Kwa sasa jukumu la kusomesha watoto apewe mwanamke pekee, wanaume tunadharaulika sana watoto wakifikia kilele cha mafanikio

Mganguzi

JF-Expert Member
Aug 3, 2022
1,432
3,498
Nimeona tabia hii imeshika Kasi sana ,akina mama au wazazi wenzetu wanatutambua kama wazazi pindi watoto wanapohitaji karo za shule na mahitaji yote! Wake zetu huwaambia watoto kupeleka mahitaji yao kwa baba ' iwe karo, mavazi, chakula, matibabu na kila kitu mhusika mkuu ni baba!! Lakini baadae watoto hubadilika na kumtelekeza baba Kisha kuambatana na mama!

Watoto wakishafanikiwa baba anageuka adui! Kila kitu ni mama, mama atajengewa nyumba, mama atapandishwa ndege, mama atafanyiwa shopping na wakati mwingine kumhamisha mama kabisa na kumuondoa mikononi mwa baba!

Akina baba huko vijijini wana hali mbaya sana! Watoto hawapokei hata simu za akina baba Kuna haja gani akina baba kuendelea kuwaghalamikia watoto wa kizazi hiki wasio na akili?
 
Kila mtu anavuna alichopanda. Kwa watoto wenye upendo wa kweli hawawezi jenga matabaka kwa wazazi.

Kuna sababu zinazofanya watoto wamjali mama zaidi. Kwa mifano hai niliyoishuhudia na ninayoendelea kuishuhudia ndio chanzo. Uwezi kumzalisha mwanamke umuache apo anapambana na watoto enzi za ujana wako alafu umezeeka ndio unataka ukaribu na watoto.

Ukali nao ni sababu nyingine, kuwa mkali inapotakiwa lakini sio kila mda ni kufoka foka mpaka watoto wakisika baba anakuja wanakimbia vyumbani. Tengeneza urafiki na wanao.
 
Sure hapa chini ndiyo point muhimu sana kwa kizazi hiki, sababu maisha yanabadirika sana.

Iwe ukali, ukata, upendo au vyovyote bado hayo hayawezi kuwa sababu usimpende babako, babako ni babako tu awe vyovyote vile bado ana nafasi kwako.

Tutunze mapato yetu wenyewe pasipo kushirikisha yeyote labda bank tu, endapo litatokea lolote.

Pambana tu uweka amana zako za uzeeni vizur watoto sio kuwategemea kabisa utakuja kufa na kisukari...........
 
Kila mtu anavuna alichopanda. Kwa watoto wenye upendo wa kweli hawawezi jenga matabaka kwa wazazi.

Kuna sababu zinazofanya watoto wamjali mama zaidi. Kwa mifano hai niliyoishuhudia na ninayoendelea kuishuhudia ndio chanzo. Uwezi kumzalisha mwanamke umuache apo anapambana na watoto enzi za ujana wako alafu umezeeka ndio unataka ukaribu na watoto.

Ukali nao ni sababu nyingine, kuwa mkali inapotakiwa lakini sio kila mda ni kufoka foka mpaka watoto wakisika baba anakuja wanakimbia vyumbani. Tengeneza urafiki na wanao.
 
Mwanaume, kama wakati wa ujana wako hukuwa na time na familia yako basi usitarajie wao kuwa na time na wewe pindi umejizeekea ukute na pesa huna ndio unarudi kujitilisha huruma jua tu utavuna ulichopanda.

Hizo familia si rahisi kuwa hivyo bila sababu lazima kuna aina ya maisha waliishi hao wazee ndio yamepelekea leo hii watoto wamejikausha kimya na mama zao, fuatilia utagundua kitu.
 
Kila kitu kina sababu mtoto awezi kufanya hivyo kama amna kisababishi,kuna mzee mmoja alikuwa analalamika kama wewe.yy watoto wake kama watatu wanaishi marekani ila majimbo tofauti basi mama yao ilikuwa anatoka Jimbo hili kwenda lingine mama akirudi Tanzania mzee analetewa zawadi tu .mzee ajawai kanyaga USA,mzee yalimshinda ikabidi aende kwa mchungaji kulalamika,mzee kuulizwa uliishi vipi na watoto wako akajibu nilikuwa ni simba pia alikuwa na upendeleo wa wazi kwa wanae.sawa na matendo yako utavuna ulichopanda
 
Kila mtu anavuna alichopanda. Kwa watoto wenye upendo wa kweli hawawezi jenga matabaka kwa wazazi.

Kuna sababu zinazofanya watoto wamjali mama zaidi. Kwa mifano hai niliyoishuhudia na ninayoendelea kuishuhudia ndio chanzo. Uwezi kumzalisha mwanamke umuache apo anapambana na watoto enzi za ujana wako alafu umezeeka ndio unataka ukaribu na watoto.

Ukali nao ni sababu nyingine, kuwa mkali inapotakiwa lakini sio kila mda ni kufoka foka mpaka watoto wakisika baba anakuja wanakimbia vyumbani. Tengeneza urafiki na wanao.
Hakuna namna utafanya kuwahamisha watoto wakupende kama wanavyompenda mama yao.
Chakufanya mwanaume timiza wajibu wako kama baba wa familia, halafu punguza matarajio ya kwamba ni lazima waje wakusaidie, ili wasipokusaidia usife kwa pressure! Kama ni msaada wakupe kwa kupenda wao hasa watoto wako wa kiume maana nao inawezekana watakuwa na majukumu ya kulisha familia zao.
 
Back
Top Bottom