Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,662
- 8,787
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetoa hukumu ya kesi ya madai ya mwanamuziki Lameck Ditto dhidi ya Kampuni ya Multchoice Tanzania Limited maarufu DStv, uamuzi ambao haujaacha kicheko kwa mlalamikaji.
Ditto ambaye jina lake halisi ni Dotto Bwakeya alifungua kesi ya madai mahakamani hapo mwaka 2020 akiiomba iamuru DStv imlipe fidia ya Sh6 bilioni kwa kutumia wimbo wa Nchi Yangu aliodai ni wake kwenye matangazo yao ya biashara bila ridhaa yake wakati wa kampeni za Fainali ya Mataifa ya Afrika (Afcon) mwaka 2019.
Baada ya hukumu iliyoipa nafuu DSTV, msanii Lameck Ditto amefunguka
Pia, aliiomba Mahakama iamuru alipwe Sh200 milioni kutokana na madhara ya jumla sanjari na malipo ya riba ya asilimia 25 tangu siku alipofungua shauri hilo akidai kampuni hiyo imemnyima fursa ya kunufaika na kazi yake.
Hukumu hiyo iliyosainiwa na jaji mfawidhi wa Mahakama hiyo, Salma Maghimbi ambaye hakuwepo mahakamani ilisomwa na naibu msajili wa Mahakama hiyo, Mery Moyo leo Julai 23, 2024, akisema wimbo uliotumiwa na DStv sio halisi ambao Ditto ndiye mmiliki.
Kabla ya kusoma hukumu hiyo, iliyokuwa na kurasa kumi, Moyo amesema imetolewa na Jaji Maghimbi na yeye amepewa kuisoma huku akianza kwa kueleza katika uumbaji, Mungu ametoa karama mbalimbali ambazo ndiyo chanzo cha kipato na mali.
Moyo amefafanua maana ya haki miliki akisema ni neno la kisheria linalotumika kutafsiri haki ya anayetengeneza kazi fulani akizichanganua kazi hizo ikiwamo ya muziki.
Amesema hakimiliki inatunza kazi ya asili ambayo imetengenezwa.
Katika hukumu hiyo alizitaja nafuu ambazo Ditto aliziomba katika shauri hilo na kubainisha kwamba, jitihada za kuwasuluhisha kwa sheria ya mwenendo wa madai hazikuweza kufanikiwa.
Mwananchi
Pia, soma=> Msanii Ditto afungua kesi ya Madai ya Tsh. Bilioni 6 dhidi ya Multi Choice (DSTV)