Kila unalotakiwa kujua kuhusu IPTV (kuangalia TV kwa kutumia internet)

Mkuu nimechimbua hadi huko SS lakini hakuna inayoonyesha, kama kuna VPN unatumia tuelekeze nasi tupate hizo SS

Hapo ulipofika ndo penyewe..sijui...labda ni tatizo la network ya line unayotumia..sio mtaalam sana mm ila mi natumia vodacom na wakat wa mechi huwa inaonyesha vizuri tu
 
Mimi natumia zantel 3G maana ndiyo ina bundle zenye unafuu kidogo pia inastream hadi hd 720P bila ya kuloga.
ngoja niweke bundle ya buku voda nicheck kama zitafunguka.
 
kamanda hzo janga sema jamaa anakufcha tu hazioneshi...mm mwenyew hvyo hvyo natumia galaxy note 3 line ya vodacom lkn wap...nmetest had kwa washkaj hvyo hvyo akuambie ukwel tu

Ahaaaa!!
Hakijaharibika kitu maana kuna bein sports,sky sports etc so mziki unachezeka
 
Tumezoea katika maisha yetu tukiangalia Tv basi huduma ile tunaipata kupitia madishi, cable au antenna. siku zinavyosogea mbele na technology ndivyo inavyokuwa na ndio jinsi madish na antenna vinavyopitwa wakati. leo kwenye uzi huu tutaangalia IPTV.

Ni nini hii IPTV?
IPTV ni kifupi cha Internet Protocal TeleVision. Hii ni aina ya uangaliaji TV kupitia mtandao wa internet ambapo kituo cha TV badala ya kutumia satelite dish au cable wenyewe wanarusha matangazo kwa internet.

Unawezaje kuangalia IPTV?
Utahitaji kifaa chenye internet na uwezo wa kustream ili kuweza kuangalia kama vile smartphone, tablet, laptop, desktop hadi TV zenye internet zinaweza kustream.

Internet yenye speed gani inahitajika?
Internet yoyote hata ya edge inaweza kustream ila iwe na latency nzuri, zipo stream zinahitaji speed ya 200kbps tu (25KBps). Kama una latency ndogo hata internet iwe na speed vipi huwezi kustream live utastream tu vitu ambavyo si live. Kujua zaidi kuhusu latency nenda thread hii
https://www.jamiiforums.com/tech-ga...iwa-na-download-speed-kubwa-ndio-mzuri-2.html

Je software gani inatumika kustream hizo TV?
Kikawaida browser yenye flash au html5 inaweza kustream tv lakini ukitaka kustream vizuri zaidi software kama VLC au KODI ni muhimu. Kutokana na uhaba wa links za VLC nitazungumzia zaidi jinsi ya kutumuia KODI kuangalizia IPTV.

KODI ni nini?
KODI ni software (media centre) ambayo hutumika kuubadili muonekano wako wa simu uwe kama TV na kuweza kuenjoy TV unazotumia na inapatikana kwenye simu, tablet, computer hadi TV.
Kodi-devices-smudged.jpg


Kuidownload nenda website yao hii hapa chini, ni bure haiuzwi
Downloads | Kodi

Nikishadownload kodi nini kinafuatia?
Utahitaji ku install plugin ili uweze kuangalia TV online. Click video add on halafu chagua watchmojo, install halafu ifungue tuone kama itafanya kazi.
9vW4MHp.jpg


KODI imefanya kazi, je siwezi angalia mpira na vipindi vyengine?
Unaweza angalia mpira chanel unayotaka kuanzia za ki-Africa kama Super sport, za Ulaya kama Sky sport, za Asia kama Bein sport hadi za kimarekani kama NBC cha muhimu uwe na plugin (add ons) husika, hizi plugin za mpira na michezo mengine zinapatikana tu internet mfano mimi plugin yangu ninayotumia inaitwa Vdtube25 ina channel nyingi sana kuanzia mpira hadi movie.
zNbDtYR.jpg

PppArCw.jpg


Hio hapo juu sky sport 3

Uzuri wa hizi plugin za kodi zipo TV ni HD na nyengine ni full HD kabisa hivyo internet yako tu.

Malipo?
Kila kitu kuanzia juu hadi hapa ulipofikia ni bure hutoi pesa, ila hizi plugin za bure haziaminiki zipo za kulipia ambazo hazikati ovyo. Mimi sijawahi kulipa natumia tu bure ila kama unahitaji service nzuri zaidi unaweza kulipa ila pia kuwa makini na matapeli

Tutorial ya kuweka na mahala pa kupatia plugins
Plugin yangu ninayotumia ya vdtube25
https://seo-michael.co.uk/how-to-install-vdubt25-add-on-kodi-xbmc

Website hio hio pia utapata plugins nyingi.

Kama una swali lolote usisite kuuliza chini

Mkuu chief mkwawa ubarikiwe tena na tena kwa huu uzi mzuri, na nimejilizisha kama kitu ni live kwa kuiangalia tv ya arijazila kwenye laptop na king'amuzi nikakuta Habari ni ileile.
 
Haujakosea kitu kitu rudi tena video then add on utaona ile add on yako ipo (imeshakua installed) iclick itafunguka na kuonesha video zake

Sasa hivi nikifungua inasoma hivi kwanza. Na shida ingine nataka kuzipata chanell za movies kam WB,HBO nk
 

Attachments

  • 1439373139901.jpg
    1439373139901.jpg
    32 KB · Views: 219
Shukrani zimwendee mleta uzi, solution n Nini kwenye tatizo la kuplay muvi afu unasikia sauti tu huku picha haionekani. .?
 
Sasa hivi nikifungua inasoma hivi kwanza. Na shida ingine nataka kuzipata chanell za movies kam WB,HBO nk
Itakuwa hio add on inataka add on nyengine kufanya kazi.

Hbo ipo kwenye add on nyingi tu, sina pc hapa nkuangalizie ila nafkiri hata kwenye phoenix unaipata hebu test kuieka phoenix
 
Itakuwa hio add on inataka add on nyengine kufanya kazi.

Hbo ipo kwenye add on nyingi tu, sina pc hapa nkuangalizie ila nafkiri hata kwenye phoenix unaipata hebu test kuieka phoenix

Mkuu nimeiona HBO kwenye phoenix Asanteh sana na vipi taratibu za kuweka add on nyingine ni kama alivyoelekeza mkuu uludodi au vipi?
 
Last edited by a moderator:
kamanda hzo janga sema jamaa anakufcha tu hazioneshi...mm mwenyew hvyo hvyo natumia galaxy note 3 line ya vodacom lkn wap...nmetest had kwa washkaj hvyo hvyo akuambie ukwel tu

Kwa nn niwafiche..wakti mi sifaidiki na chochote hata nikikudanganya...mkuu kwangu inaonyesha,sijui kwenu tatizo ni nn,labda mwenye uelewa ataelezea baadae...niliwahi kupost kwa nn supersport 3 niliyonayo inaonyesha mechi na za kwenye decorder hazionyeshi.mechi...nilichogundua ni kuwa iliyopo kwenye kodi ni hd japo quality yake ni standard quality...mkuu endelea kujaribu...nilipweka israeltv mara ya kwanza,trace urban ilikataa kabisa ila siku kadhaa mbele ilionyesha,nakusihi kuwa mvumilivu au tafuta ushaur kwa watu wenye uelewa zaid
 
Kwa nn niwafiche..wakti mi sifaidiki na chochote hata nikikudanganya...mkuu kwangu inaonyesha,sijui kwenu tatizo ni nn,labda mwenye uelewa ataelezea baadae...niliwahi kupost kwa nn supersport 3 niliyonayo inaonyesha mechi na za kwenye decorder hazionyeshi.mechi...nilichogundua ni kuwa iliyopo kwenye kodi ni hd japo quality yake ni standard quality...mkuu endelea kujaribu...nilipweka israeltv mara ya kwanza,trace urban ilikataa kabisa ila siku kadhaa mbele ilionyesha,nakusihi kuwa mvumilivu au tafuta ushaur kwa watu wenye uelewa zaid

barida kamanda wangu nmekusoma ngoja nijarbu jarbu kibish coz kwangu inaload tu
 
Kaka hapo sasa sijui tatizo ni nn,hebu tafuta ushauri kwa watu wenye uelewa zaidi hasa mleta uzi

uko sawa mkuu INNOMATIX mimi mwenyewe nilipata tatizo kwenye add on ya Pak india live before ilikua haifunguki lakini baada ya siku kadhaa nilipofungua kodi ikafanya updates yenyewe tu ikaanza kuonyesha .,
hata kwenye hizo supersport na mimi napata tatizo hilo hilo so ngoja nivute subira labda zitaonekana siku zijazo kama kweli wewe unazipata
 
Last edited by a moderator:
Chief Mkwawa,Njuwa Mavoko,asanteni kwa taaluma mliotupatie,kwangu nimefata hatua zote na kufanikiwa,isipokuwa kwa Vdubt25 ukifungua haioneshi channel yeyote na Paki india live ukifungua zinaonesha channel zoe ila ukiclip to play baada ya sekunde kadhaa inadisplay massegi hii PLAYBACK FAILED.Error check the log for more information. sijui tatizo ni nini,ila Phoniex inaonesha vizuri tu
 
Back
Top Bottom