Kimei alaani mauaji ya kijana Octavian, ataka haki itendeke na kuwatuliza wananchi

MTANZANIA620

Member
Jun 20, 2023
38
45
TAARIFA YA KIFO CHA NDG OCTAVIAN HUBERT TEMBA

Mbunge wa Jimbo la Vunjo Mhe Dkt Charles Stephen Kimei amelaani vikali mauaji ya Ndg Octavian Hubert Temba miaka 25-30 toka kijiji cha Komela, kitongoji cha Komela Kaskazini kata ya Marangu Magharibi ambaye anashukiwa kuuwawa na askari wa hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro (KINAPA).

Dkt Kimei amesema kwa muda mrefu sasa mahusiano baina ya wananchi wanaoishi jirani na hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro sio mazuri kutokana na namna watumishi wa hifadhi hiyo hususani askari wa uhifadhi wanavyowatendea wananchi kwa madai ya kwamba wanasimamia uhifadhi endelevu jambo ambalo sio sawa.

Ifahamike kwamba panapotokea moto mlima Kilimanjaro wananchi wa vijiji vinavyopakana na KINAPA ndio wanaobebwa kwenda kushiriki kuzima moto pamoja na madhila wanayokutana nayo.

Mara zote nilizofanya mikutano katika maeneo hayo wananchi wamekuwa wakieleza kuteswa, wanawake kubakwa, kupigwa na hata kunyang'anywa mali zao kwa kudaiwa wameingia kwenye hifadhi au wamevuna miti ndani ya hifadhi madai ambayo hayatoi uhalali wa matendo ya kinyama na kikatili wanayowatendea wananchi wenzetu.

Familia ya marehemu Octavian ilipofuatilia polisi Himo na Kituo kikuu Moshi Mjini walijulishwa kuna mwili wa mtu anayedaiwa kujinyonga ndani ya hifadhi ya KINAPA ambao polisi wameuchukua na kuupeleka hospital ya KCMC.

Familia ikamjulisha diwani wa kata hiyo Mhe Filbert Shayo ambaye alitushirikisha ofisi ya Mbunge na taarifa zikamfikia Mhe Dkt Charles Stephen Kimei ambaye alishauri Familia ikautambue Mwili kama ni wa kijana wao pamoja na kuukagua kuona kama una majeraha ya kuashiria kushambuliwa (physical torturing). Familia iliridhia na OCD alitoa ushirikiano kwa Familia na ikafanikiwa kufika mochwari KCMC na kuutambua mwili ni wa kijana wao, katika kuukagua wanadai ulikuwa na jeraha linalodhaniwa alipigwa risasi kichwani na wala shingoni hakukua na alama ya kujinyonga kama walivyoelezwa awali.

Familia ilitoa mrejesho kwa haraka sana mamlaka za kiserikali kwa maana ya mkuu wa wilaya alijulishwa pamoja na Mbunge ambaye alimjulisha Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Anjela Kariuki ambaye alimhakikishia hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wote watakaobainika kusababisha mauaji hayo ambayo yanachafua taswira ya uhifadhi pamoja na utalii wa Nchi yetu.

Mpaka sasa zipo hatua kadhaa zimechukuliwa ikiwemo askari wa uhifadhi waliokuwa doria usiku huo kuwekwa chini ya ulinzi huku jeshi la polisi likiendelea na taratibu zake za kiuchunguzi.

Dkt Kimei amesisitiza uhifadhi endelevu hauwezi kujitenga na mahusiano mazuri na jamii. Matukio ya kikatili kama haya ya mauaji, ubakaji na hata kutesa wananchi kwa dhana ya kukabiliana na uvamizi ndani ya maeneo ya hifadhi au kukabiliana na ujangili haukubaliki kwani ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

Wanyamapori na misitu tuliyojaliwa nchini kwetu ni zawadi toka kwa Mungu tuvitumie kwa maendeleo yetu na vikawe neema kwetu badala ya vilio, hofu na mateso kwani hiyo ni laana.

Dkt Kimei ameendelea kuwasihi wananchi wawe watulivu wakati huu ambao serikali inaendelea na taratibu za kisheria pamoja na kuitaka serikali kuhakikisha haki inatendeka, utaratibu wa uhifadhi endelevu uzingatie mahusiano mazuri na jamii zinazopakana na maeneo yanayohifadhiwa.

Serikali imelipokea jambo hili kwa uzito mkubwa na haki itaonekana kutendeka.

IMG-20240511-WA0023.jpg
 
Ila polisi ni majanga sana sijui Huwa wanasomea nini huko chuoni ni aibu wanajitia yaani wameuchukua mwili wa marehemu wameupeleka na hospital kabisa baadae wanawataarifu ndugu zake kwamba marehemu kajinyonga na ndugu wanapopewa nafasi ya kumkagua mpendwa wao wanakuta ana jeraha la risasi kichwani.

My country people .
 
Ila polisi ni majanga sana sijui Huwa wanasomea nini huko chuoni ni aibu wanajitia yaani wameuchukua mwili wa marehemu wameupeleka na hospital kabisa baadae wanawataarifu ndugu zake kwamba marehemu kajinyonga na ndugu wanapopewa nafasi ya kumkagua mpendwa wao wanakuta ana jeraha la risasi kichwani.

My country people .
Ifikie mahali familia ziamue kuwasusia polisi miili wakae nayo huku taratibu nyingine zikiendelea
 
Mtanikumbuka 😂
Huyo mtanikumbuka ndo aliyebariki na kurasmisha mauaji ya namna hii.

Katika hifadhi ya kisiwa cha rubondo kule chato kuna watu wengi wameuawa kipindi cha utawala wake na hao maaskari wa TANAPA kwa kupigwa risasi, kufungwa kamba kwenye mawe na kuzamishwa ziwani au kuchimba mashimo na kuzikwa wakiwa hai (mkikamatwa kundi mnachimba kaburi la pamoja kisha mdogo kuliko wote anawazika mkiwa hai, yeye anaachiwa kufikisha tu ujumbe kwenye jamii ili jamii iwe na hofu na kuacha) japo bado haikuwa mwarobaini.

Pale Burigi-Chato (kama alivyoiita mwendazake)cases za mauaji sikuzisikia, ila watu wanapata ulemavu (physically & mentally) kwa vipigo huku baadhi wakijifia baada ya miezi/miaka michache. Wanawake kubakwa ni kawaida sana.

Serikali inatakiwa kupambana vilivyo na maadui wale watatu (ujinga, maradhi na umasikini) ili kuboresha maisha ya wananchi, wawe na fursa za kuboresha vipato vyao. Badala yake imechagua kutumia nguvu nyingi akili kidogo kwa kupambana na wananchi wenyewe ambao hukosa fursa halali za uhakika na kuamua kuzifuata zile ambazo ni haramu zenye malipo mazuri.

Matokeo yake itaendelea kuwaua wananchi tu na matokeo hayatokuwa chanya.
 
Back
Top Bottom