Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 27,710
- 27,002
Mgombea wa chama chochote cha siasa kuchaguliwa na mpiga kura hua ni hiyari, uhuru na haki ya mwananchi mpiga kura. Mgombea wa cha siasa kukataliwa na wananchi kwa kuambulia kura zero, sio kuibiwa kura ila ndiyo hali halisi ya mgombea husika mbele ya wapiga kura. Ni muhimu sana kwa wagombea wanao kataliwa na wananchi kwa kuambulia kura zero, kukubali hali hiyo halisi na daima kua wangwana na kujipanga upya na chaguzi nyingine zijazo. Huenda mgombea uongozi huyo hajaeleweka vyema na kukubalika kwa wananchi kwa wakati huo.
Kama taifa la kidemokrasia Tanzania,
ni vizuri kujiepusha na dhana au nadharia potofu ya kuibiwa kura hali ya kua hukupigiwa kura wala hukuchaguliwa na mpiga kura yeyote eneo mahalia la kupigia kura. Ni upotoshaji wa kiwango cha juu sana kudai kuibiwa kitu ambacho huna, hususani kura zero. Ni vizuri kukubali kwamba ukikataliwa au ukikubaliwa na wananchi hiyo ndio demokrasia yenyewe.
Tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu wa kihistoria Tanzania, uchaguzi ambao utakua ni huru zaidi, wa wazi zaidi na wa haki zaidi ya chaguzi zote ziliozowahi kufanyika Tanzania tangu tupate uhuru, ni vizuri sana wagombea wa vyama vyote vya kisiasa, katika nafasi zote urais, ubunge na udiwani, kujiandaa na hali hiyo ya matokeo ya uchaguzi ya ama kukataliwa vibaya sana na wanachi au kukubaliwa sana na wananchi, bila kusingizia kuibiwa usichokua nacho na kusababisha fujo.
Vyama vyote vya siasa nchini na wagombea uongozi wao kwenye Uchaguzi mkuu ni vema kujiandaa kikamilifu kupokea matokeo yao ya kukubaliwa au kukataliwa kwa kura zero na wananchi kwa amani
Mungu Ibariki Tanzania