Kuku wangu 1 anataga mayai 3-4 ndani ya masaa24!

Hii sio kweli
 
Mkuu punguza akili za kijima, kwani umepata madhara gani kula hayo mahindi au kuku?
 
Anafugwa kienyeji 100%
Bado haisaidii
Mkuu punguza akili za kijima, kwani umepata madhara gani kula hayo mahindi au kuku?
Yaani kama hujui madhara ya kula kuku hawa wa kisasa na mayai ya kisasa. Na mahindi na mpunga huu wa kutumia madawa na mbolea...! Basi wewe unaishi tu ili mradi ufike utakapoishia.

Unafikiri haya magonjwa ya uvimbe uvimbe,matatizo ya viuno,matatizo ya nguvu za kiume kwa vijana wengi siku hizi. Kwa uchache hayo yanatokana na nini? Na magonjwa siku hizi ni mengi tena ya ajabu ajabu. Yote hayo yanatokana na haya mavyakula yenye madawa na mbolea. Wewe unabugia tu ndugu?

Kwa taarifa yako mazao yanahitajika sana ulayo kama cocoa,parachichi hizi wanatuma na watu kabisa wa mafunzo namna gani yapandwe. Wanasisitiza yatumie mbolea za wanyama(samadi). Yasipuliziwe dawa. Hata wakihitaji mchele tu wanahitaji ule ambao haujatumia mbolea za kiwandani,pia usiotumiwa dawa za kiwandani. Wanakuja na kipimo kabisa kujua kama umetumia mbolea za kiwandani
 
Tunaambiwa kwenye history mtemi milambo wa tabora alikufa kwa ugonjwa wa kansa ya ukoo ina maana na yeye alikuwa anakula kuku wa kizungu na ugali wa mahindi ya kisasa?

Hayo magonjwa yote uliyotaja yalikuwepo hapo kabla gonjwa jipya ni ukimwi pekee yake. Kichatugharimu siku hizi ni lifestyle tunakula mavyakula mengi huku tukiwa hatuna shughuli nzito za kuburn calories hii ndio sababu kuu ya kuongezeka kwa vifo na sio vyakula.
 
Jaribu kutafuta Jogoo mzuri alafu mayai yake uyatotoleshee, watoto uwafanyie selective interbreeding upate breed ya kuku wanaotaga hvyo wote
 
Pole sana. Endelea ulipoishia. Kutokujua Jambo tunaita uko gizani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…