Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,012
- 121,292
Saudia Arabia haiwezi kuguswa
Saudia ni large exporter wa petrol duniani ana export 17%+ ,huku wengine waki export 2%.
USA na saudia ni marafiki na washirika ,saudia akimuambia USA afanye hiki lazima atafanya refer ishu ya Yemen
Kingine petrodollar,saudia na USA ndio waasisi wa petrodollar ..saudia amemuahidi
USA atamlindia petrodollar na USA amemuahidi saudia atamlindia maslahi yake ..so Trump hana uwezo na hawezi kumzuia saudia mfano mzuri ni congress walivyotaka mwaka Jana waishitaki saudia ,saudia akapiga mkwara wake ishu imemalizwa na kupotea juu juu ..
Dollar ya USA inashikiliwa na saudia ,jeuri "Dollar" ya USA inashikiliwa na USA ..saudia ni untouchable
Kumfungia Iran ni ujinga na Trump kaonyesha chuki waziwazi ,ktk nchi ambazo Trump anazichukia kikweli kweli ni Iran&China ,haswa dharau waliyoifanya Iran mwaka Jana kuwakamata wanajeshi wa USA Trump alilalama sana.
Trump akiigusa saudia Arabia urais wake utakuwa mashakani na kujiwekea kisu shingoni
Ila uzuri Iran hanaga kujipendekeza ,ana uhasama na saudia ,USA lakini anafanya mambo yake vizuri anatengeneza makombora yake ,teknolojia yupo vizuri na hategemei misaada ..big up Iran
Israel ni mtoto wa mama na hawezi kuguswa
Saudi Arabia ni ally wa Marekani.
Unajua maana ya ally?
Ukweli kwamba Saudi Arabia ndiko walikotokea maghaidi wengi wa 9/11 haimaanishi kwamba hata huo ughaidi wao ulipangwa ndani ya Saudia.
Ughaidi wao ulipangwa kwenye ma milima ya Afghanistan huko.
Na Saudia, kwa vile ni nchi mshirika wa Marekani, huwa inasaidiana na Marekani katika mambo mengi ikiwemo kukamata watu wanaojihusisha na hayo mambo ya kighaidi.
Sasa kuna sababu gani ya kumwadhibu mshirika wako?
Ushirikiano ambao Saudia inatoa kwa Marekani ni tofauti kabisa na ushirikiano ambao Yemen na Iraq zinatoa kwa Marekani.
Hivyo, kwa kifupi ni kwamba, mshirika wako huwezi kumwadhibu kwa sababu huwa anakusaidia na wewe.