Kuhamia Dodoma: Haya ndio mateso kwa wananchi,watumishi na tanuru la kuchoma kodi

KWANI KINACHO WASHINDA HAO WAKURUHWENZI KUHAMIA DODOMA NINI HADI WAAMUE NENDA RUDI YA DAR - DOM
Hao watumishi waliobaki Dar wataongozwa na nani? Link ya Dodoma na Dar ni hao wakurugenzi,wizara INA watumishi tuseme 600,walioenda Dodoma 50,kiutawala unafanyaje?
 
Wananchi wangapi ambao hupata huduma moja kwa moja toka wa Waziri au Katibu Mkuu? Au unaongelea wapiga dili?
Hujawahi kusoma zile barua zimeandikwa "BARUA ZOTE ZIELEKEZWE KWA KATIBU MKUU" ...yeye ndiye mwenye wizara/ofisi
 
Wacha dodoma waingiliwe nao waanze kujua maana ya ugumu wa maisha sio kukaa omba omba na kubweteka na maisha.....

nafikiri watanielewa wakianza kupanda tax kwa elfu 10 baada ya elfu 5 waliozoea.....
Tushawapandishia bei ya nyumba....... watajiju

Sasa hivi ni.mwendo.wa kupachika tofali fasta fasta vichwa vinakuja
 
Mtoa hoja ni mgonjwa wa kufikiri. Anajiangalia mwenyewe tu. Hoja zake hazina mashiko. Ni hewa tu. Uamuzi wa kuhamia Dodoma ni uamuzi wa busara sana. JPM ametumwa na Mungu kutekeleza hili.Wafanyakazi wanaopinga waache kazi. Mitaani kuna watu wengi hawana ajira na ni wasomi wazuri tu.
Hujajibu habari alizoleta.

Hata kama kuhamia Dodoma kunaweza kuwa uamuzi wa busara, ametoa points nzuri kutuonyesha kwamba utekelezaji wake si wa busara.

Hujazijibu point alizotoa.
 
japo mimi siipendi ccm.. ila kuamia dodoma ni uamuzi wa busara sana...

wizara zinahudumia nchi nzima... kuna mikoa kutoka huko hadi kufika dar ni mbali sana.. angalau dodoma inafikika na mtu anaetoka mkoa wowote kiurahisi..

changamoto ni kawaida tu.. hata ukiwa unahama nyumba moja kuhamia nyingine sio rahisi....

within 3 yrs wizara zitakuwa zimeseto dodoma zinaaendelea na huduma huko...

unafikiri zikikaaa dar kuogopa changamoto dodoma wataamia kweli?? wahame tu
unajua maana ya globalization? Siku hizi hata Washington DC ni kama Temeke mikoroshini na tandika! Mazingira, technology nk zimebadirika!

Sababu za kuhamia huko za Mwaka 1978 hazipo tena! au wewe mwenzetu unaandikaga P.O. Box mpaka Leo? nadhani kila kitu kimebadirika na serikali ingezingatia hilo!
 
Hao watumishi waliobaki Dar wataongozwa na nani? Link ya Dodoma na Dar ni hao wakurugenzi,wizara INA watumishi tuseme 600,walioenda Dodoma 50,kiutawala unafanyaje?
kwani wakati wanaishi Dar hawa watumishi wa mikoa mingine ukiwemo Dodoma waliongozwa nakusimamiwa na nani,
 
Huu mradi wa kuhamia dodoma ulianza kuimbwa miaka kadhaa iliyopita lakini haukuwahi kufanikiwa,kimsingi,ulibaki vitabuni tu.

Hatimaye miujiza imetokea,na sasa serikali,kidogo iko dodoma kwa ajili ya Ku satisfy daftari la mahudhurio.

Kinachotokea ni nini?

Waziri,katibu mkuu,naibu katibu mkuu,na baadhi ya wakurugenzi wako dodoma,wataalam wengi waliobaki wako Dar es salaam,hawa watu wanafanyaje kazi bila wataalamu wao.Hapa ndipo posho hunoga,

Mawaziri,katibu wakuu na baadhi ya wakuu wa idara huja Dar es salaam kuhudumia wataalamu waliowaacha,watakaa Dar kama wiki moja, wakila posho zao Nene,baadae hurudi Dodoma,

Wakati huo huo wataalam nao hupishana njiani,huyu anaenda Dodoma yule anarudi kupeleka na kurudisha nyaraka mbali mbali.

Kwa wananchi je? Mwananchi anafika Dodoma ana shida na waziri au katibu mkuu au mkuu wa idara fulani, anajihimu,anapanda basi mpaka Dodoma analala,asubuhi anaamkia wizarani, salaalee!!anaambiwa waziri yuko Dar na atakaa wiki moja,kama unaweza mfate,anapanda basi tena(gharama)anafika Dar anakutana na waziri,waziri anamkabidhi kwa wataalam,wanamhudumia,wakimaliza,wanamwambia hili suala lazima lipitishwe na katibu mkuu,kama unaweza rudi Dodoma....


Upande wa majengo,sasa asilimia zaidi ya 98 ya wizara zote zimepanga majengo(kwenye bajeti ilikuwemo?) Wale maofisa nao waliostahili nyumba wamepangishiwa Dodoma na wameacha Nyumba zao tupu Dar es salaam....kodi inalika.

Sasa kila siku Barua inafika Dar inapelekwa Dodoma ...inarudi Dar....gharama za usafirishaji.

Nadhani haya ni mateso ambayo yatafuatiwa na bajeti ya ujenzi wa majengo ya ghorofa kwa ajili ya wizara huko dodoma kuanzia mwakani wakati pesa hiyo ingefaa kuboresha afya,maji na elimu.

Kiuchumi,hakuna tija kuhamia Dodoma ....kuhamia Dodoma hakuongezi pato la taifa,

Kiusalama kuhamia dodoma hakuna tija ....siku hizi kuna inter continental ballistic missile,mtu kakaa baharini anarusha kombora kigoma.

Kama taifa ....hatujaambiwa eti viongozi wakikaa dodoma ndio tutapata maisha bora.

Kuhamia Dodoma nakufananisha na kujenga Nyumba kwa tofali za barafu!!!
Ngoma zaidi ni cc tunaotumia barabara dar dodoma kama ni wimbo wao wa hapa kazi wamechemsha , eti wakiwa wanatoka tu ikuru gari zoote zilizoko njiani kutoka dar mpaka dodoma zinasimamishwa zote zinaamrishwa zisimame kuna msafara wa eidha rais makamu na au wazirr mkubwa .

Mtakaa kwenye gari masaa mengi sana bira huruma jaman tunaomba mgebaki hukohuko dar au mngebaki ddm maana mlituhakikishia kuwa utawala wenu utakuwa wa kazi tu mbona sasa mnatugalagalaza barabarani kazi tutafanya saa ngapi ikiwa tunashinda tunawasubiri mpite ndio na cc tuendelee na safari tunaomba bas kama mnaenda safari tumieni bombandier ili kupunguza mwingiliano wa barabara. mbona kama kutukomesha sie tumekoma.bana tunajua hakuna binadamu aliyekamilika laki hii inatukumbusha kuwa ni viburi tu vya kibinadamu.

Kumbuken bas hapa kaZi tu.
 
Walioko dar wamepewa mamlaka kamili kuhudumu na walioko dom pia wana mamlaka kamili kuhudumu
 
Uamuzi wa kuhamia idodomya kidharura dharura ni wa kisiasa zaidi kuliko vinginevyo. Yaani ni ili kuwe legacy ambayo imeonekana ngumu kwa watangulizi.
Uamuzi wa kuamia idodomya ni mzuri na ulipangwa na mimi ninavyoona unatekelezeka vizuri tu.....uzuri wa serikali yetu ya sasa ipo makini kwa itendaji....
 
Walioko dar wamepewa mamlaka kamili kuhudumu na walioko dom pia wana mamlaka kamili kuhudumu
 
Wasafiri wanaotumia barabara hiyo kwenda mikoa ya kanda ya ziwa wanapata kero,cha ajabu ndege zipo lakini hawapandi
Ngoma zaidi ni cc tunaotumia barabara dar dodoma kama ni wimbo wao wa hapa kazi wamechemsha , eti wakiwa wanatoka tu ikuru gari zoote zilizoko njiani kutoka dar mpaka dodoma zinasimamishwa zote zinaamrishwa zisimame kuna msafara wa eidha rais makamu na au wazirr mkubwa .

Mtakaa kwenye gari masaa mengi sana bira huruma jaman tunaomba mgebaki hukohuko dar au mngebaki ddm maana mlituhakikishia kuwa utawala wenu utakuwa wa kazi tu mbona sasa mnatugalagalaza barabarani kazi tutafanya saa ngapi ikiwa tunashinda tunawasubiri mpite ndio na cc tuendelee na safari tunaomba bas kama mnaenda safari tumieni bombandier ili kupunguza mwingiliano wa barabara. mbona kama kutukomesha sie tumekoma.bana tunajua hakuna binadamu aliyekamilika laki hii inatukumbusha kuwa ni viburi tu vya kibinadamu.

Kumbuken bas hapa kaZi tu.
 
Sababu za kuhamia Dodoma miaka ya 70 yawezekana hazipo leo.
Lakini kuwa na miji mikuu miwili yaani Dodoma Utawala na Dar Biashara kwa hali ya sasa ya uchumi itatugharimu.
Ifike wakati mwingine maamuzi kama haya ya kuhamia Dodoma yangerudishwa kwa wananchi wakajadiri upya.
Dodoma ina upepo mkali na vumbi kali,je mmeishapanda miti ya kupunguza kasi ya upepo na vumbi?
 
Back
Top Bottom