Kwanini nyumba ikifika hapa inakuwaga ngumu kumalizia?

Kwa sababu tunafosi kujenga.

Mimi nikishakuwa na bajeti ya gharama ya nyumba mpaka inaisha nikahakikisha kwamba kiasi hicho ninacho kwa muda huo ndio nitaanza kujenga.

Kujenga tuna ku overrate sana wakati ni process za maisha kama process zingine.

Kwa maisha yangu mimi pakukaa sio tatizo,tatizo vyanzo vys mapato ndio shida,ninachofanya ni kupambana nipate biashara safi nitoboe na hapo nitajenga within a few weeks mjengo unasimama.
Kwa hz akilo we suala LA kujenga achama nalo.Nami nilikuwa nasema sitajenga yapo chumba na secure Ila nitanunua nyumba ya angalau 20M Ila nikaja kushtuka Nina 37yrs na watoto ndio Hao na wanakua Ikabidi nianze mdogo mdogo
 
Tajirii
 
Yeah. Hiyo nayo ni mbinu mojawapo. Baadaye ukimaliza chumba kimoja unahamia halafu unaendelea kujenga vyumba vingine lakini wakati huo wewe utakuwa 100% uko kwenye nyumba yako. Halafu sasa inakuwa kupeana shifti na fundi - akijenga huku akimaliza unahamia na mchezo unaendelea hadi nyumba inaisha ww ukiwa mumo humo.:D
 
Kwa hz akilo we suala LA kujenga achama nalo.Nami nilikuwa nasema sitajenga yapo chumba na secure Ila nitanunua nyumba ya angalau 20M Ila nikaja kushtuka Nina 37yrs na watoto ndio Hao na wanakua Ikabidi nianze mdogo mdogo
Mkuu wewe sio reference yetu katika haya maisha.

Ukishindwa wewe haina maana na sisi wengine tutashindwa hapana.
 
Mawazo kama hayo yalifanya wengi wakafa na nyumba zao kichwani bila ya utekelezaji wowote kufanya.

Na binadamu mwingine kukubadili msimamo wako huo hasi ni vigumu sana, sawa na ngamia kupenya kwenye tundu la sindano.
Mkuu mtu akifa hana nyumba lakini alikuwa anapambana kupata michongo endelevu sio shida.

Wagapi wamekufa hawana chochote na maisha yakaendelea,hakuna cha kupoteza tunapoamua kujitoa katika dunia.
 
Ndiyo ni kweli kabisa hususan pale inapotokea badiliko kwenye bei za vifaa, gharama ya usafirishaji, uaminifu na umakini wa mafundi.
Haiwezekani ukawepo site muda wote kama nyapara/msimamizi saa zote kwani wewe binafsi pia unayo majukumu mengine muhimu.
Halafu usisahau pia kwamba, kwa bahati mbaya baadhi ya vifaa vinaweza kuharibika e.g. kuvunjika kwa ceiling boards(Gypsum boards), sink za vyooni, Vioo au kitasa kuwa ni kibovu n.k. Tena inawezekana ukalazimika kubomoa sehemu fulani ambayo imejengwa vibaya au unataka kufanya maboresho katika ramani yako. Mambo ni mengi yanayoweza kuyumbisha bajeti ya awali kiasi kwamba ile 25% uliyoweka kama tahadhari ikaisha na bado isitosheleze.
Ndivyo ilivyo, gharama za ujenzi zinabadilika kulingana na location kilipo kiwanja, muinuko/msawazo wa kiwanja, sehemu unayojenga either mjini au kijijini, accessibility ya eneo lako kwa ajili ya kupitisha materials, nature ya wakazi wa eneo hilo/majirani(wengine ni wachawi wa maendeleo), upatikanaji wa usafiri k.v boda, toroli, kenta n.k

Hivyo vitu hapo juu vinaweza kuku-suplize na mfumuko wa gharama za ujenzi hadi uje ushangae labda waliokupigia tathimini walikuwa mazwazwa au ukawashutumu mafundi kuwa wamekuibia

Kuna location moja nilianza msingi aisee ziliingia tofali za kutosha na kokoto pamoja na cement hadi niliishiwa pumzi. Wakati huo ulikuwa kiangazi mvua zilivoanza na kulikuwa ni bondeni kidogo kumbe ule udongo wa pale unatitia ukuta wa nyuma wa msingi ukatengeneza nyufa na kuachana na kingo za mbele yaani ikabidi nianze upyaa
 
Kudundulizia mfukoni ni ngumu, inatakiwa kudundulizia hardware.....

Ukipata kiasi unapeleka hardware kama wana lipa namba ndo kabisa haupati uvivu, ukipata tu unatuma, ukipata kiasi unatuma unashangaa mara ya kupaua imetimia.
Ni risky sana utaratibu huo (na nimeshuhudia)kwani ikitokea kwamba mmiliki wa hardware ulikolimbikiza fedha zako akifariki au hardware ikapata ajali e.g. kuungua moto, utapata wakati mgumu sana ku-claim fedha zako ulizowekeza kwake. Lakini pia na wewe unaweza kupata changamoto ya kimaisha. Ni bora ukawekeza benki ambako utapata na kafaida fulani kuliko kwa mtu baki i.e. hardware.
 
Back
Top Bottom