Kwanini nafurahishwa sana na nazikubali mno Nyodo na Dharau za Dotto Magari ambazo ni Chungu Kwetu Wasomi, Wabaguzi na wenye Dharau kwa Masikini?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,948
119,228
1. Wasomi wengi tuna Dharau kwa wale Wasiosoma

2. Wasomi wengi ni Wabaguzi hasa kwa wale Wasiosoma

3. Wasomi wengi tunadhani Kusoma sana ndiyo kuyapatia Maisha

4. Wasomi wengi tunaishi Maisha ya Kuigiza wakati kiuhalisia tuna Shida Milioni kidogo

5. Wasomi wengi tuna Roho Mbaya iwe Makazini au Majumbani na hatutaki Kusaiia wasiosoma

6. Wasomi wengi nje ya kupata Vidigrii, Vimasta na Vipihechidii vyetu tunajiona tumeshayapatia Maisha

7. Wasomi wengi licha ya Kusoma Kwetu ila bado tu Ushamba na Ulimbukeni kuliko hata wale Wasiosoma

Kama kuna Mtu ( mwana JamiiForums ) ambaye anavutiwa na Nyodo na Dharau zote azifanyazo Dotto Magari nadhani GENTAMYCINE ni namba moja. Kudadadeki acheni tu Jamaa atunyooshe Wasomi kwani ALIDHARAULIKA, ALITENGWA, ALITUKANWA, ALIFITINIWA, ALISINGIZIWA UWONGO ALICHUKIWA na hadi kuambiwa ATAKUFA MASIKINI ila leo kawazidi mbali mno Wote waliokuwa wakimfanyia haya Mambo.

Namalizia kwa kusema BINADAMU TUTAPANGIANA MAISHA ILA MWENYEZI MUNGU HAPANGIWI NA ANAMBARIKI YULE AMTAKAE MUDA NA WAKATI WOWOTE PASIPO KUANGALIA MADHAIFU YAKE AMBAYO WANADAMU WANAMUHUKUMU NAYO. Na sijui kwanini Mwenyezi Mungu HUWABARIKI PAKUBWA WALE AMBAO WANAONEKANA ni reject katika Society na Family.

Safi sana Dotto Magari endelea tu KUTUNYOOSHA Baba kwa NYODO zako Sisi Wasomi hadi Akili zetu zikae sawa sawa.
 
Mtani kusoma na kufanikiwa kimaisha ni mambo mawili tofauti na mtazamo huo utaupata Kwa wasomi wa nigeria, kenya, uganda na Rwanda huko walishaacha kuona vyeti kama dhamana ya maisha, na ukimsikiliza hata kishimba utajua bado wasomi wanamiliki vyeti na sio akili ya maisha
 
Acha ATUNYOOSHE Kudadadeki. Kama unatamba umesoma halafu Dotto Magari ambaye hana Elimu na Exposure kama uliyonayo Msomi Wewe / Mimi kwanini tu asitudharau na kutufanyia hizi Nyodo na Dharau zake? Umesoma halafu Gari ulilonalo na unalotamba nalo ni la Mkopo, Nyumba Umepanga na kila Siku tu unagombana na Baba mwenye Nyumba wako au hata Kumkwepa wakati Yeye Dotto Magari ana Magari ya Kutosha na ana pa Kuishi vile vie huku bado akiwa anaingiza tu Hela kwa Mdomo wake kuliko Wewe na Elimu yako ya Kukariri ili upate Degree, Masters na PhD ambayo haijakusaidia na inaendelea tu Kukutesa kwa Maisha yako magumu na ya Dhiki japo ukiwa humu Mitandaoni unajifanya umeshayapatia Maisha.

Safi sana Dotto Magari Mimi ni Fun wako mkubwa sana endelea hivyo Kutupandisha Hasira kwa hayo Mafanikio yako.
 
Huyo dotto mqgari ana nyumba wapi hapo dar sie tunamjua bado kapanga tu usimpe vitu ambavyo hana kuwa na nyumbq dar unadhan mchezo
 
Namkubali kinomanoma huyu Jamaa na namwomba Mwenyezi Mungu azidi Kumbariki na Kumuinua ili wenye Chuki na Wivu nae tuumie zaidi.

Kudadadeki mkiambiwa Mwenyezi Mungu huwa HAPANGIWI WA KUMBARIKI KWA MUDA AUTAKAO TUWE TUNAAMINI jamani.
Niliskia kuna sehemu alituskilizisha wimbo anataka kuutoa unaitwa NA HAPA IPO.

Nausubiri kwa hamu sana.
 
Usomi upi unasemea ?..maana mtu ana Masters ya Surgery hana kazi ...kazi zake part time za kuunga unga ila dharau mpaka kwenye ukucha..... ninachojua Kumuheshimu mtu haina haja ya kwenda darasani ili mtu akuheshimu/umuheshimu that's all
Pole Sana kama umekutana na hiyo hali
 
Ulisoma ili kupata hela au kutoa ujinga? Pese ipo kwenye biashara, ufisadi na ujambazi. Na kwa sasa zimeongezeka sekta mbili ambazo ni ushoga na uchawa. Sasa kama hufanyi kimojawapo kati ya hivyo huo usomi wako utakuleteaje pesa?
Haya Msomi wa Pili mwenye Hasira na Mafaniko ya Dotto Magari ambayo Yeye hana ameshakuja. Pole sana Mkuu.
 
Back
Top Bottom