Kwanini makampuni makubwa ya mafuta SHELL na BP yalijiondoa kufanya biashara Tanzania?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
127,924
244,493
Kampuni ya SHELL japo ilikuwa ama bado mpaka sasa iko kama NEMBO HALISI ya biashara ya mafuta nchini, lakini miaka mingi iliyopita ilijiondoa kufanya biashara nchini mwetu.

Juzi juzi miaka michache iliyopita tumeshuhudia kampuni lingine kubwa la BP, kampuni pekee lililoaminika kutochakachua mafuta nalo likifunga virago vyake.

Nilikuwa nawaomba wadau waliozifahamu sababu za makampuni haya kutukimbia watuwekee hapa tuzijadili na kujifunza, na ikibidi tujirekebishe ili tusije kukimbiwa na makampuni mengine.
 
kumbu kumbu zangu , nakumbuka mwaka 2013 kukikuwa na uhaba wa mafuta hapa nchini, ikaonekana baadhi ya makampuni kama BP walikuwa hawuzi mafuta,wakati walikuwa wanayo kwa wakati huo, ndiyo serikali wakaifungia hiyo kampuni kwa muda usiyojulikana lakini baada ya mwezi, tukasikia kampuni imerusiwa kuendelea na biashara, lakini kwa masharti ya kushirikiana na Kampuni ya PUMA. mara baada ya muda nikayoona petrol satations zote za BP zimebadirishwa jina na nembo na kuwa PUMA-Energy. Swali langu nani mmiliki wa PUMA Energy? Tusaidiane hapo , kuhusu SHELL, sina data zake.
 
Bila shaka wadau watazidi kutiririka .
 
BP ndio wamiliki wa Puma energy, hawajakimbia Bali jina tu limebadilishwa!! kokote unapoiona Pima energy jua kuwa umeiona BP(British Petroleum),
 
Unadhani kwanini walibadili jina ?
hlo swali kuna mamlaka zina jibu! lakin wenyewe wanaamini hawajabadili jina Bali wameinunua Puma energy. makao makuu ya Bp yalikuwa pale kurasini - njia ya kwenda kariakoo, baada tu ya kuinunua puma energy, ofisi zao na kila kitu kikabadilika na kuwa puma, yaan jina Bp likafutika fasta.
 
Sawa kama ni hivyo je ni dunia nzima wamebadilisha jina au ni tanzania tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…