Kituo cha Polisi Ukonga Stakishari chavamiwa na Majambazi

Du! kuna haja ya kuzungushia uzio kwenye vituo vya polisi, ili kama ni usiku geti linafungwa mtu akitaka huduma agonge geti au abonyeze kengele, then mmoja akija kufungua wengine wanakuwa standby mpaka huyo mtu/watu watakapoondoka na geti kufungwa, poleni familia, poleni jeshi la polisi.
 
Poleni sana polisi wetu na mpumzike kwa amani!Tatizo polisi wamewalea sana majambazi mfumo mzima wa ujambazi polisi wanaujua matokeo ndio hayo sasa ,hakuna hata siku moja urafiki wa Paka na panya !
 
Mimi nadhani hili ni tatizo zaidi ya ujambazi, jambazi hutafuta hela ni si kutafuta silaha watanzania tukiendelea kujadili mambo kirahisi namna hii tujue tunazidi kuchelewa kulikabili tatizo.

Ni kweli nakubaliana na wewe, intelijensia ya polisi inatakiwa ifanye kazi extra mile kubaini kwanini matukio ya askari kuporwa silaha yanaongezeka! Lakini pia suala la ku-recruit na mafunzo ya askari linahusika sana, huyu chagonja mkuu wa operesheni na mafunzo anapwaya sana!
 
Kufukuzwa hovyo askari, nahisi kutakuwa kunachangia kwa kiasi kikubwa na mbaya zaidi fukuza ya uonevu.

Polisi hasa wakubwa wamekuwa miungu watu na wanachosema na kuamua ndio cha mwisho ilhali miongoni mwa maafisa sio waaminifu kama baadhi ya askari wadogo.

Sipati picha kwa mtu ambaye ni mgeni kituo cha Stakishari aingie na kuua kisha kupora kama hakuna taarifa kutoka miongoni mwa askari wenyewe au waliofukuzwa. Mungu atunusuru
 
Kwa mbaali naona kama ni ulipizaji wa kisasi maana hapo panasifika kwa kutesa RAIA wakubali makosa si yao, na hata kuwatoa roho RAIA wema. Poleni, angalieni nyendo zenu.
 
Sio jambo la kubeza na kusema ni uzembe au kufurahi kuwa ni sawa kwa walinda Usalama kuvamiwa. RIP askari wote!
 
Uvamizi ,uporaji na mauaji ya kutisha katika kituo maarufu cha Sitakishari ukonga si habari njema hata kidogo

Kutokuwa na woga na uthubutu wa kuvamia kituo hiki kinachosifika kwa kila aina ya utesaji kwa wahalifu sugu Dar es salaam ni dhahiri kuna dhamira madhubuti isiyo na woga

Mauaji ya askari takribani sita na uporaji wa silaha zipatazo 20 au zaidi ni majonzi na pia ni tishio kwa wapenda amani wote

Kutokea kwa tukio hili baya wakati serikali na chama tawala wapo Dodoma wakihubiri Amani na utulivu ni salamu za kejeli kwao!

Nini kipo nyuma ya tukio hili?
Udini?
Ugaidi?
Visasi?
Uokoaji?
 
Back
Top Bottom