Kwanini makampuni makubwa ya mafuta SHELL na BP yalijiondoa kufanya biashara Tanzania?

BP (Tanzania) Ltd ilimilikiwa kwa asilimia 50 na serikali ya Tanzania na kampuni ya BP (British Petroleum) ilimilikiwa asilimia 50.
BP(British Petroleum) waliamua kuuza shares zao na kujiondoa kwenye baadhi ya nchi za Africa kama vile Tanzania, Malawi, Zambia, Botswana ... Na kujikita zaidi Angola, Mozambique na South Africa.
Puma Energy, kampuni ya Uswisi ilinunua hisa za BP Tanzania.
Pamoja na Mafuta ya magari pia ilibidi ikubali kusambaza Castrol oil vituoni.
BP ilikuwa na 70% kwenye mafuta ya ndege huku bara na 100% Zanzibar, zote pia ziliuzwa.
Hapa mbona mnakinzana na huyu, sijaona mahali serikali ya tanzania ikitajwa kama imenunua asilimia 50

9:25AM GMT 15 Nov 2010
BP has agreed the £296m sale of stakes in its refining and marketing operations in southern Africa to Switzerland-based Puma Energy.BP said in a statement on Monday that it is selling its wholly-owned marketing businesses in Namibia and Botswana, as well as its 75pc stake in BP Zambia and 50pc stakes in BP Malawi and BP Tanzania."The decision to divest these businesses, which was first announced by BP in March 2010, followed a strategic review of BP's southern African refining and marketing businesses," the statement said."The sales do not include BP's refining and marketing businesses in Mozambique or South Africa."BP, Europe's second-largest oil company by market value, is in the process of raising $25bn to $30bn by the end of 2011 to help pay for its Gulf of Mexico oil spill.The sale is expected to be completed next year and subject to regulatory approval in the affected countries.Puma Energy is a subsidiary of Dutch-based oil group Trafigura.BP sells African assets to Puma Energy for £296m
 
BP ndio wamiliki wa Puma energy, hawajakimbia Bali jina tu limebadilishwa!! kokote unapoiona Pima energy jua kuwa umeiona BP(British Petroleum),

Nafikiri huna uhakika na unachokisema. Kama una uhakika, thibitisha kuwa mmiliki wa Puma Energy ni BP.
 
Kampuni ya SHELL japo ilikuwa ama bado mpaka sasa iko kama NEMBO HALISI ya biashara ya mafuta nchini , lakini miaka mingi iliyopita ilijiondoa kufanya biashara nchini mwetu .

Juzi juzi miaka michache iliyopita tumeshuhudia kampuni lingine kubwa la BP , kampuni pekee lililoaminika kutochakachua mafuta nalo likifunga virago vyake.

Nilikuwa nawaomba wadau waliozifahamu sababu za makampuni haya kutukimbia watuwekee hapa tuzijadili na kujifunza , na ikibidi tujirekebishe ili tusije kukimbiwa na makampuni mengine .
Naona unataka kutueleza kitu amabacho hakipo...kabla ya kuurusha huu uzi unge google kwa nini BP ilijiondoa Tanzania na nchi nyengine za kusini... Soma hapa
Major oil companies withdrawing from Southern Africa
 
Undikaji wa Shell ulifanyika miaka ya Eighties kwani kabla ya hapo kampuni ilitwa Shell and BP Tanzania serikali ikiwa na 50%, Shell 25% and BP 25%. Hapo mwanzo Shell na BP ziliungana kufanya biashara kwa sababu ya kushindwa kushindana kwani BP walikuwa wanauwezo mkubwa kwenye Uchimbaji na Utafafiti wakati Shell alikuwa na uzoefu kwenye marketing akiwa hana uwezo kwenye Utafiti, Uchimbaji na Usafirishaji. Hivyo walukubaliana katika nchi za Africa watafanya pamoja. Ilipofika miaka ya 1981 Shell ilishajijenga kwenye utafiti na uchimbaji na BP pia ilijijengea uwezo kwenye marketing hivyo waliamua kutengana. Waligana Nchi za kufanya baishara na walikubaliana kwenye nchi ambayo Shell angelikuweko basi BP asifanye biashara ya kuuza mafuta kwa muda wa miaka kadhaa siwezi kumbuka. Ndio maana Tz ilibaki BP na Kenya kukawa na Shell. Shell ilirudi mwaka 1983 lakini kufanya utafiti sio kuuza mafuta.
 
Ndugu yangu una matatizo ya akili?Nimeandika BP wapi?
Hapo hujaandika Bp lakini umefanya rationalization, ukimaanisha kujiondoa kwa BP Tanzania kuna prove point yako ya kuwa Tanzania siyo sehemu muafaka kwa kuekeza na ukatolea mfano kenya kama ni sehemu nzuri lakini hata huko BP imejiondoa...Hujaandika BP lakini nia yako ilikuwa kutuaminisha hivyo... sasa naona kama wewe ndiyo kichaa kwa kuandika kitu ambacho hukijui
 
BP iliuzwa kwa Puma baada yukuterereka kiuchumi, hii ni baada ya ajali waliyopata huko Gulf of Mexico kwa kisima chao kuvujisha mafuta mengi baharini na kupigwa faini kubwa.

Mipango ya BP kuondoka katika biashara ya uuzaji mafuta kwa rejareja barani Africa ilianza kabla ya tarehe 20 April 2010, siku ambayo ajali ya Deepwater Horizon Spill ilitokea (do some research). Kumbuka serikali yetu ilikuwa na hisa katika biashara za BP hapa nchini, hivyo majadiliano yalichukua muda mrefu. Ushauri wangu kwa watu wa aina yako ni huu, kama huna ufahamu wa kutosha kuhusu jambo flani si busara kuchangia kana kwamba una uhakika na unachokisema. Tafuta watu wanaofahamu kuhusu biashara ya mafuta hapa nchini and beyond ujifunze. It won't cost you much. Sanasana ni bia tu weekends kadhaa.
 
Kampuni ya SHELL japo ilikuwa ama bado mpaka sasa iko kama NEMBO HALISI ya biashara ya mafuta nchini , lakini miaka mingi iliyopita ilijiondoa kufanya biashara nchini mwetu .

Juzi juzi miaka michache iliyopita tumeshuhudia kampuni lingine kubwa la BP , kampuni pekee lililoaminika kutochakachua mafuta nalo likifunga virago vyake.

Nilikuwa nawaomba wadau waliozifahamu sababu za makampuni haya kutukimbia watuwekee hapa tuzijadili na kujifunza , na ikibidi tujirekebishe ili tusije kukimbiwa na makampuni mengine .

SHELL bado wanafanya business TZ, wapo kwenye GESI wamenunua hisa za BG
 
Hizi kampuni zina vitengo tofauti, kuna shell marketing ambayo inajihusisha na uuzaji wa mafuta yaliyo safishwa na kuna shell exploration inayojihusisha na kuchimba mafuta, ilio kuwa hapa nchini ni marketing. Inaweza kuwa hawakuona faida ya kuendelea na biashara au kuna ushindani mkali na ndio maana wakajitoa.
 
Wengi mnachangia kuhusu BP lakini mimi niliomba pia kuhusu SHELL .
Hebu chukuwa muda wako wa jioni hii ingia YouTube search documentary ya Al Jazeera inaitwa seven sisters nadhani utaanza kuijuwa dunia ilivyo, upo kwenye giza nene sana hata nikikupa maelezo hutaelewa, ningekuwa kwenye pc ningekuwekea hapa hiyo documentary ukiangalia na kuielewa basi majibu yako yote yapo humo, cha msingi dunia ya leo ukitaka kuelimika usiwe mvivu wa kutafuta habari na usiwe bahiri wa bundle lako tu.
 
Erythrocyte, sababu kubwa ya kujiondoa kwa makampuni haya kwenye nchi zetu hizi ni ubabaishaji uliopelekea washindwe kushindana na hivyo kupata hasara. Ili ufanye biashara ya mafuta hapa nchi, lazima uwe mbabaishaji na mkwepa kodi. Ukizingatia standards na ukashindwa kukwepa kodi utafeli kwa kuwa washindani wako wanafanya hawazingatii viwango na hukwepa. Kwa mfano, lori likiwa na tairi zimeisha halikuruhusiwa kujaza mafuta pale BP. Tank likibeba mafuta ya taa, BP hawakubali kuweka petrol kwenye tenki hilohilo. Walizingatia viwango vya juu mno, matokeo yake wakashindwa kushindana. Wakati wa tatizo la kuchakachua mafuta liliposhamiri, BP ni miongoni mwa waliolalamika sana.

Shell wamefanya kazi ya kutafuta mafuta nchi hii tangu miaka ya 1950. BP na Shell wana historia ndefu ya mashirikiano, especially in marketing. Sina uhakika, but my suscipicion is that Shell waliondoka hapa nchini pengine na nchi nyingine za ukanda huu kwa makubaliano ya kibiashara na BP.
 
na ikibidi tujirekebishe ili tusije kukimbiwa na makampuni mengine
Makampuni ya Kibeberu hayaji hapa kuekeza Kwa kuwa yanaipenda au wanapenda Tanzania au Watanzania. Yanawekeza kutafuta faida, tena faida nono (super profit). Huna sababu ya kuwa mnyonge makampuni husika yakiondoka. Waliondoka kwa sababu mipango yao ya kupata faida nono haikuendana na mipango yetu ya kisea na kisheria. Their departure shouldn't have bothered you because you will always see them coming in or and going back.
 
Back
Top Bottom