Kwanini uwanja wa Benjamin Mkapa unatumika kwa matumizi yasio ya Mpira?

Kwa sababu Mtanzania amepewa akili lakini anazitumia kwenye mambo mengine baadala ya kuzitumia kufikiri
 
Mtu yeyote anaweza kupeleka tamasha lake lamsingi alipie.
Matokeo yake ndo hayo uwanja unafungiwa kwa pitch kukosa ubora.

Hizo pesa wanazolipia zinaenda wap
 
Ni kawaida viwanja kutumika kwa functions zingine tatizo ni kutofanya ukarabati na kupiga hela.

Taylor Swift alifanya show yake Bernabeu uwanja wa Madrid. Allianz Arena uwanja wa Bayern Munich kuna functions nyingi tu zinafanyika pale mbali tofauti na match za mpira. Crypto arena zamani staples center uwanja wa kikapu wa Lakers una host shows zingine kibao including Grammy's, musical concerts etc.

Mkapa ulitengewa 30 Bil ila hadi leo hamna kitu kimefanyika na hela zimepigwa.
 
Uko sahihi sana mkuu
Wanaotumia uwanja wanalipia ila hawafanyi matunzo.
Tunarudi pale pale kwamba kama hawawez kuifanyia pitch matunzo baada ya hayo matukio, bora yasifanyike hapo
 
Ukiwa na jicho la tatu na ukisikiliza vizuri maelezo ya huyo jamaa utagundua shida haikuwa kwamba eti uwanja ulitumika mara kwa mara.

Uwanja umetumika mara kwa mara kivipi wakati kabla ya mechi ya Azam, uwanja haujatumika toka mechi za Yanga/MCA na Simba/Costantine?

Inaonyesha CAF walitaka mashine maalumu za kukata nyasi na mamlaka zikashindwa kuzileta kwa wakati, na walipokuja kukagua wakakuta hazijaletwa ndiyo wakatulima ban. Ndiyo maana anasema mashine zimefika waje wakague tena!

Ukitaka kujua hilo ninalosema ni kweli, waambie watoe hadharani barua ya CAF. Ndiyo maana anasema anataka siku nyingine wakitulima ban wapewe taarifa kwanza kabla haijatolewa kwa umma ili watupumbaze.
 
Uko sahihi sana mkuu
Wanaotumia uwanja wanalipia ila hawafanyi matunzo.
Tunarudi pale pale kwamba kama hawawez kuifanyia pitch matunzo baada ya hayo matukio, bora yasifanyike hapo

Ule sio uwanja wa mpira tu kwahiyo ni sahihi events zingine kufanyika pale as well changamoto bado ni ile ile wabongo ni waharibifu na serikali inapiga hela.

Wananchi wanavunja viti kila siku, wanang'oa mabomba ya maji wanafanya kila aina ya uharibifu na serikali ikitenga bajeti ya ukarabati inaishia mifukoni mwao tu. Nchi ya hovyo hii.
 
Ni umasikini tu.Viatu pair moja hivyohivyo kanisani au msikitini,kwenye harusi,kwenye mkutano,Bar,Kariakoo,Hospitali kumuona Mgonjwa....
 
Back
Top Bottom