Kifo cha David Balali: Kauli mbalimbali toka kwa watanzania

Kuhani Mkuu,
Swali no moja tu kwako: Kama sentenso yako ya mwisho ni kweli, ni muda mrefu sana kuanzia Januari 16 hadi Mei 16 alipofariki marhemu. Mbona USA hawakufanya kitu?
 
..HUUU HAUKUWA WAKATI MUAFAKA
..KWA HILI IMEONESHA AKILI YA MEMBE NA JK ZINAFANANA....YAANI WATU WANAOONGEA ALAFU NDIO WANAFIKIRI..SIJUI WANAITWAJE WATU WA HIVI!!!....MAANA UTAGUNDUA KAULI YA JK PIA NI YA KUTAPATAPA .KWA KUSEMA ...NI KAZI YA MUNGU!!!!....KWANI MWENYE MAMLAKA YA ROHO ZETU SI ANAJULIKANA NI MOLA!!....ANGEWEZA KUONGEA KIVINGINE..

KWA KAULI HIZI BASI NA HALI YA MAMBO ILIVYOKUA HADI ANAFARIKI..UKIFANYA UCHAMBUZI WA HARAKA UTABAKIA NA JIBU MOJA NALO NI; KIFO CHA BALALI SI CHA KAWAIDA!

Wanaitwa wakurupukaji.
 
Mimi nafikiri tuendelee mbele lakini uchunguzi wa kifo pia ufanyike.
Kwasababu we can all see kuwa kifo kinaweza kuwa related na uchunguzi wa EPA.
Uchunguzi wa kifo usipofanyika itawatia hofu wazalendo wengine kwani sasa kama mtu anaweza kuuwawa halafu hakuna kinachofanyika then tusitegemee kuna mabadiliko yatakayotokea kwasababu hii itaendeleza nidhamu ya woga miongoni mwa wazalendo.
 
Kuhani Mkuu,
Swali no moja tu kwako: Kama sentenso yako ya mwisho ni kweli, ni muda mrefu sana kuanzia Januari 16 hadi Mei 16 alipofariki marhemu. Mbona USA hawakufanya kitu?

Kweli hapo kuna mashaka na ndio maana balozi alisema eti hawezi kusema nyendo za mtu aliyeko marekani.
Inawezekana kama alioa mke mwenye uraia ama geen card then aka file upya na hivyo kuwa na haki ya kusubiri matokeo bila deportation.
 
Kuhani Mkuu,
Swali no moja tu kwako: Kama sentenso yako ya mwisho ni kweli, ni muda mrefu sana kuanzia Januari 16 hadi Mei 16 alipofariki marhemu. Mbona USA hawakufanya kitu?

Kwa sababu:

1) Marekani haigongi kila Mlango inatafuta illegal aliens.

2) Extradition ni mpaka uombwe na Tanzania. Tanzania haikuomba Ballali arudishwe.

U.S. Ready to Help Govt Find Ballali

The Citizen (Dar es Salaam)
20 May 2008

The United States yesterday declared that it was ready to help the Government establish the whereabouts of former Bank of Tanzania governor Daudi Ballali.

US embassy spokesperson Jeffery Salaiz told The Citizen:"We are ready to assist the Government to establish where Dr Ballali is we can do that anytime.

"The problem is that so far nobody from the Government has lodged special request with the US embassy asking us to help in tracing the former governor. "If they haven't made an official request it will be very difficult for us to do anything about Dr Ballali...But we can get him if he is still there."" Mr Salaiz said.

Angalia walivyo kuwa na usongo waombwe kumkamata Billali. Wanasema 'tatizo hatujamombwa....' Tatizo! Tena, angalia mtu wangu, wanasema hatujui alipo lakini tukitaka tatampata mara moja. Yani hata Sheriff akitatufa Jambazi huwa hasemi ana hakika atampata. Hawa yani ni kama wanasema huyu cha mtoto, tuambieni twende tuka mng'ang'anie. Ni procedure za Kimataifa lazima wazifuate.

Na Serikali ya Kikwete ikijua hivyo, haikusema nyo wala nywi. Ikakaa kimyaaaaa!
 
Tumeshajiuliza kama Ballali alioa mke mwenye green card ama uraia?
Maana if thats the case then mjadala huu utaishia kuwa inawezekana alifile for green card kwa kutumia mke mpya aliyemuoa mwenye either green card ama uraia.
Na kama that was the case then alikuwa na haki ya kutokuwa deported kwasababu hakukuwa na mtu aliyepinga maombi yake ya green card(ie serikali).
Kwahiyo akawa tayari ana haki ya kusikilizwa shauri lake bila kuwa deported.
Hivyo kama kuna anayejua kama jamaa alioa then mchezo umeisha.
 
Tunachotakiwa tufanye labda ni kuitaka serikali iwape wamarekani green light ya kutupa data zote!
Hapo ndio kwenye mgogoro..Serikali ibanwe ili itoe rhuksa kwa wamarekani kuprovide details zote wanazozijua.
 
Ndiyo tatizo lako wewe la kutaka kutetea hata visivyostahili kutetewa. Kifo cha Ballali kina utata mwingi sana hasa ukichukulia jinsi alivyoondoka nchini mpaka alipofariki. Inakuwaje mtu aliyewahi kushika nafasi za juu serikalini afariki dunia lakini Watanzania watangaziwe baada ya siku tano tangu kifo kitokee tena kwa kupitia gazeti binafsi? Sirikali ilifahamishwa lini kuhusu kifo cha Ballali na ni nani aliyewahamisha na kwanini waliamua kukaa kimya baada ya kufahamishwa juu ya kifo hicho? Inakuwaje mtu mkubwa kama Ballali azikwe nje ya nchi.

JK amesema kifo cha Ballali ni kazi ya Mungu, lakini bila kufafanua zaidi. Usiri mkubwa juu ya Ballali tangu alipoondoka na kama siri kali ilikuwa inajua amelazwa hospitali ipi na alikuwa anaumwa nini na kwa nini sirikali haikuweka jitihada za kumuhoji akiwa hospitalini ndizo zinazua speculation chungu nzima. Na waswahili husema, panapofuka moshi.....

unajua saa nyingine frustrations zikizidi ni vizuri utulie tu na ukubali yaliyojiri ! Sasa kifo cha Ballali ndio umlaumu Kada ?? Mimi nimesema nilichotaka kusema just like you said what you had to say ! Ndio maana nikasema watu wanatumia kifo cha Ballali kama "PRODUCT PLACEMENT". Ona sasa hata Mbowe nae keshaanza kujitafutia umaarufu kutokana na hiki kifo ! Kama nyinyi mnamsupport Mbowe kwa aliyosema kutokana na hiki kifo, basi itakuwa vizuri zaidi kama mtatanguliza doubts zenu mbele kwanza na tujue kama ni viable au la ! Lakini up to this point, sijaona chochote cha maana alichosema mbowe !

Unajua ile thread niliyoandika ni rasmi kuanzia leo jumapili ilikuwa inagusa nini mzee ? i bet you dont ! kuhusiana na doubts zangu zilizomo kutokana na hiki kifo cha ballali !
 
Another pack of bullshit from our Press. Wanasema muuaji huyu hapa lakini hawajataja. Kama ile list ya watu wa EPA ikla mtu anaifahamu, sasa labda watuambie tuwasaidie kujaribu kufigure out nani kati ya hao ni muuaji (Which i am sure JF knows), au nani hasa ndio EPA. Mjadala wa EPA utakapoingia bungeni na watu kuanza kuijadili hoja na ripoti ndio tutawekewa jina wazi. Sasa hivi kuna papa wawili watatu ambao wanaotakiwa kuvuliwa baharini ili waonekane kwa watu.
Na really MR EPA na wengine wataonekana. Subirini tu sipo Mramba atakapoingia kikaangoni, hapo ndio mnaweza kuanza kupata picha nyingine.
Lakini ukiangalia vizuri statement ya Membe kusema Serikali haihusiki na kifo cha Balali, inaonesha kuwa it was not a natural death, and not kazi ya Mungu kama JK alivyosema, it is the work of someone in Tanzania. NI confession kuwa kuna mwingine aliyehusika na huyu mtu jina lake linafahamika litatajwa wazi within weeks right here where people dare to talk openly.
 
Kauli ya Mbowe ni mwanzo mzuri endapo atashinikiza uchunguzi ufanyike na wauaji waunganishwe moja kwa moja na EPA huku wakitakiwa pia kuface death penalty kwa kifo hicho cha Ballali.
Na hii iwe mara baada ya wao kurudisha pesa.
 
viza ya mtu inapokuwa revoked huko Us unaondoka hapo hapo siku hizi toka September 11, tunawajua wengi waliorudi hapo hapo, hasa kule Texas, yaani Dallas.

Bosi wangu FMES, sio kweli kwamba visa ikiwa revoked basi unatakiwa uondoke hapo hapo. Unapewa 90 days window ya kujipanga na mambo mbalimbali. Moja ya issue ambayo unaweza kuifanya ndani ya siku hizi 90 ni kukata rufaa na kuomba immigrantion court wasikilize kesi yako. Otherwise, unatumia muda huo kukusanya kilicho chako na kuambaa zako nyumbani kwenu.

Hivi ndivyo system ilivyo kabla na baada ya 9/11. Period.

Sasa kama kuna watu unawajua waliondoka mara baada ya visa zao kutemwa, basi ni wao wenyewe tu waliamua kutimua masaa machache baada ya kutaarifiwa hivyo. Lakini ukweli ni kwamba, wangeweza kukaa kwa siku 90 kabla hawajakwea pipa kurudi bongo.......unless, walikuwa na extensive criminal record.
 
wee hujui wanasiasa wa bongo ?? mbowe kaongea ili nae aonekane kwenye kundi la mamba hata yeye (kenge) yumo ! lakini ona kama atatilia mkwazo !
 
Kwani jamani Balali hajafanyiwa autopsy? Na kama hajafanyiwa ni kwa nini? Maana sasa naona wote tumeachwa dilemma na swala zima.

Membe anasema serikali haijamua Dr.Balali, jee kwa nini yeye akusema kwamba Balali amekufa na nini? At this moment kuna consipirancy nyingi sana na moja wapo ni kuuliwa na serikali, it will be like that untill proves otherwise.
 
Unajua this is sad, ni kifo gani duniani ambacho sio kazi ya Mungu? Hivi huyu mkuu anaelewa kuwa haya yanayoendelea katika taifa letu yana-accomplish one thing, and one thing only nacho ni kuendelea kuishusha hadhi ya serikali yake ambayo tayari iko kwenye life support?

Ni taifa na serikali gani duniani inayoendeshwa namna hii? Gavana wa benki kuu anaondoka nchini, halafu anatumiwa watu wa kumchunguza, baadaye anafariki ghafla, serikali inajaribu kuomba kuhudhuria mazishi lakini inakataliwa, and then hata serikali yenyewe haina uhakika na kifo cha a former Gavana wake wa Benki kuu ya taifa? Halafu hata pale ilipothibitisha bado inahangaika kujisafisha kuwa haihusiki na hicho kifo?

Yaani hii serikali haisikii aibu, wala huzuni? Serikali imeshatamka kuwa Balali amefariki, lakini hadi ninapoongea wakuu wakubwa wa taifa wanatusumbua na simu ili tuwathibitishie kama ni kweli amefariki, it is very sad indeed!


Wakubwa hapa pana siri gani maana inaonekana watu humu ndani wanajua sana kinachoendelea kuhusiana na Balali kuliko JK au kama anavyojua JK. Sasa mtupashe basi na sisi tuone kama ni Mchele au Pumba alizokuja nazo jmushi kuhusiana na Message za ZABA SEARCH.
 
Hii issue ya suala la status la marehemu kweli linachanganya.

Kwa uelewo wangu, hauwezi ku-hold more than one viza in the U.S. Sasa iliwezekana vipi kwa marehemu ku-hold some sort of a visa, yet kuwa U.S. GC holder?

GC is an 'immigrant visa', while all other visa are categorized as 'non-immigrant visa.' Na once mtu aki-upgade to immigrant visa (GC), then the other non-immigrant visa aliyokuwa nayo inakuwa automatically dissolved.

Kwa hiyo kama Ballali alikuwa na GC, then hakuwa na haja ya yeye kuwa na U.S.visa ya aina nyingine yeyote.

Sasa kama ubalozi wa U.S. waliishu statement ya ku-revoke visa ya Ballali iliyokuwa stamped kwenye passport, then we know one thing for sure .....hakuwa GC holder. Kwa sababu, GC haiwi stamped kwenye passport......ila inatengenezewa ki-ID card chake.

By the way, mtu huwezi kuwa raia wa nchi fulani halafu yet ukawa na visa ya nchi hiyo. For what? I mean, visa is used merely for entry permit. Sasa kama wewe ni raia, then why would you need a visa to enter your own country? It just doesn't make any sense!

Wala ishu haichanganyi. Umeipatia vizuri. Rationale uliyotumia hapo ni ya nguvu, rahisi na inatosha. Lakini hata hivyo mi facts ya kuku back up hii hapa mtu wangu:

Tanzania: U.S. Ready to Help Govt Find Ballali

The Citizen (Dar es Salaam)
20 May 2008

... the US ambassador to Tanzania, Mr Mark Green, denied rumours that Dr Ballali was a US citizen. Mr Green said the US government had not made any decision on deporting Dr Ballali to Tanzania because the Tanzanian government had not requested for his extradition.

Challenged to explain how the American government could revoke someone's visa without kicking them out, Mr Green said they could not "go knocking on every door looking for illegal immigrants".

"A citizen of the United States of America is not required to apply for a permit to enter the country. Ballali is not an American citizen," he said.
 
What I want to know are the answers to these few simple questions:

1) Logic (as according to Spin Doctor Salva Rweyemamu) tells us Balali was a 'private citizen', no longer a civil servant. If that indeed was the case, what was the reason for the alleged 'late' Balali's family to contact the Government of Tanzania, PRIOR TO announcing the news of his death? Huh?

2) Ok, so there is a will that declares that Balali should be buried in the US. Is Balali a US citizen or Tanzanian citizen? Normally, one gets buried in their homeland. If he was a US citizen, why then did the Government give him such a strategically important job as the CENTRAL BANK GOVERNOR? Something stinks here!

3) Has anyone seen the will? See, if he did get buried in the US, who amongst us has witnessed (if ever) the funeral proceedings? How are we to verify that indeed it was Balali being sent back to the ashes... dust to dust? Bado haijatulia hii!

Asanteni, nasubiri majibu!
 
Kauli ya Mbowe ni mwanzo mzuri endapo atashinikiza uchunguzi ufanyike na wauaji waunganishwe moja kwa moja na EPA huku wakitakiwa pia kuface death penalty kwa kifo hicho cha Ballali.
Na hii iwe mara baada ya wao kurudisha pesa.
Mbowe na wenzake kama walishindwa kushinikiza Bunge kumruhusu mbunge wa chama chao kuhudhuria vikao basi usitegemee kwenye hili wanaweza kushinikiza chochote. Jinsi anavyozungumza kisanii utaona tu kuwa na yeye anaishi kwenye dunia ya speculations tu.

Mbowe ni mtupu wa fikra pevu ila ana macho makali.
 
*Watoa siku 30 wahusika kujisalimisha Luganga
*Waomba serikali iwaletee mchanga wa kaburi


Na Francis Godwin, Mufindi

WAKATI mwili wa aliyekuwa gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Dkt. Daud Ballali umezikwa Washington, Marekani Ijumaa iliyopita, baadhi ya wazee wa kabila la Wahehe wamekuja juu na kutoa siku 30 kwa yeyote aliyehusika kwa njia moja ama nyingine na kifo hicho, kujisalimisha kijijini Luganga, Mufindi mkoani Iringa alikozaliwa gavana huyo.

Wazee hao kutoka kijiji cha Luganga na Mtwango, wameiomba serikali ifanye uchunguzi wa kina juu ya kifo hicho na kufanya kila linalowezekana kuresha mwili huo nchini, ikishindikana ilete mchanga wa kaburi hilo ili wafanye mazishi ya kimila.

Wakizungumza na Majira jana kwa niaba ya wenzao, Mzee Samweli Kalinga (76) na Yohanes Kalinga (85), walisema wataamini kuwa mtoto wao amekufa baada ya kupata ufafanuzi wa kina kupitia kauli ya Rais Jakaya Kikwete kuhusu kifo hicho.

Walisema wao kama wazee wa siku nyingi wa kijiji cha Luganga na Mtwango, wanashindwa kuamini kuwa mtoto wao amekufa, wataamini jambo hilo baada ya kuona maiti au picha yake akiwa amekufa.

Mzee Samweli alisema taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari hazitoshelezi kuamini kuwa ni kweli mtoto wao kipenzi, Dkt. Ballali amekufa hivyo ameiomba serikali kuunda tume haraka kuchunguza mazingira ya kifo cha gavana huyo wa zamani.

Alisema moja ya sababu inayowafanya waendelee kuamini kuwa Dkt. Ballali bado mzima ni mazingira ya sasa ya nyumbani kwao kijijini Luganga na nyumbani kwa baba zake wadogo eneo la Ziroziro, Mtwango.

" Nimeishi Mtwango tangu utoto wangu sijawahi hata siku moja kuona nyumba yenye msiba haina waombolezaji", alisema Mzee Samweli

Alisema kwa mujibu wa taratibu za kihehe, msiba unapotokea huombolezwa siku tatu mfululizo ama zaidi ambapo kwa muda huo, majirani hukusanyika nyumbani kwa wafiwa kuwafariji.

Alisema inawezekana ni kweli, Dkt. Ballali amekufa kama ilivyothibitishwa na baadhi ya ndugu zake lakini wao kama wazee wakihehe, wanasubiri serikali itoe taarifa rasmi ya kina ikiambatana na uchunguzi kamili wa kifo hicho.

"Tunaomba kuelezwa ugonjwa uliosababishia kifo cha mtoto wetu na jitihada zilizofanywa na serikali kuokoa maisha yake... Tunashindwa kuelewa serikali inapotoa pole wakati iliwahi kusema Ballali hajulikani alipo", alisema Mzee Samweli.

Kwa upande wake Mzee Yohanes alisema wanafanya mpango kukutana na ndugu wa marehemu kufanya tambiko la aina yake la kifo hicho na kuomba dua maalum kulaani kifo hicho kama kimetokana na 'mkono wa mtu'.

Mzee huyo, alisema wametoa siku 30 kwa watu waliohusika kwa njia moja ama nyingine na kifo hicho kujisalimisha kijijini hapo, vinginevyo watu hao hawatadumu kwenye nyadhifa zao.

Alisema iwapo kifo hicho kimetokana na mapenzi ya Mungu basi wanamshukuru kwa kutimiza matakwa yake na kama ni kwa mipango ya shetani na wanadamu, basi itashughulikiwa ipasavyo.

Pamoja na mwili huo kuzikwa Marekani, wazee hao wameiomba serikali kufanya kila linalowezekana kuurejesha nchini, ikishindikana waletewe mchanga wa kaburi lake ili wafanye mazishi kwa mujibu wa mila za kihehe, Luganga alikozikwa baba yake mzazi Mzee Timoth Ballali aliyefariki dunia Aprili 3 mwaka 2000.

" Hata kama imeshindika kuleta mwili wake basi wasafirishe mchanga wa kaburi tuje tufanye mazishi kwenye makaburi ya Luganga alipolala baba yake mzazi. Kumzika Marekani ni sawa na kumtenga na familia yake", alisema Mzee Yohana.
http://majira.co.tz/kurasa.php?soma=tanzania&habariNamba=6779
 
Last edited by a moderator:
kama mwanasiasa mbowe ningemshangaa kama angenyamaza kimya!
kwenye siasa hakuna nafasi ya kupoteza time ya kufanyia chama kampeni....hata kama kwa blah blah!
mbowe nakupa hongera kwa kusema kama mwanasiasa, japo kuwa nimezichukulia kuwa ni blah blah
 
Kada nilikwambia mwanzo mwa mwaka huu kuwa huu mwaka wa ukombozi na mtakuwa na hali ngumu sana kwani kila siku yataibuliwa mengine mengi, washauri waache kusema uongo kwanza, the watueleze kwanini walificha balali alikuwa anaumwa nini, alilazwa hospitali gani, alikufa lini, na kwanini hakurudishwa nyumbani kwa mazishi. Usimlinganishe balali na watu wengine balali alikuwa gavana na alikuta mtuhumiwa mkuu wa EPA.
 
Back
Top Bottom