Kisa cha Desmond Doss na dhana ya uwezo wa nguvu za Mungu

Slowly

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
10,549
35,107
_si.jpeg

Duniani kuna Imani nyingi za kidini , karbia kila mwanadamu anaamin uwepo wa nguvu zisizo za kawaida katika maisha ya binadamu... uwepo wa Mungu ni dhana inayoaminika na wanadamu karbia wote duniani , hata hvyo Mungu huyu anaabudiwa Kwa mfumo na Imani tofaut tofaut ... Kuna wanaomuabudu kupitia maandiko matakatifu ya Biblia (hapa kuna madhehebu mamia Kwa mamia) kuna wanaomuabudu kupitia Qur'an ( hapa Napo kuna makundi yake) na wengine kupitia viumbe hai na visivyo hai e.g ng'ombe , jua n.k .....

Basi kila mmoja anamfikia Mwenyezi Mungu Kwa namna anavyoamin, ...ukiachilia mbali visa vya kwenye maandiko matakatifu e.g bahari ya shamu kugawanyika katikati, vijana kutoungua kwenye tanuru la Moto , Eliya kushusha Moto kutoka mbinguni huku watu wote wakiona n.k ...Kwa sasa ni nadra Sana kukutana na shuhuda zenye ushawishi....kwani shuhuda nyingi za watu hvi Leo zina sintofahamu na zingine ni usanii mtupu ....japo watu wengi tunaamin uwepo wa Mwenyezi Mungu hata hivyo ni wachache Kias gan wanaomtumaini kiukweli ukweli , hata Kwa wale wanaojidai kuliitia jina la Mungu mfano viongozi wa kidini bado kuna usanii mtupu wanafanya...
Kisa cha Desmond Doss kinashangaza kidog na kinaibua mjadala mkali Ulimwenguni kote kuhusu uingiliaji Kati wa Mungu kuwalinda wale wanaomtumaini ,


Desmond Doss alizaliwa mwaka 1919 huko Virginia Marekani , alitokea familia ya kikristo ya dhehebu la wasabato ...Baba yake alikuwa veterani wa WW1, mama yake ndo alishika dini Sana , Baba yake alikuwa mlevi sababu ya scar na memory za WW1, Desmond alikuwa mtiifu Kwa amri kumi za Mungu , wakat vita ya pili ilipotokea ulikuwa ni mtihani mzito Kwa Desmond Doss kuitimiza amri inayosema "USIUE"... Kuanzia mwishoni mwishoni mwa mwaka 1941, Marekani ilikuwa kwenye vita na Japani( Imperial Japanese force ) katika bahari ya Pacific , vijana wengi walijitokeza kuungana na jeshi, wakiwemo watu maarufu kama John F. Kennedy yeye alikuwa upande wa Navy ( wanamaji) na George Bush upande wa Aviation ( fighter pilot) .....


Doss alikuwa anafanya kazi naval ship yard Kwa kipind hcho , yeye alijiunga na jeshi la ardhini (Us marine ) Baba yake alimuonya kujiunga na jeshi kwani vita ni disaster, hata hivyo kijana alinuia kujiunga na jeshi.....

Mzee ikabidi awe mpole , kijana akaenda, huko kambini mambo hayakuwa rahsi Kwa Doss , kijana alisimamia msimamo mkali wa kidini , yeye alihitaj awe Daktari wa jeshi na hvyo kwake yeye hata kushika silaha ni dhambi ....na pia alitaka kila jumamosi apewe ruhusa akasali ...
Alijikuta katika wakat mgumu sana kupingana na kawaida za kijeshi, kwani hata kama ni daktari , silaha ni muhimu Kwa ajili ya kujilinda , mazoezi ya kawaida ni lazima Kwa kila askari, wengi waliamini kijana hayuko Sawa kiakili , wengine walimtenga kambini na kumuona kama taahira , wengine walimtesa na mmoja ilifikia hatua akamwambia wewe huna msaada wwte , na tukifika vitani ntahakikisha haurudi tena , wewe ni useless ( huna msaada) ..... Alifikishwa mpak mahakama za kijeshi Kwa sababu ya msimamo wake wa kutoshika silaha na mara zote yeye jibu lake lilikuwa ni moja tuu , 'Mungu kasema nisiue, na hvyo kazi yangu ni kuokoa"


Kiongozi wake Jack Glover alitaman kumpiga chini, hata hvyo alijua asingekubaliwa kirahsi na viongozi wa juu wa jeshi, Kwan Zaid ya watu 20000 Aina ya Doss walikuwepo kwenye jeshi lote la Marekani japo hawakuwa na msimamo makali kama Doss na serikali iliwatambua Kwa kufanya Non combat issue ( masuala yasiyo ya mapigano ) kama vile kuwa madaktari , viongozi wa kidini jeshini , wasaidizaji n.k ....mwisho Kwa sababu ya uhaba wa madaktari jeshini ( Wajapani waliwaandama Sana Askari wenye nembo za medics or Dr) Doss aliungana na wenzake kwenda vitani , japo kiujumla hakupewa ushirikiano kabisa ...


Mnamo 1944 Vita ilikuwa imehamia visiwa vya solomon ( Solom islands ) southern Pacific , Doss alikuwa sehemu ya 307th Infantry Regiment, 77th Infantry Division ( hizi ni term za kijeshi kuzielezea kiswazi ni ngumu kidogo) kikosi chake kilikuwa sehemu ya pambano la kisiwa cha Guam ( July 21-August 10 1944) na pambano la Leyte (17 Oct - 26 Dec 1944) ni katika mapambano haya kikosi kizima walitambua umhimu wa daktari huyu mshika dini ,na hapa ndipo wote walianza kumheshimu , kwani Doss ndo daktari pekee kwenye kikosi aliyekuwa anadhubutu kuwatibu Askari waliojeruhiwa umbali wa Mita 20 Tu kutoka eneo linalokaliwa na maadui ( Behind the enemy line) ...

Wakati mwingine alipokuwa anamtibu Askari aliyejeruhiwa na kuachwa na wenzake alisikia askari wa kijapan wakiongea , hvyo alifanya kazi Kwa kujitoa mhanga Sana under extreme danger na bado alifanikiwa kuwavuta majeruhi mpak sehemu salama zaidi...


Kufikia mwaka 1945 vita upande wa ulaya ni kama ilikuwa imeisha , Ujeruman ilikuwa ime- surrender , upande wa bahari ya Pacific mambo yalikuwa bado , japo Japan ilikuwa inazd kuelemewa , na sasa Kwa mara ya Kwanza tangu miaka 5000 Japan ilikuwa inashambuliwa kwenye ardhi Yao wenyewe ,.....


Pambano kubwa zaidi la mwisho katika vita ya pili ya Dunia lilikuwa linatokea kwenye kisiwa cha Okinawa kama maili 250 Tu kufikia Tokyo Japan...hii kitu iliwaumiza Sana wajapan na hivyo walipambana mpak tone la mwisho ( defending fiercely to the last man ) kuanzia April -june mwaka 1945 mapigano makali yalikuwa yakiendelea Okinawa , .....
Faith-Of-Doss_Article_The-Ten-Commandments_1-1038x576.jpg

Desmond Doss akiwa kwenye kisiwa cha Okinawa April 1945

Vita ya Okinawa,ilijulikana kama Operation Iceberg ikihusisha askari 306,000 wa Us na washirika wake dhidi ya Askari 130,000 wa Japan na idadi kubwa ya wananchi wa Okinawa .

US-Navy-shelling-Okinawa-1945-World-War-II.jpg


origin.jpg


U.S. Navy LSM(R) (Landing Ship Medium, Rocket) shelling Japanese positions on Okinawa, 1945.

origin (1).jpg

Ndege za kijeshi za Marekani zikirusha makombora kwenye kisiwa cha Okinawa 1945

Doss na kikosi chake walikuwa assigned kulitiisha ( To seize ) eneo lililojukana kama Maeda escapement au Hack saw ridge ..eneo lilikuwa na jabali (Cliffs) na mwinuko wa takriban wa futi 400, mziki ulikuwa kupanda kule juu ambako ndiko Askari wa Kijapan walikuwa wametulia , wakijitengenezea mapango na kujificha wakiwasubir waje....

Kimsingi kila aliyejarbu kupanda kule juu aliuliwa , mpak walipoamua kutumia cargo net pembeni kidogo, baada ya mapigano ya hapa na pale zaidi ya Askari 200 walifika eneo la juu na kuanza kusonga mbele.. hata hivyo wajapan walikuwa wamewasubiria wakiwa wamejificha kwenye mapango na mashimo.....

Kwa ghafla walianza kushambuliwa tokea pande tatu ,( in a vicious counterattack) kibaya zaidi waliokuwa wanawashambulia walikuwa hawaonekani,
Walichokuwa wakikiona ni milipuko ( Motar and artillery blast) , risasi za machine gun na bunduki za kawaida (rifle) pamoja na walengaji (snipers) sambamba na maiti za wenzao na kila Kona kulikuwa na kilio cha kuomba msaada Medic!! Medic !! Medic ... Mapigano yalikuwa makali Sana kiasi cha kumlazimu kamanda wao Jack Glover kutangaza kurudi nyuma na kukimbia ( the team were forced to withdraw/ Retreat) ... hata hivyo ni Askari 75 Tu waliofanikiwa kukimbia na kurudi kambini Kwa nguvu zao wenyewe ...hata kamanda wao alikuwa amejeruhiwa vibaya na hivyo hakuweza kukimbia kurudi .....
US-Marines-control-ridge-Naha-Okinawa-May-1945.jpg

Heavy fire fight Okinawa 1945

Marines-Battle-of-Okinawa-1945-World-War-II.jpg

Members of the U.S. 1st Marine Division advancing behind a flame-throwing tank during the Battle of Okinawa, May 11, 1945.

Marines-Japanese-bunker-Battle-of-Okinawa-1945-World-War-II.jpg

U.S. Marines clearing a Japanese bunker during the Battle of Okinawa, May 1945

Desmond doss pekee ndiye aliyebaki eneo la tukio ( battle Field) na hapo ndo alipotumia masaa 12 kuwavusha na kuwashusha Zaid ya Askari 75 akiwemo na kamanda wake Jack Glover....
Swali linakuja aliwezaje kufanya hvi peke yake kwenye eneo linalokaliwa na maadui? (Active enemy area) bila kufyatua risasi na bila kubeba silaha.... Alipoulizwa alisema

mortars.jpg
2b2a17e2ddfc344c727b57c196661865.jpg
0c836bc7282169173c9494d7492b7962.jpg
417d04fae01015640843d1dc6861374a.jpg

Japanese Force in Okinawa WW2, note : picha mbili za mwisho ni drawing art , zingine zote ni picha halisi (photography)1945

"kila mara nilikuwa naomba na kusali , nilipofanikiwa kumtelemsha mmoja niliomba na kusema Bwana nisaidie niweze kumsaidia mwingine". ,

alipoulizwa je hukupata mashambulizi yyte , Alisema kila mara nilipokuwa nikimbeba majeruhi nilikuwa nikishambuliwa , ..... "Nilikuwa naona risasi zikipaa , hata hvyo hazikunipata "

dosshacksaw_custom-70d43a750baea2157d13b3d47c9437930cfd2b31-s800-c85.jpg


Maeda escapement or Hacksaws ridge eneo ambalo Desmond Doss aliwasaidia Askari zaidi ya 75 kimiujiza , hii ni picha halisi na aliyeko juu ni Desmond Doss mwenyewe..Askari walipanda juu Kwa kutumia wavu wa kamba (cargo net) kama inavyoonekana

Kamanda Jack Glover miaka ya badae baada ya vita alipoulizwa alisema , kama Mungu yupo basi nimemuona katika maisha ya Desmond Doss....

Doss aliushinda ubaya Kwa wema , wengi wa wale aliowakoa sku Ile ndo waliokuwa wakimchukia Zaid kambini kabla ya kuingia vitani , kambi ilimheshimu Sana Doss , ilifikia hatua wakawa wanasubiri Kwanza Doss asali ndo waende kwenye uwanja wa mapambano, Askari wengi walimuona kama mwokozi wao , Mwishon mwa mwez mei 1945 , Doss alijeruhiwa Kwa bomu la mkono (grenade) na hivyo aliondolewa kwenye uwanja wa mapambano , wakat akitolewa aliona askar mwingine amejeruhiwa Zaid yake aliruka toka kwenye machela na kwenda kumtibu Yule majeruhi .... Katika harakat hzo Doss alipigwa risasi ya Bega na sniper , Doss alijivuta takriban Mita 300 mpak sehemu salama....

Kwa kwenda mbali zaid Doss aliwatibu mpak Askari wa Kijapan
Kwa kipind hcho japan ilikuwa ikikabiliwa na upungufu mkubwa wa madawa , na hvyo Askari wake Weng walikufa Kwa kukosa tiba , magonjwa ya mlipuko kama chorela na hata Malaria ...na hvyo Doss aliwatibu pale alipokutana na Askari adui akihitaji huduma hyo.....
Aliondolewa Okinawa na kupelekwa kisiwa cha Guam kwenye hospital ya kijeshi na kisha kuridishwa Marekani , .... .
22-46-24-images.jpg

Desmond Doss baada ya kujeruhiwa

Zaidi ya Askari Million 16 wa kimarekani walipigana vita ya pili ya Dunia Kati Yao ni Askari takriban 400 Tu ndo walitunukiwa medali ya heshima ya kijeshi , Kati Yao alikuwemo Desmond Doss , na yeye Peke yake ndo alipata medali hyo bila kubeba silaha .... Ilishangaza Sana , Doss alioa na kubahatika kupata mtoto mmoja , mke wake alifariki mwaka 1991 Kwa ajali ya gari, yeye alifariki mwaka 2006 akiwa na miaka 87.....
Na siku zote za uhai wake alishuhudia ya Kuwa ni Kwa uwezo wa Mungu yeye alifanya hvyo na hamna kingine...

images (23).jpeg

Desmond doss akiwa na Raisi wa 33 wa Marekani Harry S. Truman kabla ya kutunukiwa medali ya juu ya heshima ,white House mwishoni mwa mwaka 1945

Vita ya Okinawa ndo ilikuwa the largest and last world WW2 battle....zaidi ya Askari 17000 wa Marekani waliuawa na Zaid ya Askari 33000 walijeruhiwa , Japan ilipoteza Askari wapatao 100000 , na wananchi wa wa Kisiwa cha Okinawa wapatao 150000....
Vita ya Okinawa ilionyesha Japan haipo tayar kujisalimisha (Surrender) na ni moja ya sababu ya Us kutumia Atomic bomb to end WW2..

5f2d3c6c1b7b866c05d34ccf2b04c75c.jpg
53b8dc1e8a15948fe6f2beebb778cf5f.jpg

Meli ya kivita ya marekani (USS bunker hill aircraft carrier), ikiwaka Moto baada ya kushambuliwa na ndege za kivita za Japan (Kamikaze suicide bomber) katika kisiwa cha okinawa



okinawa-naha.jpg

Mji wa Okinawa unavyoonekana miaka ya hv karbuni

Kisa chake kinajulikana vyema kwenye mtandao wa internet na kimesimuliwa pia kwenye movie ya kivita iitwayo Hack saw Ridge , iliyotoka mwaka 2016 na iliogozwa na mwongozaji nguli wa movie ya Apocalipto Aitwaye Mel Gibson.....

Hacksaw_Ridge_poster.png

By Slowly mtu mbaya
 
Kumtegemea Mwokozi,
Kwangu tamu kabisa,
Kukubali neno lake,
Nina raha moyoni.

Yesu,Yesu namwamini,
Nimemwona thabiti;
Yesu,Yesu,yu thamani,
Ahadi zake kweli.
 
Kumtegemea Mwokozi,
Kwangu tamu kabisa,
Kukubali neno lake,
Nina raha moyoni.

Yesu,Yesu namwamini,
Nimemwona thabiti;
Yesu,Yesu,yu thamani,
Ahadi zake kweli.
Mkuu hujaenda kanisan ha haaa
 
Back
Top Bottom