Kufungua biashara iliyo nje ya taaluma yako, ni upotevu wa ada kwa yule aliyekusomesha

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,638
40,855
Wengi tunaamini kuwa, tunachokisoma mashuleni na vyuoni, ndivyo tunavyoenda kuviishi huko mtaani.

Tunategemea mtu aliyesoma fani kama udaktari wa kutibu, uhandisi, uanasheria, uhasibu, ugavi, masoko n.k aende akaishi kile alichokisomea, iwe kwa kuajiriwa au kwa kujiajiri.

Changamoto iliyopo kwa sasa hivi; utakuta mtu kahitimu labda sheria, mambo ya utawala, uhandisi wa mifumo, siasa na utawala n.k unamkuta yupo anafanya biashara labda ya kuuza nguo, viatu n.k ambayo haiendani na fani alioisomea.

Hiyo tunasema, ni matumizi mabaya ya ada au upotevu wa fedha.​
 
Swala la kwanini nilisoma halina umuhimu maana nishasoma mkuu, kuna maswala kama uelewa mdogo kwenye course selection, kusalitiwa na marefarii, kufata mkumbo na nk
:D:D:D. ieleweke tu, kufanya shughuli yoyote nje ya taaluma yako ulioisomea; huo ni upotevu wa ada, kwa sababu ile elimu haikusaidii; bora ile fedha ingetumika hata kwa kulimia mpunga​
 
:D:D:D. ieleweke tu, kufanya shughuli yoyote nje ya taaluma yako ulioisomea; huo ni upotevu wa ada, kwa sababu ile elimu haikusaidii; bora ile fedha ingetumika hata kwa kulimia mpunga​
Na kitendo cha kunizuia nisifanye kitu nje ya taaluma yangu ni upotevu wa rasilimali mkuu yaan nimepoteza pesa na bado unataka nipoteze nguvu kazi pia
 
Mkuu labda unaongelea huko nchi za ulaya lakini hapa Africa itakiwa ngumu, professional zingine zinahitaji mtaji mkubwa ili uweze kuishi kulingana na professional yako mfano mtu amesome mambo ya petrol na gas,
 
Nakubaliana na wewe; tatizo linakuja kwenye uchaguzi wa fani
 
Back
Top Bottom