Kutoka Bahari Beach Hotel: Yaliyojiri katika Mapokezi ya Edward Lowassa kujiunga CHADEMA

Mara nyingi konda wa basi akikushusha njiani porini huwa mara nyingi utapata lifti gari kutoka kwa gari jingine na lile basi utalipita njiani. Lowasa kashuka kwenye Leyland Victor kaingia kwenye Scania 94H
 
Yaan hana kaz kabisaaa....

Mkuu pale huyu mzee kapotoka kidogo, huenda hakumanisha kijana kapigiwa chapuo ila kauli ile italeta tafsiri nyingi kidogo, nilifikir anataka kusema mh. aliifanyia makubwa sana wizara ya maji ktk kipind chake kumbe anamaanisha malezi ya kijana wetu mtiifu.
 
Kuna watu wanasema Lowassa anatafuta nini. Kama pesa anazo, huko Ikulu anakimbilia nini? Si angetulia tu ili ale taratibu.

My take;

Hayo ni mawazo ya wachumia tumbo.

Hapo ndio ujue Lowassa hana lengo la kuingia Ikulu kwa lengo tu la Ikulu. Kwa jinsi alivyohatarisha maisha yake kwa tukio lake la kuachana na magamba hii inaonyesha anatazama maslahi mapana zaidi ya Taifa kwa ujumla na sio kula.

Lowassa angekuwa mchumia tumbo angejipendekeza kwa Magufuli na kumsapoti, angesaliti dhamira yake ya kweli ya kuwakomboa watanzania na kutulia asigombane na System, ili system iendelee kumtunza.

Lowassa hajaingia CHADEMA kwa sababu ya uhakika wa kuingia Ikulu, hapana, he has taken a big risk, amejihatarisha ili kuleta mabadiliko. Ujio wake utadhoofisha sana CCM mbovu, na baada ya uchaguzi, baada ya CCM kulia kilio na kukosekana wa kuwapangusa machozi, ndipo CCM itaweza kujijenga sawa, lakini kwa hali ya sasa mbio za Kinana ni za sakafuni tu.

Na pia naomba kuwahakikishia kuwa Kinana, Filikunjombe, Ndugai, Jenista, Kingunge, Makamba, Mzee Bilali na wengine ambao sitawataja kwa sasa watahamia UKAWA siku moja kabla ya uchaguzi bila kujali hatma zao kisiasa. Lengo likiwa kuikomboa Tanzania. Watalipa gharama. Kina Mandela walilipa gharama na kukaa gerezani zaidi ya miaka 20, gharama hii watakayolipa ni kitu gani.

Nchi hii mwaka huu inaenda kukombolewa. Siyo kwa kupata Malaika hapana bali kwa kumwondoa shetani,.. CCM!

Kama huamini basi endelea kuishi, usitoroke dunia ndugu yangu, utayaona!
 
mbowe asema : Bwana asifiwe...
anamkaribisha Lowasa na familia yake yote CHADEMA.
 
Back
Top Bottom