Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Ndugu zanguni! Wakati watu wanatoa shuhuda humu nilikua nahisi haiwezekani, safari ilikua ndefu sana written za kutosha na oral mbili plus kukosa oral! Hatimaye wakati wa Mungu wakati sahihi umenifikia! Database imeniona nilifanya oral ya mwsho february! Na post ilihitaji watu wawili tu tukaitwa 15! Naomba msiache kujaribu na msikate tamaa wapambanaji! Ikawe heri kwenu pia siku moja ndugu zangu!
Halafu mnawasumbua UTUMISHI, wanawafanyisha usaili, mkipangiwa vituo vya kazi, hamtaki kwenda, wote mnataka mbaki DSM, acheni hizo aiseeh
 
Hata mimi huyu kanoshangaza kila siku tunaimba na watu hapa kuwa hata nafasi ikiwa moja hakikisha unaenda usikose interview….cha msingi ni kuingia oral…aende akalale hata stand ….aache kulialia dunia sio ya watu wanaotafuta visingizio…yani nafasi 28 mtu akache aiseee nitasikitika sana
Naenda mkuu, siwez kuacha.
 
Day 1 Dar na Moro
Day 2 Dodoma na Tanga
Day 3 Pwani na Arusha
Day 4 Kigoma,Iringa na Mbeya
Day 5 (kesho) ?

Wazee wanaosubiria asali ya Tamisemi tucheze na mikeka kidogo
 
Day 1 Dar na Moro
Day 2 Dodoma na Tanga
Day 3 Pwani na Arusha
Day 4 Kigoma,Iringa na Mbeya
Day 5 (kesho) ?

Wazee wanaosubiria asali ya Tamisemi tucheze na mikeka kidogo
Hivi mishahara ya tamisemi ni sawa na wizara au kunakuzidiana? Nimeona MD mmoja uko insta. Anadai hawezi kwenda kuripoti kazini kwasababu mishahara wizara kamzidi tamisemi parefu. Na kazi tamisemi wanapiga sana vile vile malupulupu kama extra duty tamisemi hayapo, je ni kweli??
 
Kwa uhakika zaidi wacha tusubiri wajuzi waje watoe ufafanuzi, ila niliwahi kuona mahala wanasema ngazi za mishahara ni zilezile ila tofauti inakuja kuwa kwenye mazagazaga ya nje na mshahara kama hizo extraduty kote nafikiri zipo ila sasa utofauti mkubwa ni kulipwa kwa wakati, fursa za hapa na pale kama kusimamia mitihani ya vyuo vya afya, na vitu kama hivyo
 
Hivi mishahara ya tamisemi ni sawa na wizara au kunakuzidiana? Nimeona MD mmoja uko insta. Anadai hawezi kwenda kuripoti kazini kwasababu mishahara wizara kamzidi tamisemi parefu. Na kazi tamisemi wanapiga sana vile vile malupulupu kama extra duty tamisemi hayapo, je ni kweli??

Mishahara ya watumishi wa afya walioko serikali kuu (wizara ya afya) na serikali za mitaa (TAMISEMI) zinalingana.
 
Back
Top Bottom