Kibatala wewe ni wakili mzuri na msomi lakini punguza majivuno na dharau dhidi ya mamlaka

1979Magufuli

JF-Expert Member
Feb 20, 2023
454
1,800
Huwa navutiwa sana ninaposikia Kibatala anamtetea mtu, nimeanza kukufuatilia kitambo sana uwezo wako kisheria na kweli umenifanya hata mimi nipende kusomea sheria, Wakili msomi Kibatala, mimi nimeshuhudia mawakili wengi wasomi kuliko wewe, mfano marehemu Dkt.Masumbuko Lamwai, Herbet Nyange, Mosses Maira, Mabere Nyaucho Marando, Professa Abdallah Safari nk.

Nilikuwa nashinda Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwasikiliza mabingwa hao tu wakiwakilisha watu mahakamani, miongoni mwa mawakili waliobaki ni huyu msomi Majura Magafu.Huyu ni bingwa kuliko wewe Kibatala.

Kwanza kwenye roll of advocates nadhani Magafu ni senior kwako, lakini hata hivyo nimekuwa nikikuona sana Kibatala ukiongea kwa kebehi sana dhidi ya serikali.Kwa mfano leo katika kesi ya Boniface na Malisa unasoma hati ya mashtaka mbele ya waandishi wa habari kwa majivuno ukisema unawasubiri hao waliokuwa wakifanya press yaani Jeshi la Polisi na utaomba waitwe mahakamani ili uweze kuwahoji.

Ukaongea kwa kebehi eti nanukuu, " Tutaomba pia hao ambao mwanafamilia amesema ni jeshi waje pia kutoa ushahidi." mwisho wa kunukuu.

Maneno hayo ni ya dharau, kebehi na majivuno, huko serikalini kuna wanasheria wasomi kuliko wewe, kwanza unavyojifanya mjuaji naona kama unawatafutia balaa hao washtakiwa wawili, kesi ni ushahidi na ushahidi kuwa washtakiwa wametenda kosa ushahidi dhidi yao utathibitishwa mahakamani na hao unaowapa matumaini utawasababishia matatizo.

Wewe kujua sheria haina maana kuwa Jacob na Malisa hawawezi kuwa behind the bars, nakusihi sana Bro, navutiwa sana sana sana na uwezo na kipaji ulichonacho kisheria lakini sio sawa kuwa mjivuni, kudharau mamlaka kwa sababu tu una itikadi za Chadema.

Sasa Jamhuri itakupangia mawakili wa saizi yako na huyo Jacob atakonda mwenyewe baada ya mwezi.
 
Huwa navutiwa sana ninaposikia Kibatala anamtetea mtu, nimeanza kukufuatilia kitambo sana uwezo wako kisheria na kweli umenifanya hata mimi nipende kusomea sheria, Wakili msomi Kibatala, mimi nimeshuhudia mawakili wengi wasomi kuliko wewe, mfano marehemu Dkt.Masumbuko Lamwai, Herbet Nyange, Mosses Maira, Mabere Nyaucho Marando,
Mimi Kibatala nilianza kumpenda kipindi alikuwa namtetea mh Mbowe kwenye kesi ya ugaidi ,mulitaka kumnyonga Mwamba nyie maswine.
 
Huwa navutiwa sana ninaposikia Kibatala anamtetea mtu, nimeanza kukufuatilia kitambo sana uwezo wako kisheria na kweli umenifanya hata mimi nipende kusomea sheria, Wakili msomi Kibatala, mimi nimeshuhudia mawakili wengi wasomi

Sasa Jamhuri itakupangia mawakili wa saizi yako na huyo Jacob atakonda mwenyewe baada ya mwezi.
Hili ni onyo kubwa toka kwa wazee. Kama ana akili basi atazingatia lasivyo ….
 
Huwa navutiwa sana ninaposikia Kibatala anamtetea mtu, nimeanza kukufuatilia kitambo sana uwezo wako kisheria na

Sasa Jamhuri itakupangia mawakili wa saizi yako na huyo Jacob atakonda mwenyewe baada ya mwezi.
Mkuu,
Ukimtoa wakili msomi tundu lisu anae mfuatia Ni kibatala..

Na kwa taarifa yako hao walio kutuma watalala na viatu..

NB.
Kama unaona kibatala anafaidi haukatazwi na wewe uende ukawe wakili msomi
 
Huwa navutiwa sana ninaposikia Kibatala anamtetea mtu, nimeanza kukufuatilia kitambo sana uwezo wako kisheria na kweli umenifanya hata mimi nipende kusomea sheria, Wakili msomi Kibatala, mimi nimeshuhudia mawakili wengi wasomi uyo Jacob atakonda mwenyewe baada ya mwezi.
Hakuna dharau wala kebehi hapo wewe ni mjinga tu hujui haki za raia na wajibu wa mwanasheria.

Kama tuna tatizo Tanzania basi tatizo hilo ni kwamba wanasheria wetu si wakali vya kutosha, hawana kebehi za kutosha, hawana dharau za kutosha.
 
Huwa navutiwa sana ninaposikia Kibatala anamtetea mtu, nimeanza kukufuatilia kitambo sana uwezo wako kisheria na kweli umenifanya hata mimi nipende kusomea sheria, Wakili msomi Kibatala, mimi nimeshuhudia mawakili wengi wasomi Jacob atakonda mwenyewe baada ya mwezi.
kuna wasiwasi wasiwasi mkubwa hawa ndugu washtakiwa wapotoshaji wakakosa kupata haki zao za msingi kwa majivuno, ubishi na ujuaji usio kua na tija wa wakili wao 🐒
 
Back
Top Bottom