Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Miongoni ya habari ambazo zimepokelewa kwa shangwe kubwa hapa nchini, ni hii ya kusimamishwa kazi kwa aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai, Ole Sabaya
Kulikuwa na malalamiko mengi sana toka kwa wananchi, kwa kipindi kirefu kuwa huyu jamaa, anatumia ubabe, tena kwa kutumia vyombo vya dola, kuwadhulumu wananchi wasio na hatia.
Malalamiko kama kutumia silaha za moto kwa kuwanyang'anya wafanyibiashara pesa zao, zimekuwa ni tuhuma zilizozoeleka masikioni mwa wananchi, kumhusu huyo, Ole Sabaya, aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai
Hatimaye kilio hicho kimesikika kwenye mamlaka ya uteuzi, ambapo Rais wa Jamhuri ya Tanzania na Amiri Jeshi mkuu, Samia Suluhu Hassan, amelazimika kuchukua uamuzi mgumu wa kumsimamisha kazi, ili kupisha uchunguzi.
Nimediriki kuuita ni uamuzi mgumu aliochukua Rais Samia Suluhu, kwa kuwa ilizoeleka wakati wa utawala uliopita wa mwendazake, kutosikiliza kabisa vilio vya wananchi, kuhusu wateule wake.
Kwa hiyo hii iwape funzo wateule wa Rais, kuwa enzi zimebadilika na mwendazake, ambaye ndiye alikuwa "akiwakingia" kifua, sasa hayupo na tuna kiongozi mpya, ambaye kwa kipindi kifupi, alichoongoza nchi hii, ingawa yeye mwenyewe amekuwa akikaririwa akisema kuwa yeye na Magufuli ni kitu kimoja, lakini kutokana na mwenendo anaoenda nao, ni dhahiri kuwa wapo tofauti sana katika utendaji wao, wakati mwendazake alipenda sana kuendesha serikali yake kwa ubabe na kuona hakuna umuhimu wa kutotii sheria, kwa kupitia wateule wake. Huyu wa sasa, anaelekea ana hofu ya Mungu na angependa wateule wake, watekeleze majukumu yao kwa weledi na kwa kufuata sheria za nchi.
Mama Samia Suluhu ni kama vile amewasha "warning bell" na kwa hiyo wale viongozi waliokuwa wakitekeleza uonevu mkubwa kwa wananchi, hususani kwa viongozi wa vyama vya kisiasa vya upinzani kwa maelekezo ya mwendazake, watambue ya kuwa mwendazake keshatangulia mbele za haki na hivi sasa nchi ina kiongozi mpya, Rais Samia Suluhu, ambaye mwelekeo wake unaonekana una tofauti kubwa baina yake na mtangulizi wake.