Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

1. Pope kafanyaje?
2. Huyu mdada ni tricks za magic Kama nyingine tu...jifunze code zao utaelewa video zipo kibao YouTube Kuna Hadi vipindi vya breaking the magician code...vinaelezea mazingaombwe Yanavyofanywa hata we ukijifunza unafanya ni akili tu
3. Halloween ni tradition, ni kama Christmas..kule wenzetu Christmas wanaita happy holidays na ni sikukuu coz of tradition.. Halloween kwao si kwamba wanalogana na kufanya uchawi...no wanahave fun kuvaa nguo za kichawi na kutembeleana ni sikukuu tu haina uchawi.
Bado hujaprove kwamba jamii za wazungu zinaamini uchawi.
Unaposema Halloween ni tradition wanavaa nguo za kichawi nk

Alafu unasema hawaamini uchawi??? Una uhakika ww una akili??
 
Utakapotoka kwenye utegemezi na kuingia mtaani kutafuta maisha mwenyewe ndipo utakutana na mambo mengi ambayo yatatanua upeo wako ila kama utaendelea kukaa hapo kwa mjomba hali itaendelea kuwa hiyo hiyo.
Mi skia kwa mjomba...nimepanga naishi Mimi na mke wangu...🤣au mpaka nije mtaani kwako..okay ukiachana na Hilo. Je Kuna watu ambao hawakai kwa mjomba wao Ila bado hawaamini uchawi? Yes wapo...😁so wao unawapa ushauri gani waone mambo ya kichizi unayoona we na wenzako
 
Unaposema Halloween ni tradition wanavaa nguo za kichawi nk

Alafu unasema hawaamini uchawi??? Una uhakika ww una akili??
🤣🤣🤣Mi nikivaa Kama superman inamaanisha ninaamini Kuna superman? Mbona unakuwa Kama mtoto wa la tano wewe. Angalia bac hizo Halloween uone
Ni sherehe tu Kama zingine...
 
Kwa sababu sisi ni watu logical ndo hatuoni hivi vitu...ni uwongo na story za mababu ambao hawakujua hata mvua inasababishwaje wanajua miungu inashusha. Ndo jamii tuliyotoka, kitu Kama jua, mbwa, paka, miti hatubishani kama ipo au haipo..why we uone peke yako kitu ..huo ndo uchizi. Kuona maruwe ruwe ni tatizo la kiakili

Si ni kama vile wewe unavyomuona mke wako mzuri wakati wengine Wala hatuuoni huo uzuri wake. Maana yake nini...ni kwamba mapenz yamekufanya umekuwa kipofu huoni. Sasa kama kitu kidogo hivi kimekushinda kuona ndo utaona paranormal activities!??

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Huyu nae ni mpuuzi mmoja tu...anatetea ujinga eti Mungu wa walokole..mbona wamejazana watu wenye njaa na ambao hawana kazi huko
 
Story hizi nizakweli kabisa na ninaamini uchawi upo, na hakuna mtu wa kuniaminiaha uchawi haupo uchawi upo.

Kisa 1. Mwaka 2013 nipo Secondary shule moja inaitwa Shinyanga secondary (Shybush) nilikuwa natoka nje ya bweni kukojoa ile naangalia chini nikaona panya wawili wananizuia kupita nikienda huku wananifata nikienda kule wananifata ilikuwa ni getini sasa nikaona hapa sito ingia nikawaruka nikaingia ndani ya bweni kuja kujikuta nimejigonga ukutani bega likashtuka.

Kisa 2. Mwaka huo huo 2013 tukafunga nikaenda mwadui kwa baba yangu mdogo, ile natoka nakatiza uwanja wa Mwadui katikati kipindi hicho kulikuwa hamna fence akatokea mwewe kama mlisikia mwewe kabeba Ng'ombe Sumbawanga basi ndio ilitaka kunikuta yule mwewe alifika na kunipiga kichwani ni kama nataka kubebwa hivi. Niliona nikama nimetuliwa na tofali kichwani kumbe mwewe.
Nilikuja kujishika kichwani kumbe nimekwaluliwa huyo mwewe alinifata mpaka nilipo kuwa naenda, nikafika namuona tu yupo juu anazungukia maeneo yale basi nikaingia nikakaa kama saa hv ndani ile natoka nikamkuta anazungukia tu maeneo yale nikatoka hapo nikaenda sehemu ambayo huwa nalala aisee bdo alinifata tu mpaka hapo nikaingia ndani nayeye nikamuacha anazunguka juu nikalala zangu mpaka usiku ndio nikatoka.

Kisa 3. Niliajiriwa kijiji x nikawa nimeenda kama Muuguzi, Akatokea mjamzito nikamzalishe sasa akawa anashida fulan za uzazi nikatoka nje nikamuite mwenzangu ili tupeane ushauri jinsi ya kumsaidia ile navuka barabarani namuonga mtu kavaa kaniki nyekundu na nyeusi nikajikaza nikasema sasa huyu namsalimia badi nikawa nimemsalimia masna alikuwa bize anainama mara anainuka nikawa nageuka geuka nyuma yupo pale pale nilivyo enda na kurudi hayupo.

Visa nilivyo pambana navyo ni vingi ila niishie hapo, na sio Hallucinations.
Cha kwanza panya...sioni uchawi Cha pili mwewe sioni uchawi...Cha tatu... hallucinations...😁Next
 
Ngoja nikupe story ndugu nina kishamba changu maeneo ya machimbo kwa mzee limboa chanika mbele ya kwa mstaafu simon siro.

Kuna huyo mama anaendekeza sana haya mambo na mtoto wake,
Ile sehemu wengi ni wastaafu wamenunua mashamba tena wanajeshi na maaskari na yeye ndo alikuwa mtu wa mwanzoni maeneo hayo.

sasahivi kuna majumba makubwa ni yeye pekee amebaki na nyumba ya udongo. Mpaka chumvi anaomba

Funny enough akaanza kuwadanganya watu kwamba ndani kwake kuna madini ety majini yamemuonyesha ikabidi awaite vijana wa machimbo.

Ndugu yangu simbampole walichimba shimo refu ndani siyo nje na hakuna kilichopatikana.

Hawa watu wengi huwa Wana matatizo ya akili. Ila kadri siku zinavyoenda wataelimika
🤣🤣Afu utaskia baadae watu wanasema yule bibi sijui kafanyaje sijui nyumba haibomoki sijui aaah bro nishawazoea
 
Kwanza Mimi sijasema Mazingaombwe ni Uchawi... Ila ni wewe unayefikiri Uchawi ni sawa hayo Mazingaombwe.
Ninachokuambia hiyo Talent kwa asiyeijua ndio anaita Uchawi. Kama wewe na wenzako msivyojua talent ya matibabu pasi na kushika mgonjwa, Mtaita Uchawi.

Ni wewe ndio uliyeniambia nitazame Behind The Scenes, kama sio unafikiria Mazingaombwe ni Movie za Mazombi, sema basi behind the scene zake uliziona wapi?
🤣We huna elimu...behind the scenes sio lazma iwe movie .hata live shows Kama Mieleka, dances, etc performance za wasanii Zina behind the scenes. Acha kuwa ignorant sawa. Behind the scenes namaanisha maelezo ya hiyo performance au practice zake hivyo
 
W
Wewe hujui Uchawi ni nini na yaweza kuwa unauishi.

Nilikuuliza je Umeshawahi kwenda kwa mganga wa kienyeji, ukajibu ufuate nini!
Sasa labda nikujuze, WAGANGA WA KIENYEJI(TIBA ASILIA) NI MIONGONI MWA WATU WAFAHAMIKAO KUWA WACHAWI.

Ukifikiri Tiba Asilia ni wa Kina Ndodi tu, umepotea. Tiba Asilia ina ramli, INA masharti ya njia panda, ina tunguli, ina makaburi, ina manuizi, nyota, nyungu, nk....

Ushamba ni mzigo!
🤣🤣🤣🤣Okay tiba asilia hata mi naweza kula mmea nikapona. Tuje kwenye tunguli, nyota, nyungu, makaburi...una evidence ya ulisemalo au unaongea kwa hisia...
 
Uchawi si kuloga tu kupata hela, Uchawi ni kufunga mwizi asiibe, Uchawi ni kufunga mke asichepuke, Uchawi ni kuchanja mifugo iongezeke, Uchawi ni kujua usalama wa safari yako, Uchawi ni kujua wabaya wako, Uchawi ni kutibu magonjwa yako, Uchawi ni kinga, Uchawi ni silaha, Uchawi ni kila kitu...

Sasa nitafute Tujaribu hilo la Wizi, nikuelekeze mahali ambako utatumia sayansi yako ya kukaririshwa ukaibe, kama utatoka salama.

Umesema una watoto, lakini ajabu unawaza kama watoto wako.
Hujui Sayansi ni Nini ..Sayansi haiishi darasa la Saba ulipoishia wewe...Sayansi ipo katika maisha .ukitembea ni Sayansi Kuna skeletal movement, kuna friction, Kuna energy ndo science sawa...elewa bac
 
Hujakutana na maswaibu wewe! Unaweza kwenda na dalili zote za kisukari hospital hao madaktari wako waliosoma miaka 7 wengine 10 kila wakipima hawaoni ugonjwa..pima pima hawaoni ugonjwa ila una dalili zote za mgonjwa wa kisukari..mwisho wa siku hao hao madaktari wanawaambia go back to the roots..

Hapo sasa ndipo yanapoingia mambo ya Kiroho ambayo ni beyond human scope ni wachache wenye kuyafahamu.Sasa hapo ni wewe kwenda kuombewa au kwenda kutibiwa kienyeji.

Wanakuambia Ukiujua ulimwengu wa Kiroho unavofanya kazi Utamiliki na kutawala..maana mambo yote unayoyaona mwilini chanzo chake ni Ulimwengu wa roho.

Nyongeza: Maisha yetu wanadamu tunayoishi na mambo tunayofanya yameanzia rohoni yawe ya mafanikio, umasikini,kukuharibia maisha e.t.c..hata magonjwa unayoona mfano mtu kisukari, kansa, ukimwi, e.t.c akienda kuombewa au kwa waganga unasikia watu wamepona chanzo cha hayo yote utatuzi/solution yake ni Rohoni.
Mganga au mchawi wana access na mambo ya rohoni.Ndo maana wao wakiamua kuua mtu au kukamata wezi huji kusikia anakuja physcially anatega kwa sayansi yake na unajaa.

Take care, Usibishe usivovijua
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣Bas kamwambie mganga wako aniue ..toka hapa na story zako....we na umaskini wako unaenda zahanati yenu ya mtaa hamna hata kipima joto unasema huoni ugonjwa...🤣Hizi story ziishie kwa mwamposa sio hapa
 
Hakuna unalojua wewe!Bure kabisa...! Nashangaa hata watu wanaokujibu! Unaweza ukawa una type upo sebleni kwa shemeji hapo unaangalia katuni..!
🤣🤣🤣🤣Niambie bac nikitoka kwa shemeji yangu nitaona uchawi au utanipa kisingizio kingine Cha kwa Nini we ni chizi na unaona hallucinations
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom