Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 21,975
- 23,475
Utazingatia chama cha siasa na itikadi yake tu,
Utazingatia ilani, sera, mipango, dira, mbinu, uelekeo na mikakati ya chama husika, katika kutatua changamoto mbalimbali na kuleta maendeleo kwa wananchi?
Utazingatia Elimu, umakini, uadilifu, umahiri, maelezo na ushawishi wa mgombea kwenye kujenga, kueleza na kutetea hoja na mahitaji ya wananchi?
Utazingatia record ya utendaji wa mgombea kama aliwahi kua kiongozi huko nyuma, na record ya chama chake katika kuwathamini wanachama na wananchi?
au,
utazingatia sura ya mgombea, rangi za chama chake, jinsi anavyolalamika na kulaumu wengine kwa ukali na kufokafoka, bila kueleza hata kidogo mbadala wa suluhisho la malalamiko na lawama anazozitoa?
utazingatia nini ndugu mwanainchi, ili tuweze kufanya maamuzi sahihi na kuchagua viongozi sahihi wa kuskiza na kusaidia kuishauri serikali kuongeza juhudi kwenye kutatua kero kwenye vipaumbele vya wananchi na katika kutatua changamoto nyingine mbalimbali katika maeneo husika ya wananchi...🐒
Mungu Ibariki Tanzania