MzalendoHalisi
JF-Expert Member
- Jun 24, 2007
- 4,664
- 1,594
Taifa la ajabu ajabu sana eti mimi naitwa Dr samia na unapenda ukiitwa hivyo kwa faida ya nini ni ushamba tu! Mwalim Nyerere na umahiri wake hawahi kuitwa Dr Nyerere
Hizo hazipaswi kuitwa PhD, ni DL yani Doctor of Letters. PhD inasotewa, DL inapewa tu haIsomewi, kuitwa Dr .... ni makosaNinaomba michango yenu !
Kumekuwa na tabia watu kupewa Phd ambazo Sio Za kusomea wanspita mitaani wakikutana Phd( Dr)
TCU njooni Jf!
Hoja hii ilikuwepo Rais Samia hapaswi kuitwa DaktariWanabodi,
Tuiombe TCU ilifafanue hili, kwa kuzingatia hoja ya Prof. Joseph Kironde
Wananchi, rukhsa kuwaita Daktari, na kwenye mikutano ya kawaida, ila kwa sisi media, na kuandikwa kama title, hili linahitaji Ufafanuzi wa TCU, na baada ya TCU kulifafanua, MCT nayo ilitolee muongozo kwa vyombo vya habari kuhusu kuwataja au kuwaandika madaktari hao.
La mwisho, ni kwa madaktari wenyewe hao wa heshima.
Hivyo kwenye hili la kuitana titles za udakitari wa heshima, kugeuzwa ni title rasmi, kitendo cha watwa kutokemea, au kukaa kimya, tafsiri yake ni wanapuuza tuu kwasababu sio wao wanao jiita madaktari, ni maadam ni title ya heshima, kuna ubaya gani mtu kuheshimika na kuitwa title ya heshima ya usomi ubobezi na ubobevu ili hali ni title ya heshima tuu?, hivyo kuitwa anahesabika kuridhia!, jee tuwashauri viongozi wetu wakemee?.
Wasalaam
Paskali
True, naunga mkono hoja, PhD za Honoria Causa, sio official title ya kuitwa Dr, ila kwenye social gatherings na kwenye events ni sawa kumu address as Dr. na ndio maana kwenye press release za ikulu, huwezi kuona Rais Samia akiandikwa Dr.Utaratibu wa doctorates ni kwamba, mtu anayetakiwa kuitwa DOKTA ni yule tu ambaye aliusomea huo udokta darasani (PhD), mfano Dr. Magufuli, Au Dr. Tulia.
Mtu aliyetunukiwa udokta wa heshima hapaswi kabisa kuitwa au kujiita DOKTA. Udokta wake unabaki kuwa wa heshima na sio udokta wa TITLE. Hizi ni kanuni za utoaji wa Doctorates.
Samia hapaswi kuitwa DOKTA SAMIA kwa sababu hakusomea udaktari (PhD). Alitunukiwa tu.
Hapana hii kapewa ya mgao wa umeme, ukosefu wa maji, dola na petrol
Wanabodi,
Kiukweli kabisa mfumo dume bado ni tatizo kubwa kwa baadhi ya Watanzania wenzetu na haswa wa Kanda yetu fulani!.
Japo Rais Nyerere, Mwinyi na Mkapa, walitunukiwa PhD za heshima za honoris causa lakini hawakuitwa kwa title za Dr. Lakini Rais Jakaya Kikwete baada ya kutunukiwa aliitwa Dr na hakuna aliyepinga wala kupiga kelele, ila baada ya Rais Samia kutunukiwa PhD na kuanza kuitwa Dr, kelele zimeanza,
Anastahili
Hili kweli is not right, PhD za honoris causa, hazibadili title ya mtu kuitwa Dr!. Mwalimu Nyerere alipewa na hakuitwa Dr, Ali Hassan Mwinyi alipewa na hakuitwa Dr. Benjamin Mkapa alipewa na hakuitwa Dr. Jakaya Kikwete alipewa na akaitwa Dr, sasa kama JK aliitwa Dr kwa PhD ya honoris causa, na hatukusema wala kupinga, now Mama kapewa, why sasa ndio tunasema na tunapinga?.
Tuiombe TCU ilifafanue hili, kwa kuzingatia hoja ya Prof. Joseph Kironde View attachment 2778748
Usikute sio yeye, au usikute...
ila kwa vile JK aliitwa na hakugoma, why not her?.
Kuna mtu kujiita Dr, Professa, tulikuwa na Profesa Matikisa, Profesa Singira, Profesa Maji Marefu, Dr. Manyaunyau, Dr. Ngwizukulu Jilala, Dr. Mwaka, rais wa Manzese, rais wa Wasafi, rais wa Yanga, hakuna ubaya wowote mtu kujiita vyovyote, na kuna kuitwa, sio wewe bali wanaokuita, Dr, Prof, rais au kuitwa vyovyote pia hakuna ubaya wowote mtu kuitwa vyovyote as long as ni informally, lakini unapoandika jina lako kwenye usajili wowote, lazima utatumia majina rasmi na title rasmi.
Rais mstaafu wa Marekani, Barack Obama, ametunukiwa Ph. D za heshima 14!, lakini huwezi kusikia popote akiitwa Dr au kuandikwa Dr.
Kwa vile huu utaratibu wa shahada za heshima, sio utaratibu wetu wa jadi zetu, viongozi wetu wanapotunukiwa Ph. D hizi, ni vyema tukaufuata utaratibu na utamaduni wa shahada hizo.
Wananchi, rukhsa kuwaida Daktari, na kwenye mikutano ya kawaida, ila kwa sisi media, na kuandikwa kama title, hili linahitaji Ufafanuzi wa TCU, na baada ya TCU kulifafanua, MCT nayo ilitolee muongozo kwa vyombo vya habari kuhusu kuwataja au kuwaandika madaktari hao.
Sisi washauri wa bure, tumeikubali hii title ni well befitting her na tumeshauri Baada ya kutunukiwa PhD na kuwa Dkt. mnaonaje jina la "Mama" sasa tukaachana nalo ila Nyumbani wanaweza kuendelea kumuita Mama?
La mwisho, ni kwa madaktari wenyewe hao wa heshima.
Nakumbuka kwenye moja ya matukio yaliyokuwa yakitangazwa live Mubashara na TV zetu, mmoja wa viongozi aliteleza ulimi na kumuita Mkuu wa nchi "Mheshiwa Mungu" mbele ya Mkuu huyo wa nchi, Mkuu yule alicheka tuu kwa kujua mzungumzaji ni ameteleza tuu ulimi.
Yule aliyeita Mheshimiwa Mungu, hakuomba radhi, bali alirekebisha tuu na kuendelea,
View: https://youtu.be/6y3V86aZYf0?si=kJQf8vmFWBtauuAC
Na Mkuu wa nchi alipokuja kuhutubia, aliendelea tuu na hotuba yake as if nothing happened!. Kikichokuja kutokea is now a history!, kwasababu hakuna ajuye sababu, this could have been kulichangia!.
Alichopaswa kufanya Mkuu wa nchi ni kukemea!. Huwezi kuitwa Mungu kimakosa radhi isiombwe na wewe kuendelea as if nothing happened!.
Hivyo kwenye hili la kuitana titles za udakitari wa heshima, kugezwa ni title rasmi, kitendo cha watwa kutokemea, au kukaa kimya, tafsiri yake ni wanapuuza tuu kwasababu sio wao wanao jiita madaktari, ni maadam ni title ya heshima, kuna ubaya gani mtu kuheshimika na kuitwa title ya heshima ya usomi ubobezi na ubobevu ili hali ni title ya heshima tuu?, hivyo kuitwa anahesabika kuridhia!, jee tuwashauri viongozi wetu wakemee?.
Kufuatia maendeleo ya utandawazi kumeibuka vyuo vikuu vya mtandaoni, online universities zinazouza shahada za kununua, bila hata kuingia darasani, vyuo vikuu hivi vya mtandaoni vina issues Ph. D za heshima kwa kulipia tuu tena ni dola 100 tuu!, hili lisipotolewa muongozo na ufafanuzi, utafikia wakati tutashindwa kutofautisha yupi ni Daktari wa kweli wa kusomea, Daktari wa heshima, na Daktari wa kununua makaratasi, tutakuja kuichanganya jamii yetu.
Mbona kwa wanasheria hili limewezekana ili mtu kuwa wakili, lazima uthibitishwe na Jaji Mkuu wa Tanzania na kusajiliwa na Chama cha Mawakili Tanganyika, hivyo TCU yenye jukumu la kutoa ithbati ya vyuo vikuu, hii madaktari wa heshima kuitwa madaktari na kuandikwa madaktari , kuna haja ya kulitolea ufafanuzi au tuiachie tuu?.
Wasalaam
Paskali
Maza ni mpenda sifa snWatu wote wavivu wa kusoma hupenda uhuni ktk mambo mengi na hupenda short cut,kama tunawapenda sana viongozi wetu tuwasihi wakasome shule,yaani chini ya CCM ELIMU inadhalauliwa sana.