Mwifwa
JF-Expert Member
- Apr 3, 2017
- 48,234
- 125,341
Haya mambo ya kujiona special yalikuwepo sana enzi za shule/sekondari hasa Advance ambapo kama mtu alikuja na Div I kali anaanza kuhisi wengine sio type yake ila kadri muda unavyozidi kwenda anajua kuwa alikuwa hajui uhalisia wa mambo.Hapana mzee inawezekana Kuna Pepa moja mwaka juzi nadhani tulienda udom pale sasa tulikuwa na jamaa zangu mmoja hivi alikuwa anapenda kujitenga sana as unajua wale watu wanaokuwaga na gpa kubwa sana wanaonaga hata hawatakiwi kudiscuss na wengine sasa akawatenga washikaji wakaja maeneo niliyokuwa wanalalamika nikawambia tulie tupitie hizi notes tukapiga msuli fresh Pepa ikaja tukapiga ,ile tumetoka jamaa anakwambia aah Pepa imetoka mule mule na Hawa jamaa wengine wanasema hawaelewi walichojibu ,majibu kuja kutoka yule jamaa alipata 23 mzee na wengine wote wale walienda oral ,kwahiyo hizi mambo usikate tamaa pia usijiamini sana na kuwatenga wengine hata kama umewazidi uwezo
Mimi ikifikaga ishu hizi huwa najishusha hata kwa yule ambae najua nimemzidi uwezo lakini najua lazima kuna kitu lazima atakuwa nacho tu.
Na pia destiny ya mtu haipo kwenye maamuzi yetu ni nature ndio inakuchagulia pakwenda