Kilango sasa awageukia akina Slaa

Fundi unanitupa? MWFK umechokoza nyuki!

Qualify maana weka mipaka. Ainisha vizuri isije wote hapa tukaonekana tumemsifia. Sikusema Fidel80 amesema "wote tumemsifia," ila alichosema kinaweza kutafsiriwa hivyo, ni sentensi tata.

Ndio maana nilikuuliza swali fupi tu la a-qualify kwa nini?

Walimsifia. Alimsifia na nani? Sisi wote au yeye Mwafrika Wake Wa Kike? Sasa wewe Bonnie tueleze Clyde alikuwa anamaanisha nini? j/k

Una hakika kabisa kuwa mimi ni mmoja wa waliomsifia, hata kama tukiwa ni wawili tu - mimi na Fidel, basi hii inatosha kabisa kuweka wingi kwenye maandishi yake. Angesema wote ningekuelewa lakini yeye alisema tu- na sio wote tu-

qual·i·fy

1 a: to reduce from a general to a particular or restricted form : modify ...d: to limit or modify the meaning of (as a noun)

Merriam-Webster Unabridged Dictionary

Get it? LOL!

Sioni kama hii imesaidia chochote kile kwenye argument yako...

Get it?
 
ccm inadatisha kwa kweli.....mama kilango katika kwenye mpigania haki ya mtanzania hadi kwenye mtetea chama cha mafisadi in one week!
kweli linalosemwa ndani ya nec kwa mbunge wa ccm ni amri isiyopingika. msimamo wa chama ni msimamo wa chama kwa yoyote yule. na msimamo wa ccm sasa ni kusafisha wale walioshutumiwa kuwa mafisadi.
 
... hata kama tukiwa ni wawili tu - mimi na Fidel, basi hii inatosha kabisa kuweka wingi kwenye maandishi yake. Angesema wote ningekuelewa lakini yeye alisema

"Tulimpongeza" ina maanisha wawili au mia mbili. Au members wote hapa, mpaka kina Brutus- ambao huwa hawasemi ila wanapo come out of the woods kufanya brutality!

Qualify -kama kamusi ilivyotuambia, sawa na jinsi nilivyo itumia - maana yake weka mipaka.

Mlimpongeza wewe na nani? Na MWFK au wote hapa?
 
"Tulimpongeza" ina maanisha wawili au mia mbili. Au members wote hapa, mpaka kina Brutus- ambao huwa hawasemi ila wanapo come out of the woods kufanya brutality!

Na hiki ndicho alichomaanisha hapa, yaani kuna mtu zaidi ya mmoja hapa amempongeza mama Kilango. Angeanza kutaja majina space isingetosha lakini kutumia uwingi ilikuwa sawa.

Qualify -kama kamusi ilivyotuambia, sawa na jinsi nilivyo itumia - maana yake weka mipaka.

Mlimpongeza wewe na nani? Na MWFK au wote hapa?

Wewe mwenyewe unakiri na umeleta tafsiri kuonesha kuwa qualify ni kulimit. Yeye hakujumuisha wote ila ametumia wingi. Wingi sio lazima umaanishe wote, get it?
 
Inside information, amesema kuwa alinukuliwa vibaya na kwa lengo maalum,ila aliahidi kuwa anaweza kutoa maelezo juu ya kile alichosema.

Lets give her another chance if she was genuine......will let you know soon.
 
No chances...!
Tunajua nini kifanyike waache ujinga!
Wakamate hao MAFISADI MARA MOJA!
Mbona mnatuletea ze comedy?
Mnataka kuliingiza taifa kwenye janga gani?
 
Fundi unanitupa? MWFK umechokoza nyuki!

Qualify maana weka mipaka. Ainisha vizuri isije wote hapa tukaonekana tumemsifia. Sikusema Fidel80 amesema "wote tumemsifia," ila alichosema kinaweza kutafsiriwa hivyo, ni sentensi tata.

Walimsifia. Alimsifia na nani? Sisi wote au yeye na Mwafrika Wake Wa Kike? Sasa wewe Bonnie tueleze Clyde alikuwa anamaanisha nini? j/k

qual·i·fy

1 a: to reduce from a general to a particular or restricted form : modify ...d: to limit or modify the meaning of (as a noun)

Merriam-Webster Unabridged Dictionary

Get it? LOL!

Hapana, Mkuu! Nilijua hautaniangusha! Haya,Mama Afrika, mimi sikuwemo, Kuhani hakuwemo. Pengine Mheshimiwa angetutoa katika hilo jumuisho mambo yangekuwa poa.
 
Hapana, Mkuu! Nilijua hautaniangusha! Haya,Mama Afrika, mimi sikuwemo, Kuhani hakuwemo. Pengine Mheshimiwa angetutoa katika hilo jumuisho mambo yangekuwa poa.

Jumuisho ni lipi, Angesema wote basi angetakiwa kuwatoa nyie. Lakini akisema wengi (kwa kutumia u-wingi) sidhani kama ni lazima awatoe nyie.

Najua kuna tofauti kubwa sana kati ya wengi na wote kama hili nalo linahitaji ufafanuzi unaweza kusema.
 
FMES,Mwanakijiji,FMES,Kuhani Mkuu, Fundi Mchundo, jmushi1,....

..alipohojiwa na Mwanakijiji Mama Malecela alikuwa hajui hata tofauti ya Apartheid regime na yanayojiri ktk Tanzania ya leo.

..then a month later anaibukia Bungeni na ku-invoke philosophers like Socrates etc etc. i felt something was not right.

..lakini hata ukirudi kwenye mahojiano yake na Mwanakijiji, pale Mama Malecela anapodai kwamba CCM haina matatizo wenye matatizo ni mafisadi, ni lazima ukubali kwamba huyu Mama Malecela wants to eat her cake and have it.

..the best case scenario ni kwamba hoja ya EPA ni hoja nzito na Mama Malecela has no intellectual and strategic capacities to follow it through. at worst inawezekana Mama Malecela ni msanii tu, mwanasiasa mwenye hoja na mitizamo kama za Tambwe Hiza.

NB:

..nadhani lipitishwe azimio la kumuomba radhi jmushi1 "dogo." basically the kid saw this coming. lakini alipotuonya wengi walimshambulia na kumuita majina
 
ccm inadatisha kwa kweli.....mama kilango katika kwenye mpigania haki ya mtanzania hadi kwenye mtetea chama cha mafisadi in one week!
kweli linalosemwa ndani ya nec kwa mbunge wa ccm ni amri isiyopingika. msimamo wa chama ni msimamo wa chama kwa yoyote yule. na msimamo wa ccm sasa ni kusafisha wale walioshutumiwa kuwa mafisadi.

Gaijin,

Trust me CCM to its adherents is more like a religion. It is now a conglomerate of individuals that has tentacles in every sphere of influence in the political and social landscapes of Tanzania. What drives dictators (like Mugabe) Ithe world over is what is driving CCM in and out of Tanzania. Think of the mushrooming CCM branches in places like UK and far-off countries like India. To its worshipers, CCM is first then Tanzania second full stop.

When it comes to controversial issues that affect the millions of our fellow countrymen, CCM applies what I call preemptive political strikes. People like Ana Kilango will come and wriggle their way into the minds some of us and like blind fools we will feel the elephants tail and be convinced that jumbo is just a flexile rod!! Like Shakespeare said "it's all sound and fury signifying nothing".

CCM is beyond repair and again quoting Shakespeare "even all the perfumes of Arabia cannot clean CCM's bloody hands". Anybody connected to CCM is a potential FISADI unless he/she gets out. Ana Kilango is one such person and how I wish we could be discussing something else (tears!!).
 
... yaani kuna mtu zaidi ya mmoja hapa amempongeza mama Kilango. Angeanza kutaja majina space isingetosha lakini kutumia uwingi ilikuwa sawa.

Qualify ni kuondoa generalities kwa ku limit ulicho kisema.

Haimaanisha ulikosea au uorodhesha wote waliosema hicho kitu. Qualify ina maanisha chomekea kaneno hapo katakako modify hicho kitenzi ili kuondoa utata. Jiongelee mwenyewe na kundi lako.

Alitakiwa aseme hivi: "Mama Kilango baadhi yetu tulimpongeza."

Hiyo ndio maana yake mtu akikwambia qualify sentensi yako.

Ukisema "tulimpongeza" inaweza kumaanisha wewe na yeye wawili au kila member hapa, na hata wakimya kina Brutus, ambao wakiibuka from the woods, ni kwa nia moja tu, kufanya Brutality. Sasa Mama Kilango hapa jamvini has been a divisive figure. Sio fair kumuongelea kana kwamba wote tunamkubali huyu Mama.

Labda niwe brief ndio utaelewa.

Bado hakuna kosa kwenye alichosema... yeye alisema tuli- na hakusema wote tuli-, katika hili kosa ni lipi?
 
Gaijin,

Trust me CCM to its adherents is more like a religion. It is now a conglomerate of individuals that has tentacles in every sphere of influence in the political and social landscapes of Tanzania. What drives dictators (like Mugabe) Ithe world over is what is driving CCM in and out of Tanzania. Think of the mushrooming CCM branches in places like UK and far-off countries like India. To its worshipers, CCM is first then Tanzania second full stop.

When it comes to controversial issues that affect the millions of our fellow countrymen, CCM applies what I call preemptive political strikes. People like Ana Kilango will come and wriggle their way into the minds some of us and like blind fools we will feel the elephants tail and be convinced that jumbo is just a flexile rod!! Like Shakespeare said "it's all sound and fury signifying nothing".

CCM is beyond repair and again quoting Shakespeare "even all the perfumes of Arabia cannot clean CCM's bloody hands". Anybody connected to CCM is a potential FISADI unless he/she gets out. Ana Kilango is one such person and how I wish we could be discussing something else (tears!!).

Ndugu mag3 maneno yako ni mazito.
Mchango wako ni muhimu hapa...Tuendelee!
 
Jamani kuna member wapya hapa wenye maneno mazito...Na sasa wacha wakate issue ili heshima ya forum iendelee!
NO TIME TO WASTE WANDUGU.
 
Labda niwe brief ndio utaelewa.

Bado hakuna kosa kwenye alichosema... yeye alisema tuli- na hakusema wote tuli-, katika hili kosa ni lipi?

Sikusema alikosea. Aliombwa aanishe. "Tuli"mpongeza ikiachwa inaelea elea hewani inaweza kutafsiriwa kwamba kulikuwa na consensus, kwamba ilikuwa ni conventional wisdom ya jamvi, kwamba kakubalika hapa. Ukweli ni kwamba Mama Kilango hapa amekuwa a lighting rod, a divisive figure. Baadhi ya watu mmemwimbia sifa, lakini wengine wamemkataa, kwamba ni msanii wa CCM.

Nimeona nirudie rudie maneno yenye maana ile ile labda utaanza kupata picha.
 
Bado hakuna kosa la kutumia tuli- kama unamaanisha kuwa kuna mtu zaidi ya mmoja aliyefanya hivyo.

Kama lipo liseme wakati pia ukikiri kuwa umefanya makusudi kuweka neno wote kwenye maandishi ya fidel wakati unajua kabisa kuwa hakuliweka.
 
Kitila Mkumbo JF Senior Expert Member Join Date: Sat Feb 2006

Re: Kilango sasa awageukia akina Slaa

Kitu ambacho wengi tunashindwa kukipata ni kwamba mama Kilango na wabunge wote ni wanasiasa na hivyo wana upande. Mwanasiasa makini siku zote atajaribu kuonyesha kwamba upande aliopo upo sawa na upande wa mpinzani wake haupo sawa.

Sasa katika hili, pamoja na hoja zake nyingi kufanana na wapinzani, binafsi sikutarajia kwamba mama Kilango angefika mahala awasifie wapinzani na akiponde chama chake. Mama Malecela thus far amefanya kazi yake vizuri as mbunge wa Same na CCM. Ametetea wananchi wake wa Same na watanzania kwa ujumla na wakati huohuo amehakikisha kwamba anabaki CCM na anakitetea chama chake.

Sasa katika vita hii ya ufisadi, lazima kuna kuzidiana katika kuonyesha nani ni adui, nani mpiganaji na nani kamanda wa hayo mapambano. Ningeshangaa sana kama wabunge wa CCM wangekaa kimya na kukubali kwamba kamanda wa mapambano ya ufisadi ni wapinzani. Malecela, mke wake na wabunge wengine wa CCM wanaodai kwamba mapambano ya ufisadi yameanzishwa na wao CCM wapo sawa kisiasa na wangekuwa ni wajinga sana kisiasa kama wangekiri kwamba kweli yameanzishwa na wapinzani.

Kuna mkakati ambao sasa hivi unaendelea ndani ya CCM kuhakikisha kwamba wanateka hoja ya ufisadi na kuifanya kuwa ni ya kwao. Ndio maana of recent wabunge wa CCM wameanza kuwa wakali kwenye hili jambo. Na ndio sababu kubwa ya kukataa kurusha moja kwa moja hotuba ya Dk Slaa. Sasa as opposition na wale ambao ni activists inabidi kulielewa hili jambo vizuri. We have to understand that politics is always about strategies, some of them clean and some of them dirty. Unfortunately the only strategy available to CCM is the latter.

Sasa ni kazi yetu wapinzani kuendelea kupigana na hii vita ya ufisadi na kuhakikisha kwamba ukamanda wa mapambano haya ya ufisadi tunaendelea kubaki nao. Tukizubaa CCM watatupiku na ukamanda utachukuliwa na akina Anna Kilango na ikija 2010 wao ndio wataonekana kwamba ndio waliokuwa wanawatetea zaidi wananchi kuliko sisi.

Hata hivyo so far naona kwamba Dk Slaa amefanya kazi nzuri sana kwenye ile hotuba ya juzi japokuwa ilifichwa ili wananchi wasiione.
 
Mchezo mchafu huo FMES KAWAELEZE WAKUU WAKINA KIKWETE MBONA HAWAKUSIKILIZI?
Waeleze jamani waachane na mambo ya chama na wahangaikie maslahi ya taifa!
Wawatose mafisadi la sivyo chama kinakufa hicho na tunakoelekea sijui.
 
Mkuu Kitila,

Heshima mbele, unajua ndio maana huwa ninakufagilia sana nikiongea au kukutana na wakubwa wa taifa letu, tena hii siri sijawahi kukwambia mkuu, mara kwa mara huwa ninakufagilia sana maana huwa ninawaambia kwanza unaignia hapa kwa jina lako la kweli, na ni moja tu na iso siri huwa ninawamabia mpaka shughuli yako kimaisha, maana kwa analysis kama hii, ndio tunaweza kuelewa maana ya neno siasa, au mwanasiasa,

Naona kwenye hii topic kuna mpaka waliojaribu kuazima English ili waonekane tofauti kumbe ni wale wale tu yaani kenge kwenye msafara wa Mamba,

Mkuu Kitila, hapa JF tunahitaji watu wenye kuelewa siasa mna kuona mbali pia kama wewe, ambao wanaweza kuona taifa kwanza, baadaye vyama na viongozi binafsi, heshima mbele mkuu kwa mwendo huu nina imani kuwa tunaweza kuamini kuwa mabadiliko kwa taifa letu mbele ya safari ni guranteed kwa kuwa na viongozi wenye akli ya kuona mbele na mbali kama wewe!

FMES-Sauti Ya Umeme!
 
Mchezo mchafu huo FMES KAWAELEZE WAKUU WAKINA KIKWETE MBONA HAWAKUSIKILIZI? Waeleze jamani waachane na mambo ya chama na wahangaikie maslahi ya taifa! Wawatose mafisadi la sivyo chama kinakufa hicho na tunakoelekea sijui.

Mkuu Mushi,

Heshima mbele kaka, CCM inapitia majaribio makuu ya kidemokrasia, ambayo imekuwa ikidai siku zote kuwa inaaamini sana, sasa tunajionea kwa macho kuwa baadhi ya viongozi wetu huwa ni waongo, lakini mkuu kama unaelewwa historia ya mapinduzi na ukombozi wa wananchi, basi utaona kuwa pole pole tunaelekea kunakotakiwa, na ni lazima ianzie na CCM kwanza,

Mafisadi wamefika mwisho sasa, lakini hawezi wakakubalia bila a fight, lakini CCM iko sawa wala haina maneno, maana ilikuwepo kabla ya kina Lowassa na wenzake, lakini maneno yako ni mazito mkuu ninayaweka.
 
Back
Top Bottom