Mzee wa Twitter
JF-Expert Member
- Nov 5, 2023
- 1,392
- 2,170
Wadau nimekuwa nazifuatia mali za CCM wakati wa mfumo wa chama kimoja cha siasa ilikuwa wananchi wote bila kujali ni mwanachama wa CCM au huna chama ni lazima uchangie Maendeleo.
Wakati wa ujenzi wa viwanja vya Sokoine Mbeya, Nelson Mandela Sumbawanga, Uwanja wa Kirumba Jijini Mwanza na sehemu nyingine wananchi walichangishwa fedha mazao, mifugo na nguvu zao ili kujenga viwanja hiyo na waliokaidi walichukuliwa hatua.
Baada ya Mfumo wa Vyama vingi kuingia CCM ilijimilikisha viwanja hivyo wakati hatukuwahi kusoma bango lolote la ujenzi wa viwanja hivyo na CCM haikuwahi kuvijenga Viwanja hivyo.
Swali kwa CCM, kwanini Uwanja wa Taifa wa Uhuru Dar haijajimilikisha wakati nao ulijengwa wakati wa Mfumo wa Chama Kimoja?
Ushauri kwa CCM
CCM ivirudishe viwanja ilivyojimilikisha serikalini kwani vilijengwa na wananchi sio Wana CCM na kama CCM inataka kumiliki viwanja ijitafutie maeneo, ipime kisha kwani kati ya Vyama vinavyopata ruzuku kubwa CCM inaongoza hivyo haiwezi kushindwa kujenga.
Endapo viwanja vilivyoporwa na CCM vikiwa vya Serikali vitatumiwa na wananchi wote tofauti na sasa kwani Mapato yake yatakuwa ya serikali badala yakuchukuliwa na CCM wakati haikuvijenga bali ilivipora.
CCM na vyama vingine vijenge viwanja vyao kwa kutumia Ruzuku zao.