha Ndugu Manguya wa CHADEMA alishinda Kwa zaidi ya kura elfu 36 dhidi ya Mkuchika wa CCM. Alichokifanya Mkurugenzi ni kuhamisha matokeo ya Manguya na kumpa Mkuchika na kisha kumtangaza mshindi.
UNAJUA SISI MAKAMANDA WA CHADEMA TUNA HULKA MOJA TU.ILI IONEKANE UCHAGUZI ULIKUWA HURU NA HAKI NA HATUKUIBIWA KURA NI LAZIMA TUMESHINDA SISI.IKITOKEA HATUJASHINDA BASI TUTAKUWA TUMEIBIWA MATOKEO NA CCM.CCM WAKISHINDA ------WAMEIBA KURA,ACT WAKISHINDA----WAMEACHIWA JIMBO NA CCM NA SISI MAKAMANDA TUKISHINDA-----NDIO TUMESHINDA KIHAKI.PIPOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
 
Hoja hizo ndizo zilizopingwa na LWAKATARE, tena aliuliza, kama CCM wanaiba kura au matokeo vyovyote utakavyoita, yeye alipataje ubunge?
Unafikiri kwanini Zanzibar tume haikutangaza matokeo ya uraisi na kuamua kuufuta uchaguzi? Unahisi kwamba matokeo ya uchaguzi ule yangekuwa yako upande wa Ccm wangefuta uchaguzi.
 
UNAJUA SISI MAKAMANDA WA CHADEMA TUNA HULKA MOJA TU.ILI IONEKANE UCHAGUZI ULIKUWA HURU NA HAKI NA HATUKUIBIWA KURA NI LAZIMA TUMESHINDA SISI.IKITOKEA HATUJASHINDA BASI TUTAKUWA TUMEIBIWA MATOKEO NA CCM.CCM WAKISHINDA ------WAMEIBA KURA,ACT WAKISHINDA----WAMEACHIWA JIMBO NA CCM NA SISI MAKAMANDA TUKISHINDA-----NDIO TUMESHINDA KIHAKI.PIPOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Mkuu, hakika huu ni ukweli ambao unapaswa kusemwa waziwazi. Namshukuru sana Lwakatare kwa kusema ukweli
 
Unafikiri kwanini Zanzibar tume haikutangaza matokeo ya uraisi na kuamua kuufuta uchaguzi? Unahisi kwamba matokeo ya uchaguzi ule yangekuwa yako upande wa Ccm wangefuta uchaguzi.
Hivi kama hoja ndo hizo, makamanda mngeshinda kule Kawe, Kibamba, Ubungo, Temeke na Ukonga?
 
Ndiyo maana siku zote nasema Kauli ya Mbowe ya kupingana na utumbuaji majipu ni yake binafsi kwa sababu zake binafsi na siyo msimamo wa Chama. Msimamo wa Chama ni kuunga mkono utumbuaji wa majipu tangu ile kauli ya awali kabia ya kuwa Magufuli anatekeleza iani ya CHADEMA.
 
huo ndiyo ukweli.
 
Ni kweli kabisa Mkuu. Mbowe kwa sasa amebaki na fisadi wake Lowasa tu
 
Hivi kama hoja ndo hizo, makamanda mngeshinda kule Kawe, Kibamba, Ubungo, Temeke na Ukonga?
Unafikiri bila kukomaa maeneo tajwa ushindi kwa wapinzani ungepatikana? Jiongeze mkuu, usitake kuleta ubishani usio kuwa na tija. Unakumbuka wakati wa uchaguzi JF ilikuwa hacked? Unajua ni nani walifanya huo mchezo mchafu na ni kwanini?
 
Mkuu labda nikujuze kitu kimoja ambacho inawezekana hata wewe hukijui. Lakini kwa mimi ninaye ijua vizuri Ccm nitakuambia hivi; CCM HUWA HAWAIBI KURA, BALI WANAIBA MATOKEO. Mfano jimbo la Newala mkoani Mtwara, matokeo ya kura zote zilizohesabiwa zinaonyesha Ndugu Manguya wa CHADEMA alishinda Kwa zaidi ya kura elfu 36 dhidi ya Mkuchika wa CCM. Alichokifanya Mkurugenzi ni kuhamisha matokeo ya Manguya na kumpa Mkuchika na kisha kumtangaza mshindi.
wewe unaijua CHADEMA, siyo CCM. CCM unaipiga majungu tu. kama CCM inaiba matokeo basi ningewashangaa kama hawaibi majimbo ya Ubungo, ARUSHA, Iringa Mjini n.k. Acha kuiga kupiga propaganda humu, ww bado mchanga kwa propaganda.
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Kwanza naomba mniwie radhi kwa kuchelewa kuwasilisha taarifa hii kwani imepita takriban masaa 15 tangu nilipoona taarifa hii kwenye ITV Habari saa mbili usiku.Kwa hakika sikuamini kabisa nilipoona taarifa hii na nilijitahidi sana kusafisha mboni za macho yangu ili nione vizuri na kila nikiangalia hakika macho yalipatwa na ganzi.

Mbunge wa Bukoba Mjini, Wilfred LWAKATARE akiongea mbele ya Makamanda wa CHADEMA kwenye Mji wa Kahama jana alisema kuwa anawashangaa baadhi ya viongozi wanaolalamika kuwa wanaibiwa kura wakati ukweli ni kwamba hakuna kitu kama hicho. Anasema kuwa yeye anaongea kama Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA na amebaini kuwa Chama chake kimekuwa kikipoteza majimbo mengi kutokana na kukosa maandalizi ya kina. Alisema kuwa aliingia kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi wa ubunge jimbo la Bukoba Mjini baada ya maandalizi makubwa aliyofanya ya kuwaandaa vijana ambao watasaidia kumpa kura za kutosha. Ni kutokana na maandalizi hayo ndipo alipoibuka mshindi huku akimgaragaza mbunge mkongwe wa CCM, Dr HAMISI KAGASHEKI.

Kwa hali hiyo, aliwaasa CHADEMA na hasa kamanda LEMBELI kuanza maandalizi sasa kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa 2020 badala ya kuhangaika Mahakamani ambako ni kupoteza muda na fedha. Naye Kamanda LEMBELI alisema kuwa, jimbo la Kahama lina Majipu mengi ambayo yanatakiwa kutumbuliwa. Alimuomba Rais Magufuli kufanya ziara ya kushtukiza jimboni humo na yeye atahudhuria mkutano ambapo atakuwa na lengo moja tu la kumuonesha Rais Magufuli majipu yaliyojaa Kahama ambayo yanahitaji kutumbuliwa. Alisema kuwa Rais Magufuli ameanza vizuri na anaunga mkono utumbuaji majipu na kila mmoja anapaswa kumpa ushirikiano kwa vile ameonesha mwanzo mzuri.

MTAZAMO WANGU:
Ukitafakari kwa kina juu ya hoja za Lwakatare na Lembeli, utabaini mambo yafuatayo;
  1. Kwa vile Lwakatare ni Mkurugenzi wa Ulinzi na usalama wa CHADEMA, ni dhahiri kuwa chama hicho kinajua kuwa majimbo waliyoshinda, wameshinda kihalali na waliyopoteza ikiwa ni pamoja na Uchaguzi wa Rais wamepoteza kihalali.
  2. Hoja za Lowasa kuwa aliibiwa kura hazina baraka ya chama hicho isipokuwa ni hoja zake binafsi
  3. Makamanda wengi wanamkubali Rais Magufuli na wanaunga mkono jitihada anazochukua. Ila wale Makamanda Maslahi ndio wanaoendelea kulalama wakiongozwa na Lowasa na Mbowe

Hivi hujisikiaa aibu kuwa mbweha namna hii? "LOWASA ALIGOMBEA JIMBO GANI?". Unathibitisha kwamba ukiwa ccm lazima uwe pompompo!
 
Unafikiri bila kukomaa maeneo tajwa ushindi kwa wapinzani ungepatikana? Jiongeze mkuu, usitake kuleta ubishani usio kuwa na tija. Unakumbuka wakati wa uchaguzi JF ilikuwa hacked? Unajua ni nani walifanya huo mchezo mchafu na ni kwanini?
Huko kwingine walishindwa nini kukomaa? Basi hawako wamoja CHAGGADEMA.
 
wewe unaijua CHADEMA, siyo CCM. CCM unaipiga majungu tu. kama CCM inaiba matokeo basi ningewashangaa kama hawaibi majimbo ya Ubungo, ARUSHA, Iringa Mjini n.k. Acha kuiga kupiga propaganda humu, ww bado mchanga kwa
propaganda.
Naijua Ccm hata kabla haujaletwa duniani dogo,
Kwasasa endelea kuuza mashati na kofia za chama hapo Lumumba.
 
wewe unaijua CHADEMA, siyo CCM. CCM unaipiga majungu tu. kama CCM inaiba matokeo basi ningewashangaa kama hawaibi majimbo ya Ubungo, ARUSHA, Iringa Mjini n.k. Acha kuiga kupiga propaganda humu, ww bado mchanga kwa propaganda.

Unajua fika mwizi haibi kila sehemu. Huangalia sehemu zinazoweza kuingilika na akazimudu. Kushindwa kwa wezi kwenda kuvunja Benki kuu na kuishia kukwapua benki zingine, hakuwezi kumfanya mtu mwenye akili aseme siyo wezi.

Kushindwa kwa ccm kuiba kura sehemu zingine hakuwaondolei sifa ya wizi wa kura!.

Naomba ujifahamu kama hujui nyamza utafute ukweli badala ya kuongea kama uko kwenye saluni ya kusuka nywele.
 
Back
Top Bottom