Kusitishwa Msaada wa Marekani Uwe Mwanzo wa Kusitishwa Mingine

Mkuu kama si uelewa wangu mdogo suala ni kuwa mazingira gani yamepelekea kulazimishwa kwanza kujitegemea ghafla hivi.ubaguzi na uvunjaji wa utaratibu tulizojiwekea wenyewe ndio umetufikisha hapa
hapa ndio utaona upeo wa wanaojiita wasomi badala ya kuja na mkakati wa namna gani tunaweza kujitegemea bila kutegemea misaada inayotudhalilisha wamebaki wakilaumu kuwa bila misaada hatutaendelea wakati huo huo wanasahau hakuna kitu cha bure tena kwa mzungu.

Waache wakate misaada yao ili na sisi akili zetu zifanye kazi kwani watu walikuwa wanatengeneza bajeti kwa copy and paste, wanashindwa kufanya namna gani nchi ieendelee sisi tuna kila kitu lakini wajinga wachache ingawa wao wanajiona wajanja wametoa mwanya kwa makampuni ya nchi kufaidi rasilimali zetu wao si wana uchaguzi tuone kama watatekeleza hiyo demokrasia wanayohubiri.

Hiyo miradi inaweza kutekelezwa kwa pesa zetu wenyewe bila kuwapigia magoti na tukiitekeleza watatueshimu na kutammbua kumbe misaada yao haina ulazima kwetu
Nashauri serikali iwekeze kwenye rasilimali watu ili tupate watu wenye mawazo mbadala badala ya hawa wasomi feki waliojaa ofisini bila kutoa mchango wowote
 
Ningeyaelewa sana haya kama sisi ndo tungeikataa MCC.lakini kwa vile waziri amesema serikali imesikitika kwa uamuzi huo,na kwa vile waziri wa fedha amesema tutaongea nao tu hadi watazitoa tu hizo pesa basi naamini hizi zote ni drama na kutaka kuficha ushetani uliofanyika zanzibar.

Maiga ni wanadiplomaia aliyesema alichostahili kusema kulinda uhusiano mwingine. maneno yake hayaonyeshi kuiomba Marekani 'itusamehe'. Ukweli unahitaji hesabu na labda hitimisho ni ikisomwa budget. kama tutakuta mradi huo umesimamishwa kwa sababu MCC wametunyima hela basi Maiga alikuwa anawabembeleza. kinyume ni geresha ili wamarekani waedelee kujiona 'wakubwa' huku tukisonga mbele. Huwezi kuwa huru kwa kuwabembeleza watoa misaada ya masharti mengine yanakuzuia usikohoe kana kwamba kikohozi huja kwa hiyari.
 
Tungebadirisha katiba yetu ingakuwa jambo bora zaidi.hii inayotoa haki kwa kila mtanzania kuchagua na kuchaguliwa kuwa viongozi huku tukijua nchi haitolewi kwa makaratasi na kuwa kuna watanzania na machotara na watu wa kasikazini itaendelea kututia matatizoni
Maiga ni wanadiplomaia aliyesema alichostahili kusema kulinda uhusiano mwingine. maneno yake hayaonyeshi kuiomba Marekani 'itusamehe'. Ukweli unahitaji hesabu na labda hitimisho ni ikisomwa budget. kama tutakuta mradi huo umesimamishwa kwa sababu MCC wametunyima hela basi Maiga alikuwa anawabembeleza. kinyume ni geresha ili wamarekani waedelee kujiona 'wakubwa' huku tukisonga mbele. Huwezi kuwa huru kwa kuwabembeleza watoa misaada ya masharti mengine yanakuzuia usikohoe kana kwamba kikohozi huja kwa hiyari.
 
Wangeweza hata kuamua kusitisha misaada kwa kudai Lowassa ameibiwa na kuwa Magufuli hakuwa Rais halali na kuwa CCM wameiba uchaguzi. Hawakuamua kufanya hivyo kwa Bara wakati sababu zilizotolewa na CUF Zanzibar ndio zile zile zilizotolewa na CHADEMA Dar.

Na wapo watu wanaoamini kabisa kuwa Magufuli hakushinda uchaguzi lakini MCC wala nchi wahisani wengine hawakutishia kusitisha misaada kwa sababu hiyo! Kwanini waje kusitisha kuhusiana na Zanzibar?

Kwanini wanaamini CUF walionewa Zanzibar au uchaguzi uliharibiwa na demokrasia kuvurugwa Zanzibar lakini siyo Bara wakati wapo ambao wanaona kabisa kuwa hata Bara demokrasia ilivurugwa?
MM kwanza niwatake radhi wasomaji kwa neno 'kuchepuka' kabla hawajanining'iniza

Pili, nichupuke kidogo nje ya mjadala tukibaki katika kingo za MCC

MCC hawana double standard, sisi ndio wenye matatizo na undimila kuwili. Msimamo wa MCC upo wazi kupitia waangalizi kama ilivyo kwa EU,AU, EAC.Uchaguzi wa TANZANIA ulikuwa fair and free.

Kama tunakubaliana/hatukubaliani na hilo ni suala jingine, muhimu ni kauli za waangalizi wakiwemo MCC

Kutokana na system mbili za uchaguzi ambazo umezitetea mara nyingi kuwa ni Parallel yaani ule wa NEC na ZEC, waangalizi wakasema hawakuona tatizo uchaguzi unaoandaliwa na ZEC.

Kwa maana moja kwamba ule wa Tanzania (NEC),ZNZ inashiriki haukuwa na tatizo, na ule wa ZEC peke yake haukuwa na tatizo. Hivyo, sioni wapi wangetenga uchaguzi wa Bara na visiwani ikiwa kauli zao zimejieleza kama nilivyoanisha

Na kwa kutumia kigezo hicho, CCM/Magufuli wanasema 'waangalizi wa kimataifa' wakiwemo MCC wanakubali uchaguzi ulikuwa fair and free. Wasichokubali ni uchaguzi huo kuwa fair and free Zanzibar, si kwa mujibu wa MCC bali matakwa yao

MCC wana msimamo mmoja kuhusu Tanzania na Zanzibar. CCM na Magufuli wanakubali nusu glasi kwa bara, kwa visiwani una matatizo wakitumia MCC hiyo hiyo inayohalalisha bara na visiwani isipokuwa wao akina Magufuli hawataki

MCC wanapinga marudio ya uchaguzi kwa mtazamo ule ule kuwa uchaguzi chini ya NEC na ZEC ulikuwa free anf fair, hawaoni sababu za kurudia.

Hapa ndipo CCM/Magufuli wanapohamisha goli, kwamba kwa mujibu wa CCM/Magufuli kupitia Jecha uchaguzi wa ZNZ una matatizo( Huwa naambiwa 'uncle' usini pestie maneno'') wao wana paste kwa MCC. MCC ilishasema hakuna tatizo

MCC wana haki na wapo sahihi kusema demokrasia ilivurugwa na kuharibiwa ZNZ.

Haki yao si lazima iwe ukweli, bali ukweli wa msimamo wao kuhusu uchaguzi wa Tanzania ndio una wapa haki.

Na haki hiyo wanaipata zaidi pale, Jecha akiwa chini ya vyombo vya ulinzi na usalama alikwenda peke yake kufuta matokeo. Akiwa mwenyekiti wa tume huru hakupaswa kuchukua hatua chini ya shinikizo la CCM/

Tunarudi pale pale hata kwa vigezo vyetu, uchaguzi ulivuugwa kwasababu uliingiliwa.

Kwa mtazamo wa MCC walishasema CCM imeshinda kihalali, na ZNZ hakukuwa na tatizo.

Shida inaanza kwa hoja kuwa kama hakukuwa na tatizo ZNZ , tatizo lipo wapi?
Well tatizo ni kuwa uchaguzi uliokuwa fair and free kwa mujibu wa MCC haukutangazwa na hivyo ulivurugwa bila sababu za kutotangaza matokeo. MCC wapo consistent kuwa uchaguzi kote bara na visiwani ulikuwa huru.

CCM wanayumba kwamba MCC imesema uchaguzi ni halali lakini imekosea, kule ZNZ si halali!!!

Kwa kutumia vigezo hivyo na msimamo usiyoyumba kuhusu uchaguzi, MCC wapo sahihi kabisa, hawajatudhalilisha

Tulijidhalilisha wenyewe,Magufuli anabeba mzigo kwa hili.
Alikubali MCC ilipo 'favor' interest zake, akaikataa iliposimama na 'interest' zile zile lakini asizo zitaka.

MCC wanasema hawatoi pesa kwasababu hatukukidhi vigezo tulivyowahi kukidhi huko nyuma

Hatukukubaliana na mkataba wetu na wao chini ya MCC. Wanzuia mshiko wao ili nasi tuendelee na chaguzi za Machi 20 na zingine wa kadri tunavyotaka

Hamadi, hilo limewagusa CCM/Magufuli ndio maana kuanzia majuzi tunaambiwa tuwe wazalendo kwa kukana makosa yetu ituwabambikie MCC lawama. Tunajificha vichwa mchangani huku nyuma tume.. lile neno lako

CCM/Serikali hawana hoja, wanatumia uzalendo, kwasababu hawana hoja dhidi ya MCC

Ni jambo la hatari sana wote tukisimama katika uhuni kwa mwamvuli wa uzalendo

Lazima tuwe na wazalendo watakaotuonyesha wahuni wapo wapi Taifa liondokane na wingi wa wahuni na ombwe la wazalendo. Uzalendo si uongo/uzushi au uhuni. Ni tunu

MCC wapo sahihi, MCC hawajatudhalilisha hata kidogo.
 
Mzee mwanakijiji kama hujui kilichofanyika zanzibar ungekaa kimya kuliko kuuliza miswali yako ya ajabu eti ’we unajuaje aliyeshinda uchaguzi wa zanzibar na dunia inamjuaje' kilichofanyika zanzibar ni ushenzi katika demokrasia, wengine sisi tulikuwa waangalizi aliyofanya Jecha na serikali yake ni kuharibu uchaguzi aliyepata akose. Usitegemee kwa akili kama hizo itafika kipindi tutaweza kuendelea bila misaada, kujitegemea inatakiwa kuwa wamoja kama nchi na sio kundi moja kujiona wao ndio wanahaki ya kutawala milele.
 
Africa-outline-FINAL-website.jpg


Na. M. M. Mwanakijiji
Yapo matatizo mengi sana yanayotokana na nchi kupokea misaada ya kigeni bila kuwa na sera rasmi inayohusiana na sekta hiyo muhimu na yenye kugusa mweleko mzima wa maendeleo ya taifa. Baadhi ya matatizo hayo ni kuwa wenye kutoa misaada hiyo wana uwezo – wakijisikia –wa kuamua kukuambia uiname na kubong’oa bila wewe kuuliza kwanini wanataka uiname! Tena wanasubiri wakusikie unawauliza “hivi nilivyobong’oa inatosha au nibong’oe zaidi”!

Tatizo jingine la kuwa mpokeaji wa misaada hii ya kila namna ya kigeni hasa ile inayoingia kusaidia bajeti ya nchi (direct budgetary support) ni kuwa wewe katika kupanga kwako mipango yako yote ni lazima kwa uwasikilize wachangiaji hawa na uwe tayari kuwabembeleza wachangie kwenye kile kikapu cha fedha za misaada (donor basket) ili mipango yako ifanikiwe.

Wakichelewa kutoa au wakianza kusua sua inabidi wewe mwenyewe uanze kufikiria mara mbili utakamilisha vipi mipango yako bila wao. Unaweza kujikuta unawafuata na kuwauliza “mnataka nibong’oe jamani?” ili waanze kuchangia au kutimiza ahadi zao.

Lakini pia lipo tatizo kubwa la tatu; ukishawategemea na wakisha kukufanikisha kwenye mambo kadha wa kadha basi kifikra wewe mwenyewe unawafikiria hawa mara kwa mara katika mipango yako, n ahata kama huwahitaji kweli kweli unaanza kujisikia kama unawamiss hivi! Wasipokuja kuzungumza nawe unaanza kuwatafuta kwa simu na mawasiliano mengine.

Unaanza siyo tu kuwategemea kwa fedha zao wanazotoa (wakati mwingine wanatoa kwa mkono huu na kuchukua kwa mkono ule wakati umebong’oa) unaanza kuwategemea kifikra. Wakitishia kutokukupa fedha unajisikia kuumwa, unachanganyikiwa, na unaanza kuona au kuamini unaona kuwa watu wako wameanza kuwa maskini ghafla! Unaanza kuona miradi yote ambayo ilikuwa inategemea misaada yao inaelekea kufa.

Na cha kusikitisha ni kuwa wapo watu kati yako ambao wataanza kukufanya uamini kuwa bila ya hao watoa misaada kweli miradi itakufa kwani hakuna “namna nyingine” yoyote ya wewe kuitimiza. Watakuambia “unaona sasa hujabong’oa ndio maana!” na wengine kwa haraka watasema kwa ukali “si unajifanya mbishi wewe hubong’oi! Sasa watu wako watakufa ni bora ukabong’oe haraka na sisi tutakusaidia kukushika ukibong’oa!”

Ndugu zangu, uamuzi wa Wamarekani kusitisha misaada yao ya karibu dola milioni 470 ili kushinikiza Serikali ya Tanzania kufanya vitu visivyowezekana ni uamuzi ambao wenyewe unaweza kuhojika na kuhojiwa. Sababu zilizotolewa na Wamarekani za kwanini wameamua kusitisha fedha hizo kama ukizikubali unaweza kujikuta uko tayari kukubali jambo lolote bila kuhoji. Sababu ambayo taarifa ya Shirika la Changamoto ya Milenia (MCC) inazitaja zinapaswa kumuudhi Mtanzania yeyote mwenyewe kujifahamu na mwenye kuheshimu utu wake. Tamko lao linasema “Tanzania moved forward with a new election in Zanzibar that was neither inclusive nor representative” Yaani, Tanzania “iliendelea na uchaguzi mwingine huko Zanzibar ambao haukuwasisha wahusika wote wala haukuwa wa kiuawakilishi.”

Hivi ili uchaguzi uwe wenye kuhusisha na wenye uwakilishi ni lazima wahusika gani wawemo? Marekani leo hii inahangaika na Donald Trump na tunaona jitihada zinavyofanyika kuzuia mwendo wake kuingia Ikulu ya nchi hiyo. Na tena kuna hadi mipango ya njama ya kuvuruga taratibu ili asiwe mgombea. Hivi kweli ikitokea Donald Trump akatupwa nje kwa sababu baadhi ya watu hawamtaki na akaenda kushinda mtu mwingine kweli Watanzania tunaweza kusema uchaguzi wao ulikuwa wenye kuwakilisha wote na wenye sura ya uwakilishi kweli?

Hivi, kuna mtu alikatazwa kupiga kura siku ya Jumapili kwenye marudio? Hivi, ni kweli kabisa kwa vile wanatutakia mema Wamarekani na wengine wamechukua wakati gani kwenda kukaa chini na kuangalia ushahidi au madai ya serikali juu ya kuvurugwa kwa uchaguzi wa Oktoba 25? Au na wao walitaka tu uchaguzi ufanyike ili ufanyike? Hivi kweli kabisa tunataka tukubali kuwa kwa vile hawa watoa misaada wanasema ‘uchaguzi ulikuwa huru na wa haki’ ina maana ni lazima uwe hivyo?

Sijataka bado sana kuingia kuzungumzia hili la Zanzibar lakini itoshe tu kusema hapa kuwa kama tumeamua kukubali misaada ni lazima pia tuwe tayari kukubali kubong’oa. Lakini utakuwa tayari kubong’oa mpaka lini? Ni mpaka upigwe mateke mangapi wakati umebong’oa ndio utasema “huu mchezo mimi sitaki”?

Jibu lake linaanzia kwenye jibu la ‘je ni kweli bado unahitaji misaada”? Naomba kupendekeza kuwa wakati wa misaada umepita. Hata mtoto kuna wakati unamnyonyesha, unampa chupa, unamlisha, unamsaidia kula mwisho wa siku unampa kijiko ale mwenyewe! Mtoto mkubwa na asiye matatizo yoyote ya kiafya kuendelea kumlisha na kumpa chupa ya kunyonya inasema zaidi kuhusu wewe kama mzazi kuliko yeye mtoto!

Lakini pia ni lazima tuwe wa kweli; kama kweli misaada ingekuwa inainua taifa na kuleta maendeleo ya watu Tanzania ingekuwa mbali sana leo hii. Misaada ambayo Tanzania imepokea ukiangalia na ufisadi uliokuwepo unaweza kujiuliza hii misaada siyo hiyo hiyo inasishia tena kwenye ufisadi na hivyo kuhitaji misaada zaidi?

Hata wanyama wanapolea watoto wao unapofika wakati wa kuwaacha watoke nje na kujitegemea wanyama huwa wanakuwa wakali. Hadi mtoto anapata akili eh, inabidi nikatafute chakula mwenyewe sasa!

Watanzania na labda Waafrika wengine ni lazima tuanze kujiamini kuwa tunaweza bila misaada. Mahusiano yetu na wakubwa hawa hayawezi kuwa na heshima na usawa kwa kadiri ya kwamba bado tunakinga makapu yetu watusaidie. Binafsi ninaamini – katika mwanga wa yaliyotokea siku hizi mbili – kuwa Serikali ya Magufuli ni lazima ikae chini na kufanya maamuzi ya lazima, sahihi na ya makusudi. Maamuzi hayo kwa maoni yangu sehemu yake ni lazima yawe yanaamua mambo yafuatayo:

1. Serikali ikubali kwa moyo mkunjufu na kuheshimu uamuzi wa MCC kusitisha msaada wao huo. Hakuna sababu, ulazima wala haja ya kutoa kauli ya kusikitishwa na uamuzi huo. Wakati Ujerumani Magharibi ilipotishia kuondoa misaada yake ya kijeshi kufuatia uamuzi wa Serikali ya Muungano wa Tanzania kuendelea na ubalozi mdogo wa Ujerumani Mashariki kule Zanzibar baada ya Muungano Nyerere siyo tu alikasirishwa na hilo lakini alienda mbali zaidi. Aliwaambia Ujerumani wasitoe huo msaada wao na msaada mwingine ambao tayari ulikuwa imepokelewa - karibu dola milioni 1 wakati ule – akawarudishia! Na akasema neno zito sana. Alisema “Sisi si mbwa! Mbwa unaweza kumtishia na chakula, lakini sisi ni binadamu na tuna utu wetu. Ni masikini lakini tuna utu wetu” Kwa maneno mengine kuwa kwa vile tumekubali kusaidiwa haina mamana tuwe tayari kubong’oa!

2. Serikali chini ya Magufuli ifanye uamuzi wa haraka, wa lazima na wa kimkakati wa kutenga zaidi ya shilingi trilioni 1.07 ambazo Wamarekani walikuwa wazitoe kwenye kuchangia sekta ya nishati. Fedha hizi zitolewe (siyo ziahidiwe) na kutengwa kwa ajili ya kuzibba pengo hilo na zianze kwenye bajeti ya mwaka huu na kukamilika si zaidi ya mwakani. Na ni LAZIMA zitoke kwenye fedha za Watanzania wenyewe. Hili ni suala la kisaikolojia; kwamba katika umaskin wetu tunaweza kuficha aibu yetu! Ni kweli ni maskini lakini katika utupu wetu yule anayetaka kutupa hifadhi hatutaki atushikie nguo na kutuambia tuiname kwanza; hata kwenye majani tutajihifadhi kwanza. Kwani maskini hana utu?

3. Serikali ndani ya miezi hii miwili hivi au mitatu ije na sera ya kusimamia suala la misaada ya kigeni na sera hiyo iweke mkazo wa misaada nje ya bajeti. Bajeti ya Watanzania ni lazima itokane na jasho na kazi za Watanzania na si vinginevyo. Misaada yote inataka kutolewa iwe ni katika maeneo ambayo tunaamini yanahitajika – hasa kwenye suala maeneo matatu:
• Kuhamishia ujuzi na maarifa (transfer of knowledge)
• Uwekezaji na Biashara (investment and trade)
• Kurudisha uhamishaji wa wasomi wetu (reverse brain drain)
Misaada ya kigeni itapaswa kuwa kwenye maeneo hayo matatu tu; maeneo mengine yote ya kibajeti Watanzania watapanga na kuyasimamia yenyewe; kwa kupambana na ufisadi, kuleta nidhamu kazi, uwajibikaji, uwazi na usimamizi mzuri wa fedha na mali ya umma. Hatuwezi kuendelea kupokea misaada hata ya kuchimba vyoo ili tu tujisikie tumesaidiwa na kuwafanya watoa misaada huko waliko waseme “tumeisaidia Tanzania”

4. Serikali ya Marekani ikiamu kurudisha msaada wake basi tuingie tena makubaliano nao na iwe nje ya MCC. Na msaada huo uwe kwenye hayo maeneo matato hapo juu; hizo milioni 470 ziende kwenye vyuo vyetu kufundisha wasomi na wataalamu katika masuala ya nishati na wasomi hao wafundishwe ama hapa hapa nchini kwa kuanzisha mahusiano ya vyuo na taasisi za Marekani na taasisi zetu badala ya wanafunzi wetu kwenda kusomeshwa huko Marekani peke yake. Fedha hizo zinaweza kutumiwa vizuri kabis akutengeneza miundo mbinu ya kufundishia wanafunzi yenye kuunganisha vyuo vyetu na vile vya Kimarekani na hivyo kutoa nafasi kubwa ya wengi zaidi kupata mafunzo.

5. Serikali ikae chini na nchi rafiki na kuweka msingi wa mahusiano yetu nao na hili liwe wazi baada ya kuchukua uamuzi wa kutokuwa nchi ya kupokea misaada. Maana ukiwa unapokea misaada ni vigumu kuwaambia watu sikilizeni; wanaweza wakakuambia “tutakusikiliza ukibong’oa kwanza”.

Binafsi ninaamini mashinikizo yoyote ya kisiasa kwa serikali yetu yanapaswa kufanywa na Watanzania wenyewe. Sina tatizo kabisa na Watanzania wengine ambao wanailalamikia serikali ya Magufuli au wanapinga mambo mbalimbali yanayofanywa hii ni sehemu ya demokrasia na wana haki hiyo. Kama vile Watanzania wasivyo na sauti wala serikali yao isivyo na sauti mbele yay ale yanayofanywa huko Marekani au nchi nyingine basin a sisi tusitoe hiyo nafasi isipokuwa labda kwenye mazingira ambayo kweli yanapasa. Watanzania wenyewe wanajua vitu vya kushinikiza na vipi washinikize.

Ni wakati wa kusitisha misaada hii ya kigeni mara moja na daima ili kuanza kujenga uchumi kweli unaoendeshwa na shughuli za uzalishaji mali, bidhaa na huduma mbalimbali. Uchumi wetu uko katika hali ya kusahihishwa na tayari tumeanza kuona dalili za kusahihishwa uchumi huo; wakati umefika wa kusahihisha kwenye hili eneo la misaada ya kigeni kwani nalo – na wengine wameshalionesha hili – misaada hii imedumaza sana maendeleo yetu kama taifa na kama bara.
Ni wakati wa kuanza kutumia akili zetu kuendesha maisha yetu nay a watoto wetu. Hatuwezi kuendelea kunyonya na midevu yetu juu! Tunaweza vipi kujiheshimu kama tunafanya mambo ya kutokujiheshimu? Unaweza vipi kulilia kusaidia badala ya kuanza kujiuliza ni vipi nitaacha kusaidiwa ili nianze kujijengea heshima?

MMM
Yatupasa tuwe makini sana na utoaji wetu wa maoni khs hili suala la usitishwaji wa misaaada.
 
anayetaka misaada ya marekani sijui mcc ahamie hukohuko, sie bongo tumezoea mihogo na jua kali, ikibidi hata mkaa tutachoma tuendelee na maisha yetu. tukilegea zenji watakuja na issue za ushoga. uchaguzi zenji ushakwisha na maisha yanaendelea. wampe trump nchi yao sie hatuna shida nao
 
Nchi hii bana, watu wanafiki sana. Eti hatuhitaji huo msaada....wakati hata ARV tunapewa na huyo huyo mmarekani.

Kama mmarekani anatoa hela ya ndugu zako kutahiriwa huko usukumani, what makes you think 1tr sio chochete sio lolote?
 
Mzee Mwanakijiji,

Ujumbe mzito sana lakini kumbuka walozoea kubong’oa, watabong'oa hata kabla hawajaombwa kama Shinene na kibaya zaidi watalilia kama haki yao na fashion ya kizazi chao!
 
Nchi hii bana, watu wanafiki sana. Eti hatuhitaji huo msaada....wakati hata ARV tunapewa na huyo huyo mmarekani.

Kama mmarekani anatoa hela ya ndugu zako kutahiriwa huko usukumani, what makes you think 1tr sio chochete sio lolote?
Bigirita hiyo pesa ni nyingi sana. Tuache kuweka siasa ktk vitu vya msingi.
 
Bigirita hiyo pesa ni nyingi sana. Tuache kuweka siasa ktk vitu vya msingi.
Ndio Unafiki wa Miafrika. Kujitegemea ni process na inahitaji mipango isiyo tegemezi.
Kama hatujengi productive economy unafikiri fedha za ndani zitatoka wapi? kwenye kodi hii ya arrears au?
 
Mzee Mwanakijiji,

Ujumbe mzito sana lakini kumbuka walozoea kubong’oa, watabong'oa hata kabla hawajaombwa kama Shinene na kibaya zaidi watalilia kama haki yao na fashion ya kizazi chao!
Wakati mlikuwa Mnataja hizi Kms za barabara kwa mbwembwe........tena yule jamaa anajua kukariri balaa! hamkujua kwamba Mmebong'oa?

Acheni siasa za kijinga kwenye haya mambo....


Status of MCC Funded Road Projects
Trunk roads Contracts under the MCC financing are divided into six (6) lots to ease implementation within the Compact period. All works and supervision contracts have been signed and implementation is progressing fairly well, with the Tanga – Horohoro road is taking the lead. The projects will be executed for a maximum of 27 Months period with the exception of Laela –Sumbawanga road project whose construction period is 32 months.

MCC Road Projects Making Headway

1. Tanga – Horohoro (65 km) road project
The project has been contracted to Sino Hydro Corporation of People’s Republic of China. The works contract was signed on 22nd December 2009.The contract amount is US$ 53.78 million. The project completion time is 27 months from January 2010 up to April 2012. The project is supervised by Intercontinental Pvt Limited (ICT) of India. The consultancy services for supervision of Tanga – Horohoro amounting to US$ 2,294,600. The overall work progress to date is 30% against plan of 36%

2
. Songea – Namtumbo (61 km) road project
The project has been contracted to Soges Satom Company of France. The works contract was signed on 21st May 2010. The contract amount is US$ 46,693,345.11. The project completion time is 27 months from June 2010 up to September 2012. The project is supervised by Nicholas O’Dwyer of Ireland. The consultancy services for supervision of Mtwara Corridor roads amounting to US$ 4,627,400.00. The overall work progress to date is 7% against plan of 15%

3. Peramiho Jctn – Mbinga (78 km) road project
The project has been contracted to Sino Hydro Corporation of People’s Republic of China. The works contract was signed on 02nd July 2010. The contract amount is US$ 59,845,418.07. The project completion time is 27 months from August 2010 up to October 2012. The project is supervised by Nicholas O’Dwyer of Ireland. The overall work progress to date is 4% against plan of 7.5%

4. Tunduma – Ikana ( 63.7 km) road project
The project has been contracted to M/s Consolidated Contractors Group S.A (offshore) (CCC) of Greece. The works contract was signed on 22nd September 2010. The contract amount is US$ 61,883,323.23. The project completion time is 23 months from October 2010 up to September 2012. The Consultancy Services for Supervision of Tunduma – Sumbawanga has been contracted to Egis BCEOM of France. The supervision contract amount is US$ 5,050,150.00. The overall work progress to date is 2.7% against plan of 4.2%

5. Ikana – Laela( 63.7 km) road project
The project has been contracted to M/s China New Era International Corporation of People’s Republic of china. The works contract signed on 17th September 2010. The contract amount is US$ 57,050,576.67. The project completion time is 23 months from October 2010 up to August 2012. The project is supervised by Egis BCEOM of France. The overall work progress to date is 12.1% against 15.4%

6. Laela – Sumbawanga (96.6 km) road project
The project has been contracted to Aarsleff – BAM International Joint Venture V. O.F of Nertherland. The works contract signed on April 2010 up to January 2013. The contract amount is US$ 97,141,710.00. The project completion time is 32 months from June 2010 up to January 2013. The project is supervised by Egis BCEOM of France. The overall work progress to date is 13.5% against plan of 18.
 
Mkuu kama si uelewa wangu mdogo suala ni kuwa mazingira gani yamepelekea kulazimishwa kwanza kujitegemea ghafla hivi.ubaguzi na uvunjaji wa utaratibu tulizojiwekea wenyewe ndio umetufikisha hapa
swala lakujitegemea ni swala ambalo lilikuwepo tangu serikali ya awamu ya kwanza ila baada ya awamu ya kwwanza viongozi waliokuja wengi walitegemea misaada ya wahisani ambayo ilitulemaza sio kwamba awamu ya kwanza hawakupata misaada ya wahisani lakini wahisani waliitoa wakiwa na heshima sasa hivi inafikia wakati kama cameroon alipolazimisha ushoga ingawa serikali iliyopita haikusema lolote lakini ni kama wameuruhusu kwani sasa hivi wanaofanya hivyo hawajifichi wanajitangaza waziwazi
 
MMM ule mchoro una maana zaidi. la msingi hapa ni kupigana vita vyema. ninaamini hiyo 1 trillion ilikuwa ni kama kamrahaba katika 192 mil usd zinazotoka.....je teyari tumedhibiti hizo 192 mil usd zilizotoka au tunakosa yote kwa mpigo?

cha pili sijui unaishi tanzania au nje ya nchi....pamoja na mazuri yote tunayofanya sasa kama la kukusanya mapato....je tuna uhakika kuwa tulipopanga kuweka ile trilion ambayo sasa tunaiondoa kwenda kubalance hilo GAP tunapaacha pakiwa sawia? kuna hatua kadhaa ikiwemo kuongeza kodi kutafanyika kukava hizo deficits.......kiuchumi kwa maana nyingine ni kuwa the pain is equally devided to poor citizens at the expense of some few???

yap, kuna arguments kuwa tutajijongeza kwenye gas na mafuta.....are we ready there?

issue ya msingi hapa ni kuwa kwa kuwa wewe ni baba mwenye nguvu mfukoni....utamrudishia baba mkwe wako gunia la mchele alilokutumia kwa kuwa una hela za kutosha kununua mchele wako mwenyewe??? kisa kuna wakati alikuasa usipige sana watoto? kuna haja ya kuweka mambo yote mezani na kuacha kushabikia losses ndogo ndogo zinazoepukika? ni mawazo tu...
 
wewe umeng'ang'ana na wamarekani tu, tayari kuna nchi nyingine nazo zimesitisha sasa unasemaje?. Ukiukwaji wa sheria tulizokubaliana sisi wenyewe na viongozi kuapa kuzilinda ndio laana inayotupata sasa. Kiapo si cha kuchezea
 
Back
Top Bottom