Kuelekea 2025 Kumekucha CCM: Nape na Makamba 'waula', walitumbuliwa ili kutambuliwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,136
17,871
Haya ndiyo mambo ya kutumbuliwa ili kutambuliwa. Mawaziri wa zamani Nape Nnauye na January Makamba wamejumuishwa kwenye Kikosi Maalum cha CCM kinachoandaa Ilani ya CCM ya mwaka 2025 hadi 2030. Kikosi hicho kinaongozwa na komredi Stephen Wassira.

Nyaraka za kichama zinaonesha kuwa Nape na Makamba sasa wamejumuishwa kwenye Kikosi hicho ili kuongeza nguvu ya uandaaji wa Ilani ya CCM ya uchaguzi ujao. Kwakuwa Ilani hubeba maono na mipango ya kila sekta, inaaminika kichama kuwa Nape na Makamba watatumia weledi wao kisiasa kupatikana kwa Ilani bora.

Tayari Nape na Makamba 'wameshajitambulisha' kwa Wassira pamoja na wajumbe wengine wa Kikosi hicho. Sasa ni dhahiri kuwa Nape na Makamba wamepumzishwa uwaziri ili kupewa nafasi ya kuisuka Ilani ya CCM. Inasemwa na waandamizi kuwa majukumu ya uwaziri yangewanyima nafasi ya kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo.

Weledi na ukomavu wa akina Nape utaunganishwa na wa akina Wassira, Kabudi, Lukuvi na wengineo ili kupata Ilani bora ya CCM-nyaraka muhimu katika kuomba na kueleweka uchaguzini mwaka 2025. Kuna uwezekano mkubwa kuwa wote watarudi barazani baada ya uchaguzi wa 2025 na Kikosi hicho kutunukiwa nafasi ya Waziri Mkuu.

Kampeni zimeshaanza au tusubiri wakati wa uchaguzi?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
 
Wana weledi gani hao. Labda kama nikuwatolea aibu au kuwazuia wasianzishe zengwe lingine dhidi ya mama. Hao wanavyopenda uwaziri nini kingine kinaweza kuwaridhisha. Ilani ya uchaguzi ni uchumi na ustawi wa jamii kuliko siasa. Niambie Nnape anaweza kuweka input gani hapo :cool:. Hao wapigaji kwanza wataweka porojo tu. Kabudi na wassira hapo naona sahihi.
 
Kumbe ndio maana nchi haipigi hatua.

Watu wakifikishiwa huduma ya maji eti wanampongeza rais, yaani watu wanampongeza mtu wakati ni matunda ya kodi zao?

Hii yote inatokea endapo kwenye stronghold ya chama eti January na Nepi nao wanaonekana kama think-tanks.
 
Haya ndiyo mambo ya kutumbuliwa ili kutambuliwa. Mawaziri wa zamani Nape Nnauye na January Makamba wamejumuishwa kwenye Kikosi Maalum cha CCM kinachoandaa Ilani ya CCM ya mwaka 2025 hadi 2030. Kikosi hicho kinaongozwa na komredi Stephen Wassira.

Nyaraka za kichama zinaonesha kuwa Nape na Makamba sasa wamejumuishwa kwenye Kikosi hicho ili kuongeza nguvu ya uandaaji wa Ilani ya CCM ya uchaguzi ujao. Kwakuwa Ilani hubeba maono na mipango ya kila sekta, inaaminika kichama kuwa Nape na Makamba watatumia weledi wao kisiasa kupatikana kwa Ilani bora.

Tayari Nape na Makamba 'wameshajitambulisha' kwa Wassira pamoja na wajumbe wengine wa Kikosi hicho. Sasa ni dhahiri kuwa Nape na Makamba wamepumzishwa uwaziri ili kupewa nafasi ya kuisuka Ilani ya CCM. Inasemwa na waandamizi kuwa majukumu ya uwaziri yangewanyima nafasi ya kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo.

Weledi na ukomavu wa akina Nape utaunganishwa na wa akina Wassira, Kabudi, Lukuvi na wengineo ili kupata Ilani bora ya CCM-nyaraka muhimu katika kuomba na kueleweka uchaguzini mwaka 2025. Kuna uwezekano mkubwa kuwa wote watarudi barazani baada ya uchaguzi wa 2025 na Kikosi hicho kutunukiwa nafasi ya Waziri Mkuu.

Kampeni zimeshaanza au tusubiri wakati wa uchaguzi?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
Unataka kusema Chama hakina watu muhimu na wakomavu katika siasa hadi ilani ikaandaliwe na Nape?
 
Wana weledi gani hao. Labda kama nikuwatolea aibu au kuwazuia wasianzishe zengwe lingine dhidi ya mama. Hao wanavyopenda uwaziri nini kingine kinaweza kuwaridhisha. Ilani ya uchaguzi ni uchumi na ustawi wa jamii kuliko siasa. Niambie Nnape anaweza kuweka input gani hapo :cool:. Hao wapigaji kwanza wataweka porojo tu. Kabudi na wassira hapo naona sahihi.
Wassira ana nini?
Huyo mzee na akina Nape ni wale wale afadhali ya January kuliko Wassira.
 
Back
Top Bottom