mdundo ngoma sana
JF-Expert Member
- Jan 2, 2016
- 1,002
- 955
Watu wa tanzania ni mali ya serikali either iwatumie au isiwatumie upo!Nimesoma tangazo la kurugenzi ya mawasiliano ikulu kuhusu konachoitwa kutolewa kwa madaktari 500 kwa serikali ya Kenya kwa ajili ya kutoa huduma nchini Kenya.
Katika tangazo hilo, Waziri wa Afya amenukuliwa akisema kuwa wapo madaktari wengi waliohitimu ambao hawajaajiriwa na pia wapo walio nje ya mikataba na waliostaafu lakini bado wana uwezo na hivyo watakwenda Kenya kutoa huduma.
Kwa mantiki hiyo, hao madaktari wote ni free agents kwa kuwa hawana mkataba wa ajira na taasisi yoyote wala serikali . Kwa maana hiyo wanaweza kuajiriwa popote duniani bila kipingamiz chochote.
Kwa mantiki hiyo, kisheria huwez kusema kuwa serikali imetoa madaktari kwenda Kenya wakati haijawaajiri. Yaani serikali haiwez kutoa kitu isichokimiliki.
Nawasilisha.