Kufunga ndoa na ujauzito ikoje kiimani?

Wadau,

Kuna hili swala huwa inatokea mtu anafunga ndoa mwanamke akiwa na ujauzito wake tayari, tena tumbo unakuta ni kubwa au kuzaa mtoto kwanza ndio ndoa inafungwa, hili swala kiimani limekaaje ni ruhusa au wachungaji/mashehe wanalazimisha?
Katika Uislam Mwanamke haruhusiwi kuolewa akiwa katika Hali ya Ujauzito atasubiri mpaka eda yake iishe ambayo ndio kujifungua kwake kwaiyo ataolewa baada ya kujifungua ila kwafaida Mwanamke anaweza akapewa Talaka ktk hali hii!!!!
 
Kuna mchungaji nilimsikia akisema,ndoa ni agano baina ya watu wawili, sasa mwanamke akiwa na mimba anaongezeka mtu wa tatu kwenye agano hilo
Kwa baadae unakuta hao watoto wanakuja kutembea na baba zao au kama ni wa kiume unakuta wanakuwa mashoga maana agano la ndoa lina nguvu
 
Nii swala kubwa na pana kidogo lakin kufunga ndoa ni jambo la heri kutoka kwenye thambi na kufwTa baraka. My side naona poaa
 
Lakini hii kitu bana, hivi bado inaendelea? yaani kuna wakati ilikuwa kila harusi na mimba, utafikiri watu tulikuwa hatuwezi olewa bila mimba.
Kama ni dhambi ya kuzini ishatendeka cos Kiimani si sahihi kabla ya ndoa, kujaribu kuhalalisha kwa kufunga ndoa kabla mtoto kuzaliwa sidhani ni sawa kiimani. Ni taratibu tu tuliyojiwekea wanadamu kujifariji baada ya kukosa.
 
Unafunga ndoa n.a. mkeo na mtoto tumboni wote mnakua mmeunganishwa mama na mtoto
Baba n.a. mtoto
 
Tatizo letu tupo katika zama ambazo haraam imekua halali na hatuoni kama ni tatizo,,..zinaa ni kitendo kichafu na ndoa sio suluhisho la kufuta kosa hilo..kwanza inabdi watubie kwa Mola wao toba ilio ya kweli,baada ya hapo wasubiri mtoto azaliwe ndio ndoa ifungwe..
Unamnyima mtoto haki zake nyingi sana kidini kwa kumzaa nje ya ndoa.

Hii ni kwa imani ya Kiislam.
 
Sidhani kama uko sahihi mkuu
Huo ndio ukweli lile ni agano la watu wawili hatakiwi kuwepo mtu wa tatu sasa kama mwanamke anaujauzito mtajikuta wote watatu mnaunganishwa kuwa kitu kimoja, tatzo watu wanaraihisha mambo ili kuhalalisha wayafanyayo si sawa
 
Tatizo letu tupo katika zama ambazo haraam imekua halali na hatuoni kama ni tatizo,,..zinaa ni kitendo kichafu na ndoa sio suluhisho la kufuta kosa hilo..kwanza inabdi watubie kwa Mola wao toba ilio ya kweli,baada ya hapo wasubiri mtoto azaliwe ndio ndoa ifungwe..
Unamnyima mtoto haki zake nyingi sana kidini kwa kumzaa nje ya ndoa.

Hii ni kwa imani ya Kiislam.
Huo ndio ukweli
 
Kuna mchungaji nilimsikia akisema,ndoa ni agano baina ya watu wawili, sasa mwanamke akiwa na mimba anaongezeka mtu wa tatu kwenye agano hilo
Kwa baadae unakuta hao watoto wanakuja kutembea na baba zao au kama ni wa kiume unakuta wanakuwa mashoga maana agano la ndoa lina nguvu
Haswaaa kuna jamaa kabisha hapo juu ukifuatilia unagundua huu ndio ukweli mtoto anapata wapi ujasiri wa kumpanda mama yake,au bint anapata wapi ujasiri wa kulala baba yake na kuanza kumuonea wivu mama yake
 
Wanaoelewa mtoto wa nje ya ndoa ana status gani hawasubiri mpaka mdada ajifungue... Kuna rafiki yangu alifunga ndoa wakati mimba ina miezi nane... Walienda tu kwa mwenyekiti na gauni lake la kawaida wakafunga ndoa yao na kurudi kufanya kapati ka familia... Aligoma kabisa mtoto wake azaliwe nje ya ndoa

Watu wengi sana sio sasa tu hata zamani wamezaliwa nje ya ndoa, baadae ndio wazazi wakafanya process zote. . And they have turned up to be beautiful human beings kuliko waliozaliwa ndani ya ndoa

Mtoto process yake inaanza toka fertilization ya yai, kwa hiyo hata ukimbieje na tumbo la miezi 8 kwenda kuolewa that child is already 'a bastard' (according to you). . Kuwa na tumbo kubwa unaprove uzinifu wako tayari
 
Wadau,

Kuna hili swala huwa inatokea mtu anafunga ndoa mwanamke akiwa na ujauzito wake tayari, tena tumbo unakuta ni kubwa au kuzaa mtoto kwanza ndio ndoa inafungwa, hili swala kiimani limekaaje ni ruhusa au wachungaji/mashehe wanalazimisha?
Kiimani zote ni DHAMBI ,tusipindishe maneno..

Yaani kwanza Watu WANAZINI ambapo jina lao sahihi linakuwa WAZINIFU yaani walioamua kumpinga MUNGU sheria zake kwa KUJAMIIANA kabla ya KIBALI CHAKE.

WAKISHA ZINI sasa ndiyo WANABEBA huo USHAHIDI wa ZINAA yao kwenda kumwambia MUNGU tuhalalishie ZINAA YETU HII..

Kwa Waislamu hii inabaki kuwa yule mtoto anayezaliwa anakuwa wa MWANAMKE,na WAKRISTO ANATAKASWA kuwa halali yaani kwa ile ya MLIFUNGALO DUNIANI,LIMEFUNGWA MBINGUNI na MLIFUNGUALO DUNIANI LIMEFUNGULIWA MBINGUNI.

Wengi hutiana hizi MIMBA kwa kuogopa kuoa TASA ila si HALALI na pia kuogopa ile KUZAA NJE YA NDOA wakati WAMETIANA MIMBA NJE YA NDOA.
 
Back
Top Bottom