Makonyeza

Member
Feb 2, 2020
72
259
KWANI WANAWAKE MPO WAPI?

Na Moh'd Majaliwa, Adv.

Kiasi imenistaajabisha na kunistua, sikuitarajia hali hii.

Kwenye makutano na mikusanyiko mingi ya maana na ya kipuuzi, wanawake nyie huwa wengi zaidi ya wanaume, yaani mmekuwa wepesi kuhamasika na kwa ajili hiyo kipimo cha jambo lako la kijamiii kukubalika ukiweza kuwashawishi wanawake basi inatosha kutoa tathmini ya jambo lako.

Kwenye mkutano ya kisiasa zote za upinzani na hata za chama tawala, nyie ndo mmekuwa mkitumika sana tena inasemekana kwa gharama ndogo ya elfu kumi na khanga au t-shirt, japo si wote.

Kwenye mitandao ya kijamiii ndo mabingwa wa kushiriki vurugu za aina zote iwe michambo, umbea, kujipiga tu picha mkicheza na maumbile yenu.

Hivi Sasa wanawake mmekubali kutumia muda mwingi kujadili ugonvi wa Diamond na Harmonize mkigawana upande na mwisho wa siku mnawafaidisha Media tu.

Bado najiuliza halijawagusa au hamuoni umuhimu wake, au ndo ile sumu ya wanawake kutokupendana japo siamini katika hilo.
Hivi kitendo cha Rais Samia Suluhu kutangaza kuruhusu mtoto wa kike aliyepata ujauzito akajifungua aendelee na masomo, kwenu ni jambo Dogo sana?

Mbona binafsi naliona ni kubwa sana tena pengine kuliko yote aliyekwisha kuyafanya mheshimiwa Rais kwa ajili ya Mwanamke wa kitanzania.

Ameyafanya Mengi kumuhusu mwanamke, nakumbuka aliwakingia kifua wanamichezo wanawake na zawadi za viwanja akawapa, sijasikia vibe lolote kutoka kwa wanawake wa Tanzania.

Akafanya uteuzi mbali mbali akihakikisha nafasi za uongozi anazigawa sawa kwa sawa kuwalinda wanawake na kuwaongezea heshima kwamba mnaweza, lakini napo sijasikia Shangwe kutoka kwenu.

Leo kanyoosha mkono kumkomboa binti aliyetelekezwa na kupuuzwa kwa ajili ya ujauzito alioupata kwa bahati mbaya ya kubakwa akiwa shule na bado inaonekana ni jambo la kawaida tu.

Zile taasisi zilizosajiliwa kutetea mwanamke leo ziko wapi, hazioni hili, wale wanawake wanaojiita wana harakati kutetea haki za wanawake vipi nao hawajaisikia Rais ametangaza nn? Wanawake mna vyama vingi saaaana, kama elfu hivi!

Wanasiasa maarufu, wasanii, wana muziki na wana Habari wanawake mbona mpo kimya?
Nilitarajia Sasa nishuhudie makongamano ya kumshukuru, kumpongeza na kumpa moyo Rais mwanamke mwenzetu kwa kuwa pigania kiasi hiki.

Nilitarajia Mijadala kwenye mitandao ya kijamiii kushukuru kwa hili hata maandamano ya Amani, matamasha maalumu ya michezo, kwani dhambi kumshukuru Rais kwa jambo jema alilofanya hususan kwa kundi muhimu la wanawake?

Dunia ilitushangaa wakati ikihangaika kumkomboa mtoto wa kike sisi ghafla tukapiga hatua elfu kurudi nyuma kwa kumnyima elimu mtoto wa kike kwa kisingizio cha ujauzito,leo Mama ametunusuru na aibu ya dunia eti mwanamke wewe unaona ni kawaida tu, c'mon!

Kesho wewe mwanamke upo tayari kuja kukaa juani masaa kumi na mawili kusubiri ngonjera za uongo na ukweli wakati wa uchaguzi utakapokuwa ukiahidiwa shida ya umeme na maji kuwa historia mkimchagua fulani na Sauti mtapaaza hewani kushangilia!

Hivi hii nafasi ya mwanamke kuongoza mnadhani itatokea lini tena baada ya huyu wa Sasa? Binafsi naliona pengine haitotokea tena labda miaka hamsini mingine ijayo, huyu wa Sasa mpeni moyo basi, muungeni mkono, mumsaidie, Mjivunie naye.

Hili la kumrudisha mtoto wa kike darasani ni kubwa kuliko yote yaliyofanywa tangu awamu ya tano mpaka hii ya Sita, kwa wenzetu wazungu hii ingetosha kumpa Tuzo maalumu.

Mko wapi nyie, ebu amkeni bhana, pigeni shangwe kumsapoti Mama aongeze bidii bado tuna safari ndefu sana kwa faida ya mtoto wa kike.

Sisi ni waume zenu tu, lakini mwanamke ndugu yake mwanamke bwana!

Screenshot_20211126-220123~2.jpg
 
Sasa kama hujui hawna hata habari. Kujua tu kama kuna jambo hilo wanajua wanawake wenye level ya Masters na Phd tu. The rest ni group moja na sifa zao ni zile zile hata thinking yao. Samahani kama ntawaudhi lakini huu ni ukweli.

Hapa Tz mwanamke mwenye darasa la saba, form four, form six, diploma.na degree hawana tofauti saana.
 
Maisha magumu.

Mtu hana uhakika wa kula akaangaike na siasa.

Hata hivyo, adui wa kwanza wa mwanamke ni mwanamke mwenzie.

Mama akiendelea kuwaamini kama anavyofanya atakuja kupigwa na kitu kizito kichwani.
 
Wanawake mda mwingine nao huwa wapo safi kichwani,wanaona hali za maisha ya wanaume wao zilivyo mbaya, kukaa kimya inaonyesha hilo siyo kipaumbele chao. Hali za maisha ya watanzania nimagumu sana sana.mie nichukue nafasi hii kuwapongeza wanawake kwa kukaa kimya.
 
Kitendo cha kumrudisha shule binti hakijawafurahisha wanawake, binti akipata ujauzito wao husherehekea na kuona ni neema kwao, badala ya kusikitika wao huandaa sherehe ya ngoma ya kumtoa mtoto na kumtafutia mchumba binti! Sasa unapomrudisha shule insmaana umeharibu sherehe zao na sare zao za madera, nani atafurahia hilo?
 
Hakuna mzazi atakayeshangiliaaa mtoto wake wa kike apigwe mimba arudi nyumbani azae kisha amrudishe darasa la tatu B' aendelee na masomo.
Hiyo ni sababu tosha ya kutolishangilia jambo hilo chanyaa kwa kulipigia mbiu.


Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 
Tupo, na tunampongeza Mheshimiwa Rais, ingawa mioyoni tuna hofu na wasiwasi juu ya malezi ya binti zetu ukizingatia ndio wameruhusiwa kurudi shule hata wakipata ujauzito....tabu iko pale pale, Kwa tamaduni zetu fedheha ni ya mama pia.
Tupo tunatapa tapa na nafsi tu....Ila ni Jambo zuri Kwa future ya mabinti zetu.
 
Wanawake wameenda kutafuta maji toka saa tisa usiku mpaka sasa saa mbili asbh hawajarudi, umeme hakuna, huo muda wa kongamano wananuka jasho makwapani na sehem zingine wanautoa wapi!!!?
 
Sijui kama unajua maana ya kiongozi mwenye NYOTA YA MAVIII? Huyo ni nyota ya mavi tutegemee ukame, njaa, chuki, visasi ,na kyporomoka kwa uchumi ,kwa kasi kubwa hayo ndiyo matokeo ya kiongozi mwenye nyota hiyo
Rudi Kwa mola wako,naona umegubikwa na wimbi la jazba.
 
Kuruhusiwa msichana aliyepata ujauzito kuendelea na masomo,ni janga la taifa,kuanzia sasa mimba mashuleni zitaongezeka mara tatu zaidi,sijapost hivi ilitubishane,tusubiri miezi 18 ijayo asilimia 50 ya wanaokwenda leba kujifungua itakua ni ya wanafunzi waliopata ujauzito ambayo eti wasomi wa Tanzania mnauita wa bahari mbaya.

Kauli ya kiongozi wa nchi huwa inaumba mambo makubwa sana,nakumbuka kiongozi aliyepita,aliwahi kusimama hadharani na kuliambia taifa eti ukimpa askari wa barabarani sh 5000 eti siyo rushwa hiyo ni hela ya kubrashi viatu,matokeo yake mmeisha yaona jinsi trafiki wanavyojipanga barabarani kudai rushwa ,ni aibu sana.
 
Tuko busy na mambo ya msingi.

Kuwalea watoto wetu katika misingi, kuwapa elimu ya afya ya uzazi ili wasipate hizo mimba wakati wa masomo yao na wafikie malengo yao kwa wakati.
 
Back
Top Bottom