Kwanini CCM imejimilikisha viwanja ambavyo vilijengwa na wananchi wakati wa mfumo wa chama kimoja?

Yaani ili viwanja vyetu virudi kwa wananchi yaani Halmashauri zao ni kuitoa CCM Madarakani watake wasitake this 2024 serikali za mitaa kisha 2025 kwa uchaguzi mkuu.
Nguvu ya umma ikisimama kwa dhati ni nguvu isiyozuilika na lolote hata wakatae katiba mpya na Tume huru.
Sudan waliondoka, Misri, Burkina Faso nk na hakukuwa na cha tume wala nini bali dhamira ya wananchi tuu.
 
Waliwapora Waliovijenga ambao ni Wananchi Hebu tuambie lini ULIONA BANGO la ujenzi wa Hivyo viwanja na MKANDARASI ALIYEPEWA TENDA ya kuvijenga?
Kama ni wananchi jua pia walikuwepo wanaccm ambao ni wananchi pia! Usifikir chadema pekee ndo wananchi
 
CCM wamehodhi nchi na huwezi kuwafanya lolote, wewe unazungumzia viwanja vya mpira? Wewe mwenyewe hapo ni mali ya CCM, au unabisha mkuu?
 
Hadi maeneo ya wazi huku mtaani wanayapora,wanafanya
Mpaka watoto,vijana wanakosa pakucheza na kupumzikia
Watu wa ajabu sana hawa

Ova
 
Ninataka kufungua kesi kwa ajili ya kudai viwanja hivo, ninaombeni muongozo
 
Ninyi humu mnazungumzia viwanja. Nenda vijiji vya nyanda za juu kusini. Kila ghala wamechora ni lao. Una jiuliza, hawa watu walikuwa wanatumia vigezo gani? Yaani hata kama hiyo CCM unaipenda kuliko mama yako, utajiuliza uhalali wa kumiliki maghala yaliyojengwa na wanavijiji na mengine kwa uhisani unatoka wapi.

Siku umma ukijitambua, msajili ataamrishwa kufuta hiki chama, ingawa jambo hilo siyo laana au tatizo lolote.
 
Wadau nimekuwa nazifuatia mali za CCM wakati wa mfumo wa chama kimoja cha siasa ilikuwa wananchi wote bila kujali ni mwanachama wa CCM au huna chama ni lazima uchangie Maendeleo.

Wakati wa ujenzi wa viwanja vya Sokoine Mbeya, Nelson Mandela Sumbawanga, Uwanja wa Kirumba Jijini Mwanza na sehemu nyingine wananchi walichangishwa fedha mazao, mifugo na nguvu zao ili kujenga viwanja hiyo na waliokaidi walichukuliwa hatua.

Baada ya Mfumo wa Vyama vingi kuingia CCM ilijimilikisha viwanja hivyo wakati hatukuwahi kusoma bango lolote la ujenzi wa viwanja hivyo na CCM haikuwahi kuvijenga Viwanja hivyo.

Swali kwa CCM, kwanini Uwanja wa Taifa wa Uhuru Dar haijajimilikisha wakati nao ulijengwa wakati wa Mfumo wa Chama Kimoja?

Ushauri kwa CCM
CCM ivirudishe viwanja ilivyojimilikisha serikalini kwani vilijengwa na wananchi sio Wana CCM na kama CCM inataka kumiliki viwanja ijitafutie maeneo, ipime kisha kwani kati ya Vyama vinavyopata ruzuku kubwa CCM inaongoza hivyo haiwezi kushindwa kujenga.

Endapo viwanja vilivyoporwa na CCM vikiwa vya Serikali vitatumiwa na wananchi wote tofauti na sasa kwani Mapato yake yatakuwa ya serikali badala yakuchukuliwa na CCM wakati haikuvijenga bali ilivipora.

CCM na vyama vingine vijenge viwanja vyao kwa kutumia Ruzuku zao.
kwani vilijengwa na chama gani? :BillyApprove:
 
Tulipoingia mfumo wa vyama vingi CCM ilikomba ndege ya rais na kuipa jina CCM ONE! Kilichoinusuru ndege siyo gari, walipoambiwa kila siku italipiwa maegesho kwenye uwanja wa ndege ikawashinda. Kutokana na mazoea ya uporaji imepora baadhi ya shule zilizokuwa za halmashauri za miji! Imepora viwanja alivyoviacha mkoloni kama Mkwakwani na vinginevyo.
 
Wakili Damas Mbogoro alishafungua kesi kuhusu uwanja wa majimaji Songea sikumbuki hukumu ilikuwa vipi
 
Back
Top Bottom