Bome-e
JF-Expert Member
- Jan 3, 2014
- 17,153
- 26,152
Wewe ni nani mpaka umuone?Kwahiyo usipomuona wewe basi kila kitu kimeisha!Haya,mimi sikumuona Kinana,nianzishe uzi kwasababu sikumuona hospitali???Nimeshangazwa na kitendo cha Lema kutoonekana kokote pale ambapo utaratibu na maandalizi ya kuwaaga watoto wapendwa yalifanyika.
Sijamuona lema karatu au Mt meru akishirikiana na timu ya mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya katika kufanikisha zoezi la leo.wazazi na ndugu wa marehemu watakuwa ni mashahidi juu ya nani haswa walishirikiana nao toka mwanzo hadi leo hii katika hatua iliyofikiwa.
Pia sijamuona lema akienda kuwasabahi majeruhi watatu wanaoendelea na matibabu.
Badala yake nimemuona lema akiwa na gwanda zake za khaki huku muda mwingi akiongea au kutumia simu yake ya kiganjani na akitamani au kusubiria kushika kipaza ili aingize siasa.
Misiba ya watoto waliopigwa bomu katika uzinduzi wa kanisa olasiti uliendeshwa kihunihuni na kisiasa mno;lakini leo tumeshuhudia maandalizi na mpangilio mzuri ...
Ni wajibu wa kila kiongozi kuheshimu utu wa watoto hawa...tuko kwenye majonzi na sio kwenye kujitambulisha sisi ni kina nani kwenye msiba.
List ya watu walioshiriki kwa kiwango kikubwa katika uokozi,ubebaji wa miili nk ni kubwa lakini hao wote hawajataka kushika kipaza sauti pale stadium na sio kwamba wamebaguliwa.
POLE KWA WAFIWA..MUNGU AWAPE NGUVU.
KWA HISANI YA WATU WA ARUSHA.