Kwanini Lowassa haongelei General Tyre?

Mada nyepesi sana. Nimefurahi sasa hata watoto wa primary nao tunao humu jamvini. Hongera teknolojia ya mawasiliano.
 
kweli kabisa.

nilishawahi kuweka uzi humu niaahidi zawadi ya lakin 1 kwa atakaye nipa crip ya LOWASA akikemea ufisadi na wizi wa mali ya UMMA lakini hamna aliyejitokeza hata vile vibaraka wake wenye njaa na pesa zako wote walikunja mikia yao nyuma. na ule uziulifutwa

Njaa zako za lakini moja kale na ahawara yako. Wewe mleta Uzi haufai hata kidogo kwani unahamasisha rushwa. Kawasaidi ndugu zako na hiyo lakini moja kule ......... L.....do.
 
Lowasa hawez ongelea rushwa hata siku1 hawez kukemea tumbili akijikata mkia ndio mwisho wa maisha
 
Lowasa anatokea mkoa wa Arusha wilaya ya Monduli. General tire ni kampuni la tairi ambalo lilikuwa mti wa mgongo katika uchumi wa Arusha, hata nchi kwa Ujumla. Pamoja kwamba kiwanda hiki Muhimu cha Tairi kimekufa katika hali ya sintofahamu, sijawahi kumsikia Lowasa akilalamika, au kuhudhunishwa na ufilisikaji wa kiwanda hiki. Nimewahi kumsikia Lema akilalamika na kutaka kiwanda hiki kifufuliwe, lakini jambo la ajabu Lowasa hakuwahi kusikika akiongelea kuhusu kiwanda hiki, pamoja kwamba kiwanda hiki kilikuwa muhimu sana kwa uchumi wa Arusha na Tanzania kwa ujumla.

Hawezi kuzungumzia General Tyre kwa kuwa wafadhili wake ni mawakala wa tairi zinazotoka nje ya nchi. Yeye anaona ajira kwa vijana ni kuwapa Toyo.
 
Huyu alishawah kuwa wazirbmkuu...angetakiwa ajue nan kaua general tyre.
 
Huyu alishawah kuwa wazirbmkuu...angetakiwa ajue nan kaua general tyre.



Umesahau kuwa Sumaye naye wakati anapewa uwaziri mkuu alikua mwenyeji wa Mkoa wa Arusha ?
Amekaa madarakani miaka 10 na kiwanda kimeuzwa kipindi chake,wewe unataka kumuuliza mbunge.
 
Umesahau kuwa Sumaye naye wakati anapewa uwaziri mkuu alikua mwenyeji wa Mkoa wa Arusha ?
Amekaa madarakani miaka 10 na kiwanda kimeuzwa kipindi chake,wewe unataka kumuuliza mbunge.

Wote waulizwe Sumaye na Lowasa kiwanda chetu kiko wap ??Ila lowasa anatamba alifanya makubwa ndo maana tunamhoji zaid ...kiwanda alikula nan?na yeye alikuwa wap ?
 
Sasa hivi aongee kama nani!?? Subiri aingie ikulu aongee
kwa kuwa bado hajatangaza nia rasmi ,tunategemea atakapotamka rasmi atuambie mipango yake ataifanyia nini tanzania ,sisi yeye tu wote wenye kuwatoka udenda kwenda magogoni.si busara kwa watanzania kumchagua mtu ambaye mpaka aipate ikulu ndio atuambie anatufanyia nini au alifanya nini hapo awali.ataishi kujifanyia yeye na awapendao.
 
Njaa zako za lakini moja kale na ahawara yako. Wewe mleta Uzi haufai hata kidogo kwani unahamasisha rushwa. Kawasaidi ndugu zako na hiyo lakini moja kule ......... L.....do.

kama ulienda shule basi ulitoka mtupu. unajua nini maana ya rushwa? hata wewe kama ni mtiifu kwa mamvi weka hapa jamvini crip yoyote anayokemea rushwa na ufisadi. kama huwezi basi na wewe unzinyemelea za richmond
 
Sijaelewa sababu ya Lowassa kuhojiwa kwa maswali yanayotakiwa kujibiwa na viongozi walioko madarakana. Maana yeye aliachia madaraka Serikalini tangu mwaka 2008. Akianza kushughulikia maswala ya jimbo la uchaguzi lisilo lake si itakuwa balaa. Nakumbuka mvutano uliotokea mkoa wa Kilimanjaro hivi karibuni baada ya Mkuu wa Wilaya kuonekana kwenye jimbo alikozaliwa lakini Mbunge wa jimbo husika alilalamika kweli. Kwa mazingira kama haya inakuwa vigumu mtu kushughulikia eneo lisilokuwa sehemu yake, lengo ni kuepusha mivutano isoyo ya lazima.
 
Back
Top Bottom