Kinondoni; Matumizi 4 Ya Vibali Vya Ujenzi Kwenye Uwekezaji Ardhi Na Majengo

Aliko Musa

Senior Member
Aug 25, 2018
157
242
Kibali cha ujenzi ni nakala itolewayo na serikali kwa ajili ya kuruhusu ujenzi au ukarabati/maboresho ya majengo. Nakala hii ni njia mojawapo ya serikali kuchochea aina fulani ya makazi ya ubora fulani.

Kibali cha ujenzi ni kiashiria cha kiuchumi kwenye maendeleo ya afya ya sekta ya ujenzi na ukuaji wa miradi ijayo. Kupitia vibali tunaweza kupata taarifa zifuatazo;-

✓ Idadi ya vibali ujenzi vya katika wilaya husika. Wilaya ya Kinondoni.

✓ Kufahamu aina ya ujenzi unaofanyika siku chache mbeleni (ujenzi wa majengo ya makazi, majengo yasiyo ya makazi, kuongezea sehemu ya jengo au kubadilisha sehemu ya jengo.

✓ Kufahamu makisio ya thamani ya miradi inayotekelezwa au miradi inayoanza kutekelezwa hivi karibuni.

Hali ya Utolewaji Wa Vibali Vya Ujenzi (Building Permits) Kinondoni.

Wilaya ya kinondoni ni moja ya wilaya chache sana ambazo zinatoa ripoti nzuri sana na kwa wakati husika kuhusu vibali vya ujenzi. Kila mwezi hutoa hali ya maombi ya vibali vya ujenzi katika wilaya hii. Hii ndiyo sababu imenifanya nigusie eneo la vibali vya ujenzi (building permit) kwa upana zaidi.

Maeneo 4 Ambayo Vibali Vya Ujenzi (Building Permits) Vinaweza Kutumika.

Moja.

Huduma za ujenzi (Demand for construction services).

Ongezeko la maombi ya vibali vya ujenzi hutoa ishara ya ongezeko la mahitaji ya huduma za ujenzi katika halmshauri ya wilaya husika. Kupungua kwa maombi ya kupewa vibali vya ujenzi, huashiria kupungua kwa mahitaji ya huduma za ujenzi.

Pili.

Mienendo ya masoko ya makazi (housing market trends).

Ongezeko la maombi ya vibali vya ujenzi wa majengo ya matumizi ya makazi huashiria hali nzuri ya masoko ya majengo ya makazi.

Hali hii huambatana na ongezeko la mahitaji ya majengo ya matumizi ya makazi na ongezeko la bei za majengo yaliyopo katika wilaya husika.

Kupungua kwa maombi ya vibali vya ujenzi wa majengo ya makazi huashiria hali mbaya ya masoko ya majengo ya makazi. Hii huambatana na kupungua kwa mahitaji ya majengo ya majengo ya makazi.

Tatu.

Ukuaji wa ajira na uchumi.

Kuongezeka kwa idadi ya maombi ya vibali vya ujenzi na utolewaji wa vibali vya ujenzi huonyesha ongezeko la ajira na kuimarika kwa hali ya uchumi katika wilaya husika.

Kuwepo kwa maombi machache ya vibali ujenzi huashiria kupungua kwa ajira kwa vijana na hatimaye kushuka kwa hali ya uchumi katika wilaya husika.

Nne.

Fursa za kiuwekezaji (investment opportunities).

Kuongezeka kwa idadi ya maombi ya vibali vya ujenzi na ongezeko la utolewaji wa vibali hutoa taarifa muhimu kuhusu afya ya sekta ya ujenzi na fursa za kiuwekezaji zinahusiana na;-

✓ Uwekezaji kwenye ardhi na majengo (real estate).

✓ Vifaa na malighafi ya ujenz.

✓ Huduma za kifedha kwa kuangalia ongezeko la riba na kupungua kwa riba za taasisi za kifedha.

Rafiki yako,

Aliko Musa.

Mbobezi majengo.

Whatsapp; +255 752 413 711
 
Ni utaratibu gani unatakiwa kufuatwa na Manispaa pale ambapo mhusika amegundulika kuwa ameanza ujenzi wa nyumba ya makazi ya kawaida isiyo ghorofa kwenye kiwanja chake halali kisicho na mgogoro wowote lakini bila ya kuwa na kibali cha ujenzi kuoka manispaa.

Jee, ni sawa kama mtu ameanza ujenzi bila kibali na baadaye kwa hiyari yake kuamua kwenda manispaa na kuwasilisha maombi ya kibali cha ujenzi na hadi kulipia ada ya kibali, kulazimishwa kulipa fine ya 2% ya thamani ya jengo lake?

Au kuna sababu nyingine za msingi pamoja na hatua ambazo zinatakiwa kufuatwa awali kabisa na manispaa kama kupewa notisi ya kusimamisha ujenzi na muda wa kuanza utaratibu wa maombi ya kibali cha ujenzi kabla ya uamuzi wa kutoza fine ya kujenga bila kibali ilhali hujakamatwa na ulienda mwenyewe manispaa kupeleka maombi ya kibali cha ujenzi?
 
Kabla ya kuanza ujenzi unatakiwa kwenda kuomba kibali cha ujenzi.

Ambapo utaweza kupewa kibali cha awali cha ujenzi ili kuendelea na hatua hata kabla ya kupewa kibali cha ujenzi husika.

Kwa nilikuelewa unastahili kulipa faini.

Nitumie ujumbe whatsapp; +255 752 752 413 711

Majina yangu; Aliko Musa
 
Back
Top Bottom