Kwanini mfumo wa ukataji tiketi za SGR unasumbua mara kwa mara, who is behind this?

Good Father

JF-Expert Member
Feb 28, 2014
10,319
18,547
Moja kwa moja kwenye mada,

Tangu tuanze kusafiri kwa treni za SGR kumekuwepo na changamoto za hapa na pale. Changamoto huwa zipo lakini tunatarajia kuwe na ufumbuzi na kutokujirudia rudia kwa changamoto ya namna ile ile.

Kwenye mfumo wa ukataji tiketi kumekuwa na changamoto ya kudumu, mfumo sio reliable kabisa. Leo unaweza kukata tiketi lakini kesho huwezi kukata tiketi unaweza kuhangaika hata siku mbili bila mafanikio.

Hii ni bahati mbaya au kuna biashara za watu humo?

Siku moja nimehaingaika sana mpaka nikawapigi wenyewe ndo wakanikatia tiketi wakatuma control number, sasa ikiwa wao wanaweza ku-access mfumo kwanini sisi watumiaji tunashindwa? je ni mapato kiasi gani yanaweza kuwa yanapotea? ni watu wangapi watafanikiwa kukata tiketi kwa kupiga simu?

Vyombo vyetu si vipo kwanini visisaidie mambo ya muhimu kama haya?
Siku moja niliona Kadogosa analalamika SGR inahujumiwa na wanaohujumu wanawafahamu mbona hatuoni hatua zikichukuliwa au ni mabwana wakubwa wenye fedha?

Kama tutaendelea hivi nina hakika baada ya uchaguzi wa 2025 kupita SGR itakufa kama yalivyokufa mabasi ya mwendo kasi.
 
Nje ya mada mkuu.

Hivi nauli ya kutoka hapa dar mpaka moro sh ngapi?

Je, umri wa mtoto kuanza kulipa nauli ni miaka mingapi?

Sitaki kufuatilia mambo hayo kwenye mtandao, naogopa hujuma.
 
Nje ya mada mkuu.

Hivi nauli ya kutoka hapa dar mpaka moro sh ngapi?

Je, umri wa mtoto kuanza kulipa nauli ni miaka mingapi?

Sitaki kufuatilia mambo hayo kwenye mtandao, naogopa hujuma.
Royal Tsh 35,000/-
 
Back
Top Bottom