Kila Mtanzania anayeingiza kipato kwa kufanya kazi alipe kodi. Hakuna cha misamaha kwa viongozi wakiwemo wabunge kwani wote tunahitaji huduma bora

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,617
6,833
Watanzania wote wenye umri kuanzia miaka 18 walipe kodi zote kwa kazi wanazozifanya kihalali Kuanzia Rais na viongozi wengine wote pamoja na wastaafu wanaopata mishahara ya asilimia ya 80% ya walio madarakani.

Pasiwe na misamaha ya kodi kabisa. Kiongozi anapata msamaha wa kodi, halafu anawekewa mazingira mazuri na marupurupu kibao, haya maendeleo na huduma bora zitapatikana vipi kwa watanzania wote?!


View: https://youtu.be/Pqr5DnSfPr4?si=cSe0t18D0kO0aCFE
 
Tz analipwa vzr ndie asilpa kodi why?__
Mtu yuko na mshahara more 10M+ alip kodi bado ana posho na allowance za kutosha bado gari amepewa na mafuta + dereva + bima
Hili nazan wao nao wawe wazalendo kulpa kodi , (kiongoz bora ni yule anaongoza mfano)

Mishahara yao ikatwe Kodi,
 
Wanakuja wakali mnoo yakiguswa maslahi Yao alafu wanatushawishi Sisi walipa Kodi Tuwe wazalendo Kwa kulipa Kodi.
 
Wabunge wanakatwa kodi kwenye salaries zao ila wamejipigia pande kwenye posho za vikao na perdiem za kukaa Dom kwa sababu hizo hazikatwi kodi.
 
Wanakuja wakali mnoo yakiguswa maslahi Yao alafu wanatushawishi Sisi walipa Kodi Tuwe wazalendo Kwa kulipa Kodi.
Ina umiza sana watumish wa chin unakuta analpwa 300,0000/- hadi lak 1,000,000/- salary slip inamakato ya hadi 30% ya mshahara wake na hana allowance yoyote
 
Wabunge wanakatwa kodi kwenye salaries zao ila wamejipigia pande kwenye posho za vikao na perdiem za kukaa Dom kwa sababu hizo hazikatwi kodi.
Hv n kweli m-mbunge anakwatwa kodi Tz ?!
 
Mishahara yao inakatwa Kodi,,lakini marupurupu amabyao ni mengi hawalipii.Mshahara wa mbunge umeandikwa million 2 kwa mwezi lakini akiweka na marupurupu kabla ya allowance za safari wanapata million 20 kwa mwezi
 
Kila ukinunua Luku kila mwezi wanakata si ndionkodi hizo au
 
halafu mwalimu ambaye mshahara kiduchu, hana malupulupu yoyote wala kiinua mgongo chake cha miaka ya utumishi hakilingani na cha mbunge cha miaka mitano anabeba mzigo wa kodi kibao na michango mara ya mwenge mara sijui ya nini.
Mambo mengine yanashangaza sana.
 
Watu hawawezi kuwa na uzalendo wa kulipa Kodi kubwa alafu matumizi yakawa ya hovyo mifano ni mingi,34b kutengeneza makubusho ya maraisi,500b kununua magari ya kifahari,200b kulipa Wabunge wa vitu maalum nk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…