Ngumu kumeza
JF-Expert Member
- Jun 19, 2012
- 577
- 354
Kama vipi mkuu inabidi ajiongeze awe rubani manake anapenda mambo ya kuwa angani muda mwingi.
Namuona mhe Rais mstaafu JK na mkewe mama Salma kupitia Bukedde TV anahudhuria kuapishwa Museveni huko Uganda.
Jee atakuwa kaenda kwa gharama za serikali hii hii inayotuaminisha inabana matumizi kwa kuhakikisha safari za muhimu tuu ndio zinagharamiwa? Hii ni kwa vile kwa nafasi yake kama rais mstaafu hawezi kwenda kwenye shughuli hiyo kibinafsi kama vile anavyokwenda Lindi ukweni kuwasalimia.
Serikali mbona haisimamii kauli zake? Anaogopwa?