Kituo cha Polisi Ukonga Stakishari chavamiwa na Majambazi

Ni salamu kwetu sote tuliopo ndani ya Nchi hii, kwamba silaha hizo 20 zinaweza kutumika mahali popote na wakati wowote! Tujiadhari na tutoe ushirikiano kwa vyombo vya Usalama! Ili tuwe salama Mkuu! Pengine wamepanga wazitumie octoba kiongozi, au nyumba za ibada au siku ya iddi au bup/bar n.k. Kwa kifupi hatupo salama!
 
Polisi waachekufanya kazi kwa mazoea wawe na tension popote walipo hali imekuwa mbaya sasahivi sio kama zamani, kwanini hawajifunzi kwa yanayotokea??.

Inauma sana kuona majambazi wanauwa walinda usalama kirahisi rahisi tu, tena hapohapo kituoni, hii ni aibu kwa jeshi la polisi. Kwanini matukio yanajirudiarudia?

Raia wema tuungane pamoja jamani na tufichue uovu huu kwa kadiri tutakavyoweza. Pole kwa familia za wote waliopoteza wapendwa wao, Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu. R.I.P marehemu wote.
 
hawa ndio wahalifu polis waliotakiwa pambana nao badala ya kukomaa na intelejensia za ukawa
 
Wapigwe tu......juzi Zanzibar nao wamewapiga risasi wananchi kwa sababu ya uandikishaji
 
Inawezekana hii botton ikawa imebonywezwa na mmoja wa watu ambao wamejeruhiwa na "kukatwa"? Simaanishi kuleta uchonganishi... najaribu kufikiria tu moja ya possibilities
 
RIP walinzi wa mali zetu na usalama wetu, nendeni kwa aman ingawa hapo Stakishari kuna askari wadau wangu ngoja niwacheki daaaaah.
 
Pamoja na tabia mbaya inayofanywa na askari police wengi, kupindisha haki kwa kitu pesa, lakini linapokuja swala la askari kuuawa linastikitisha na kufedhehesha. Jeshi la police nadhani sasa linapaswa kufanyiwa mageuzi upya, mzee Pombe, kama ukichukua madaraka, anza na kureform hili jeshi letu...
 
Du! kuna haja ya kuzungushia uzio kwenye vituo vya polisi, ili kama ni usiku geti linafungwa mtu akitaka huduma agonge geti au abonyeze kengele, then mmoja akija kufungua wengine wanakuwa standby mpaka huyo mtu/watu watakapoondoka na geti kufungwa, poleni familia, poleni jeshi la polisi.

Du hii Kali mkuu, kituo cha polisi kina uzio na geti! Hii haijapata kutokea!
 
Back
Top Bottom