OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 51,621
- 113,092
Mwanzoni mwa 2019 niliuguliwa sana mdogo wangu. Nililazimika kufa naye kwa sababu nilianza kuishi naye akiwa form 1 wakati mimi nimeanza maisha. Aliumwa takribani mwaka mzima,gharama za matibabu zilikuwa kubwa sana lakini nikakomaa mpaka akapata afadhali kubwa.
Kabla ya hapo nilikuwa mstari wa mbele sana kusaidia ndugu wa ukoo kwenye misiba na ugonjwa. Lakini siku yaliponikuta sikuona hata mia ya ndugu. Kilichonikatisha tamaa zaidi kuna binti alikuwa anaolewa. Ndugu wakanitumia meseji ya mchango. Maana yake kwa hali yao ya kawaida waliweza kukaa vikao vya harusi kujichanga, lakini kwa huyu dogo mgonjwa sana hawakuwa kukaa kikao kumsaidia.
Ile sms ya mchango sikuwahi kuijibu ilinitia hasira. Baada ya siku mbili wakanipigia simu sikuiona ikafuata sms ya kukumbusha mchango. Nikawapuuza sana. Nikabaki na dukuduku moyoni.
Habari za kuumwa zilienea sana lakini wachache sana waliowahi kuulizia maendeleo ya dogo. Hii haikunisumbua nilichagua tu komaa na madaktari zaidi.
Sasa bana mwaka juzi ukatokea msiba wa mjomba kule kijijini nikaenda kuzika. Kwa kule kijijini nachukuliwa kama mtu mwenye uwezo sana kwa hiyo ukiwa kule kila mtu atataka kuongea na wewe. Ikawa kila mtu anaulizia habari za dogo anaendeleaje na pole nyingi sana. Nikawaza hizi pole ni za kinaa hizi. Ujinga zaidi baadhi wanakupa pole kisha wanakupiga mzinga.
Baada ya msiba huwezi kuamini baadhi yao wakaanza kuniomba nauli ya kurudi makwao, hawa ndio wale waliokuwa wananipa pole nyingi. Hiii ndio ilikuwa fursa kwangu kutoa dukuduku langu.
Hoja yangu hapa ni kwamba angalia zaidi familia yako, achana na shida za ndugu. Ndugu wasifanye wanao wasile maisha na kusoma vizuri. Ndugu hawana shukrani, utawasaidia sana lakini siku yakikufika usidhani watakuonea huruma.