Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,855
- 121,992
Wanabodi,
Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huwaletea makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa" zenye maswali fikirishi
Swali la Leo ni Je wajua kutotambua matokeo ya uchaguzi wa rais, ni Kutomtambua rais, serikali na Bunge?. Rais akiisha apishwa ni rais!, umtambue, usimtambue, it doesn't change a thing, rais bado ni rais. Kitendo cha baadhi ya watu/taasisi kusema hawayatambui matokeo ya uchaguzi mkuu, hawamtambui Rais wa JMT, hawalitambui Bunge la JMT, je huu sio ujinga?, watu au taasisi wanaofanya hivi sio ni wajinga?. Jee tutaendelea kuruhusu ujinga kama huu, kuendelea nchini mwetu mpaka lini?!.
Moja ya maeneo ambayo yamekuwa neglected na serikali yetu, sekta binafsi na Civil Society ni eneo la utoaji elimu ya uraia Kwa umna. Hii ni kazi iliyopaswa kufanywa na mihimili yote na taasisi zote, mfano Mhimili wa Serikali ulipaswa kuwa na vipindi vya elimu kwa umma kuhusu serikali na utendaji wa serikali. Bunge nalo kuwa na vipindi vyake, mahakama nayo na vipindi vyake, na taasisi nyingine zote. Matokeo ya kukosekana vipindi vya elimu ya kwa umma kuhusu somo la uraia kunapelekea hata baadhi ya viongozi wetu wengine hadi wakuu, hawajui baadhi ya mambo kuhusu uendeshaji wa nchi, wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa ndio maana baadhi yao wanafanya maamuzi ya kiajabu ajabu mengine yakiwa ni maamuzi ya kijinga!.
Tangu Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995 chama kikuu cha upinzani huku Bara NCCR Mageuzi, kiligoma kuyatambua matokeo ya uchaguzi na kwa Zanzibar CUF walisusia. Hali hii iliendelea hivi kwa chaguzi zilizofuata.
Uchaguzi Mkuu wa 2010 Chadema walijidai kususa kwa kauli ila matendo yakawa ni tofauti na tuliwaeleza humu.
Matokeo ya uchaguzi wa 2020 kuna chama kilisusa kwa kauli, kuwa hakiyatambui matokeo ya uchaguzi mkuu uliopita na kuuita uchafuzi, hakimtambui mshindi na hakilitambui Bunge lilitokana na uchaguzi huo.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, ikatoa nafasi 19 za viti maalum kwa chama hicho, Chama hicho kikatoa kauli kuwa kwa vile hakiyatambui matokeo ya uchaguzi mkuu huo hivyo hakizihitaji hizo nafasi na hakikateua wanachama wake kuzijaza, hawana haja nazo.
Hili ni bandiko elimishi kuelimisha umma kuwa, kwa mujibu wa katiba ya JMT, baada ya uchaguzi Mkuu kwa upande wa matokeo ya urais, kama una malalamiko yoyote kuhusu uchaguzi wa rais, yawasilishe Tume ya Uchaguzi NEC kabla ya matokeo ya urais kutangazwa. Matokeo ya urais yakiishatangazwa na Tume ya Uchaguzi kuwa mshindi ni fulani, Tangazo hilo ndilo linahitimisha mchakato wa uchaguzi wa rais Tanzania, matokeo hayo ni final and conclusive, vyama hata havijaridhika na matokeo ya uchaguzi mkuu huo, wanaweza kuendelea kusema kulalamika, kususa na kusema hawayatambui matokeo, lakini baada ya Rais Mteule kuapishwa na kuwa rais rasmi wa JMT, huyu sasa ni Rais, hata kama hukubaliani na matokeo, ni lazima umtambue rais wa JMT, sio lazima umpende au umkubali, that is an option lakini issue ya kumtambua rais is not an option, it's a statutory issue. Swali kwa wanaojidai hawamtambui rais, Je wanajua kusema humtambui Rais, ni kusema huitambui serikali, huitambui mahakama na hailitambui Bunge?. Hivi vyombo vitatu ndivyo vinaunda dola, hivyo kutomtambua Rais ni kutoitambua dola, hakuwezi kufanywa na mtu yoyote aliyeko ndani ya JMT kwasababu, ule uwepo wako tuu, unawezeshwa na uwepo wa serikali. Lakini Kwa mtu aliyepo nje ya JMT anaweza asiitambue serikali na ikawezekana. Hivyo mtu yoyote au taasisi yoyote iliyomo ndani ya JMT, ikisema hailitambui Bunge la JMT, maana yake ni haitambui serikali, hamtambui Rais wa JMT, haiitambui mahakama ya JMT, ni haitambui JMT, mtu kama huyu au taasisi kama hii si ni anafanya ujinga tuu?,. Watu hawa ni ya kuhurumiwa tuu na kusaidiwa, kwenye eneo la kusaidiwa, ndilo bandiko hili linachofanya, hawa watu wanahitaji kusaidiwa, ujinga huu uwatoke.
Kukajitokeza wanachama majasiri na mashujaa ambao hawakukubalia na ujinga huo wa chama chao, kutotambua matokeo, wakafanya jitihada binafsi, nje ya utaratibu wa kawaida wa chama chao, wakapata barua za uteuzi, wakateuliwa na kuwa wabunge wa Bunge la JMT.
Wenye chama chao, wakaitisha vikao vya nidhamu kuwajadili, ambapo kwa mujibu wa katiba yao vikao vilivyo itishwa ni vikao batili, maamuzi yakafikiwa kwa mtindo wa a Kangaroo Court, ambayo nayo ni maamuzi batili, wakawatimua mashujaa hawa.
Baada ya kuwatimua, vile chama chao kiliisha jinasibu kuwa hakiyatambui matokeo ya uchaguzi, hailitambui Bunge na haitambui serikali, hamtambui Rais wa JMT, ikategemewa baada ya kuwatimua ndio wamemalizana nao!.
Kumbe wameandika barua Bungeni kutaka mashujaa hao wafutwe ubunge. Nafasi mlipewa, mkazikataa, wanaozitaka wakazichangamkia, sasa kwanini mnataka waondolewe huku hizo nafasi hamna haja nazo?!.
Bunge si hamlitambui, wanachama wenu waliojiunga na Bunge ambalo hamlitambui, sii mmeisha wafuta uanachama, kuna haja gani kuliarifu Bunge?. Si muachane nao tuu kwasababu sasa hamuwatambui na wako kwenye Bunge ambalo hamlitambui, hizo barua za nini?!.
Kwa vile uanachama wa chama cha siasa unatawaliwa na Katiba sheria taratibu na kanuni, wamefungua shauri mahakamani kupinga Ukangaroo wa vikao batili vya Kikangroo, jee mahakama mnaitambua?.
Chama kinatoa taarifa ya kutolitambua Bunge, kutomtambua Rais wa JMT, huku Mwenyekiti na M/Mwenyekiti are begging to meet Rais wa JMT, and they met, one of them, more than twice!, Leo ni mara ya 3!, huku kutomtambua Rais wa JMT ni kutomtambua gani?!.
Huku kutolitambua Bunge la JMT huku unaliandikia mabarua, kwa barua moja hiyo hiyo kupelekwa Bungeni siku hiyo hiyo na watu watatu tofauti!, huku ni kutotambua gani?!.
Kuna msemo wa kizungu usemao "Spare the rod and spoil the child", members wa Chadema wanakipenda sana chama chao, wanaogopa kukirudi kwa kukiambia ukweli kuhusu ujinga wake, wakichelelea kulia,"mchelea mwana kulia, hulia yeye", hivyo akina sisi, tunaokitandika bakora Chadema, bile kuchelea Chadema kulia, usikute ndio tunakisaidia Chadema kukaa kwenye mstari, kuliko hata wale wanaokidekeza na kukikimbia nyimbo za shangwe na mapambio.
Naomb kumalizia kwa hili swali, je huu sio ujinga?, na watu au taasisi wanaofanya hivi sio ni wajinga?. Jee tutaendelea kuruhusu ujinga kama huu, kuendelea nchini mwetu mpaka lini?!.
Wasalaam
Paskali