Kura ya kupitisha bajeti yapigwa bila kambi ya upinzani kuwepo bungeni, yapita kwa kishindo

Nchi inaendeshwa hovyo hovyo tu , hawa jamaa wanatia hasira sn
 
Wabunge 251 wa CCM waliokuwemo bungeni wameikubali bajeti ( hawa ndio watakuja hukumiwa)
 
Wakuu,

Leo jioni wabunge wa jamhuri ya muungano wa Tanzania wameanza kupiga kura ya ama kuipitisha ama kuikwamisha bajeti ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Bajeti ni kitu muhimu hasa kwa sababu ina mchango mkubwa wa kuamua mustakabali wa mwaka ujao wa fedha pamoja na siku nyingine zijazo.

Kuna mambo mawili ya kusikitisha nimeyaona, kwanza kura zinapigwa bila kuwepo sehemu ya wabunge(wabunge wote wa upinzani) lakini pili ni kwa wabunge wote waliobaki wote kuwa na akili moja hata wale ambao mwanzo walionekana kutoridhia, yaani nasikia neno moja tu tangu kura zianze. Kuna haja wabunge wa upinzani na wa chama watafakari tulichowatuma bungeni.


Kwanini isipitishwe tu kwa KAULI MOJA YA NDIOOOOOO , Badala ya kujipotezea muda wao ?
 
Lazima mambo yaendelee, ni vyema wakatambua kuwa kususia vikao hakutolisaidia taifa hili. Ni wakati wa kuacha kutafuta cheap popularity kutoka kwa wananchi. Nashauri wananchi tusiunge mkono huu utaratibu kwa kuwa unatupoka sisi wananchi fursa ya kuwakilishwa. Kwa nini wakae nje wakati bunge linaendelea?
Usijifanye kujitoa akili.

Ulitaka wafanyaje?

Toa solution si tu unatoa maneno ya mipasho.
 
Siasa ni kusigana kwa hoja,,, sasa wao wanashindwa kutoa hoja zenye mashiko wanakimbilia kutoka nje,,, wanatoka nje kwa faida ya nani???
Hizo hoja wakitoa wanasimamishwa kuhudhuria vikao vya bunge.
 
Back
Top Bottom